Mkuu wa Mkoa Tabora azindua Mradi wa Maji uliogharimu Tsh. Milioni 975

Mkuu wa Mkoa Tabora azindua Mradi wa Maji uliogharimu Tsh. Milioni 975

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-06-05 at 17.04.42_96df0d1c.jpg
Tarehe 04/05/2024 Mkuu Wa Mkoa wa Tabora, Paulo Matiko Chacha amefanya ziara katika Wilaya Uyui Jimbo la Igalula katika Kata za Tura, Kigwa na Igalula.

Akiwa katika ziara hiyo ameambatana na Mkuu Wilaya ya Uyui, Zakaria Mwansasu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daud protas, katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amefanya kazi zifuatazo;

Kata ya Tura, Mkuu Wa Mkoa amezindua Mradi wa Maji uliogharimu kiasi cha Tsh milioni 975, Mradi Huu umekamilika kwa asilimia 100.

Baada ya uzinduzi huo, Mkuu Wa Mkoa alifanya mkutano wa hadhara Kwa lengo la kusikiliza Kero za wananchi.
WhatsApp Image 2024-06-05 at 17.04.43_ad472a4c.jpg

WhatsApp Image 2024-06-05 at 17.04.53_4bbee6ff.jpg

WhatsApp Image 2024-06-05 at 17.04.50_cfa9769c.jpg

Kata ya Kigwa Mkuu wa Mkoa alifanya ukaguzi Mradi wa kupeleka Maji ya Ziwa Victoria katika Kata za Kigwa, Goweko, Igalula na Nsololo unaogharimu kiasi cha Tsh Bilioni 11 Mradi upo kwenye asilimia 65 ya utekelezaji mpaka Sasa, baada ya hapo Mhe Mkuu Wa Mkoa alifanya mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero za Wananchi.

Kata ya Igalula, Mkuu wa Mkoa alipokea mifuko simenti 3200 zilizotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa lengo la kujenga Shule mpya ya msingi itakayogharimu kiasi cha milioni 400, baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa alifanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero.

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Igalula, Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daud Protas anamshuru sana, Rais Dkt Samia Hasan Suluhu kwa kuleta miradi mikubwa katika Jimbo la Igalula.
 
Back
Top Bottom