Mkuu wa mkoa wa Arusha hiyo nafasi imekupwaya, nakushauri uwaachie wengine

Mkuu wa mkoa wa Arusha hiyo nafasi imekupwaya, nakushauri uwaachie wengine

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vipi!

Binafsi sijawahi kumsikia huyu mkuu wa mkoa wa Arusha akiongelea suala la machinga.

Ila mara kwa mara wamekuwa wakisikika wakuu wa mikoa wa Dar-es-salaam ndugu Amos Makalla na Mwanza.

Ila huyu wa Arusha amerelux kama mkoa hauna wamachinga kabisa.

Kwa waliopo Arusha na ambao wameshafika Arusha mtakuwa mashahidi mji wa kitalii ulivyogeuka kuwa kichaka, nikimaanisha vibanda vichafu vimeenea kila mahali mpaka sura ya mji wa Arusha umepotea.

Juzi mzungu mmoja aliporwa pochi maeneo ya France kona kisha vibaka wakapotelea kwenye hizo vibanda vya machimga nakutokomea kusikojulikana.

Huyu mkuu wa mkoa wa Arusha sijui hata anaitwa nani kwa majina, anaonekana ni mtu mdhahifu na muoga katika suala zima la kufanya maamuzi.

Amekaa ofisini machinga wamechafua mji umeharibika. Wafanyabiashara wakubwa wanaolipa kodi wanapungua kwasababu ya hawa machinga.

Aisee unamuogopa Gambo ndio amekuteua. Jiamini acha uoga.

#Viva# Amosa Makalla!
 
Na mbunge nae ni kikwazo sababu anataka kura lakini jijini kama Arusha halipaswi kua kama kichaka
 
Alitakiwa astaafu kulinda heshima, maana hata Mwanza alinusurika kupigwa chini, lakini ung'ang'anizi wa madaraka na kushibisha tumbo ndio tatizo kwa viongozi wa kitanzania
 
Hiyo ni kazi ya mkurugenzi wa jiji, mbunge na madiwani, kuita rungu la mkuu wa mkoa ni kwamba hao watu wameshindwa kazi......
 
Mbona kama Chai inakuwa nyingi sana kwenye hili suala la wamachinga ?
 
Albert Chalamila walimtumbua bure tu kwa kumwonea lkn ni mtu makini na asiyeogopa mtu.sipati picha kwa nn Mh SSH alimtumbua lkn huyo wa arusha hauwezi huo mkoa ni mgumu sana bora angeachwa Kafulila lkn si Mwongela lkn hata hivyo karibu mikoa mingine yote wamachinga bado wako barabarani tu wanapeta.njoo huku kwetu BK barabara zote wamachinga waamefurika and nobody cares.business as usual.
 
Hata huku tunduma machinga wako Road kama kawa! Upande wa Chalamila isikusumbue kichwa mama alikuwa anapanga safu yake ya mazuzu!
 
Arusha kumekua kuchafu sana kwasababu ya hao machinga
Wamachinga hawasababishi uchafu ila serikali ni ya kizembe kubaki na miundo mbinu ya kizamani; tazama stendi kuu ya mabasi Arusha ni ya tangu enzi za viford wakati mtoto wa hayati Sokoine akipiga debe pale baada ya kuhitimu kidato cha sita ni aibu tupu.

Eneo lote lililo magharibi mwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid lilikuwa ni tupu likiwa na vichaka na mazalia ya panya buku hadi mji mpya.

Watu wanaongezeka ;lakini haliongezeki na wenye mamlaka wapo tu hawataki kupanua maeneo ya mji ili iwe rahisi kuwahamisha
 
Albert Chalamila walimtumbua bure tu kwa kumwonea lkn ni mtu makini na asiyeogopa mtu.sipati picha kwa nn Mh SSH alimtumbua lkn huyo wa arusha hauwezi huo mkoa ni mgumu sana bora angeachwa Kafulila lkn si Mwongela lkn hata hivyo karibu mikoa mingine yote wamachinga bado wako barabarani tu wanapeta.njoo huku kwetu BK barabara zote wamachinga waamefurika and nobody cares.business as usual.
Tena cha ajabu ni bora huyo Chalamila kuliko aliyeko Dar kwa sasa kutwa kucha vitisho, tambo, majivuno na mipango dhaifu
 
Mwisho.wa Machinga Arusha ni Jumatano...kuanzia kesho wameambiwa waondoke kwa hiari...

Wamepewa 72 hours...
 
Hapana naona huyu mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkurugenzi ni watu makini na wanaojua majukumu yao. Hao viongozi sio watu wa kiki au kutafuta sifa, watu wa mipango na mambo yao Huenda kimya kimya na sahihi.

Kwa sasa miundombinu ya kuwaweka wamachinga imekwisha kamilika (Kilombero, Mbauda nk) na nadhani kwanzia Kesho wanaanza Kupewa maeneo hayo mapya. Leo nilikuwa mjini na nimekutana na magari yakitangaza utaratibu huo.

Tatizo la jiji la Arusha ni aina ya mbunge tuliyenaye kwani yeye hupenda kujiona mtetezi wakati ndiye problem maker (Rejea alipomuwa RC na mgogoro wake zidi ya dc)
Tatizo linguine ni aina ya madiwani wengi hawana uwezo (elimu ndogo)

Itoshe kusema jiji la Arusha linawategemea sana Mkurugenzi, DC na RC
 
Nakumbuka siku ya uzinduzi wa chanjo ya covid Arusha pale AICC, daa hii nchi basi tu!.
 
Back
Top Bottom