Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
1. Amemteua Bw. Kenan Laban Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi, Bw. Kihongosi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Bw. Kihongosi anachukua nafasi ya Dkt. Yahaya Ismail Nawanda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
2. Amemteua Bw. Elias Daniel Mwandobo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba. Kabla uteuzi, Bw. Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais Ikulu.
3. Amemteua Bw. Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Bw. Magala anachukua nafasi ya Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
4. Amemteua Bw. George Hillary Herbet kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi, Bw. Herbet alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Uapisho wa Mkuu wa Mkoa na Msajili wa Mahakama ya Rufani utafayika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
====
Pias soma: MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi