Mkuu wa Mkoa wa Geita, Kiongozi pekee wa Serikali aliyekuwepo kwenye ibada ya Kumuombea Magufuli leo Kanisani

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Kiongozi pekee wa Serikali aliyekuwepo kwenye ibada ya Kumuombea Magufuli leo Kanisani

Hakuna binadamu mwenye mema matupu asiye na mabaya ni Mwenyezi .Mungu tu

Binadamu yeyote ana mema yake na mabaya yake akiwemo Magufuli na awaye yeyote

Asante wale walioenda wamewakilisha kukumbuka walau yale mema alifanya sababu ana mema yake pia alifanya

Asante kwa huo uwakilishi walau unakumbusha kuwa marehemu Magufuli aliwahi pia kuwa na mema yake ambayo yalifanya watu wanyonge walie mabarabarani jeneza likipita

Wenye nacho hakuna aliyeanguka wala kuzimia wala kuangua kilio kikali wanyonge ndio walianguka na kuzimia kwa maelfu hata kufa kwa kukanyagana kuaga mpendwa wao
Vp kuhusu Sabaya? Mbona ni kama niliona chozi lake jicho moja
 
Na nyie mnajiendekeza,mtu alishakufa utakaa kuzunguka makaburini ndo unamrudisha?familia yake ikimkumbuka inatosha,eti alikuwepo kiongozi mmoja huyohuyo anatosha bwana.
Pumzika kwa amani JPM
Tuache kukuza mambo madogo,nyie huko mnakowazika ndugu zenu huwa mnaenda kuwaombea kila mwaka?.Narudia familia yake ikimkumbuka inatosha,wao ndo wana stable(strong) bond na marehemu.
Hawezi kupumzika kwa amani kwa uovu alioufanya kwa nchi hii
 
Wengi wao ni kama wamekwama sehemu flan ya maisha yao na sasa kisirani chote wanakipeleka kwa Marehemu.Mtu ana zaidi ya miaka miwili hayupo Duniani,unashangaa mtu 24/7 anamtukana.Ni aina flan ya msongo wa mawazo unaoendana na kukata tamaa ya maisha.
Mbona Mkapa watu hawakumsema kwa mabaya japo ana mabaya pia, jiwe alikuwa zaidi ya shetani
 
Hata Hawa nao itakua hivyo hivyo
Sawa, na hivyo ndivyo inavyotakiwa! Marehemu Mkapa katika uhai wake alipenda kunukuu maneno ya wimbo wa kale wa dansa: "mtoto wacha kulia, waache watu waone wenyewe". Mwenyewe alikuwa kiongozi bora sana na aliyeheshimika nchi nzima. Lakini hakukubali hata kidogo kusifiwa licha ya kutukuzwa. Baada ya kufa hakuna raia wanaohangaika kujua lini alifariki na nini kinafanyika kumkumbuka; hilo ni suala la familia. Tofauti kabisa na huu umaarufu wa wanasiasa mbilikimo wa kulazimisha mpaka kumbukumbu ya kifo! Pathetic!
 
Hakuna binadamu mwenye mema matupu asiye na mabaya ni Mwenyezi .Mungu tu

Binadamu yeyote ana mema yake na mabaya yake akiwemo Magufuli na awaye yeyote

Asante wale walioenda wamewakilisha kukumbuka walau yale mema alifanya sababu ana mema yake pia alifanya

Asante kwa huo uwakilishi walau unakumbusha kuwa marehemu Magufuli aliwahi pia kuwa na mema yake ambayo yalifanya watu wanyonge walie mabarabarani jeneza likipita

Wenye nacho hakuna aliyeanguka wala kuzimia wala kuangua kilio kikali wanyonge ndio walianguka na kuzimia kwa maelfu hata kufa kwa kukanyagana kuaga mpendwa wao

Hao wanyonge mbona maisha yao hayakubadilika, au wao wameumbwa kuwa wanyonge tu? Na dhalimu alikuwa na kipaji cha kuhadaa watu wamuone mtu mwema, wakati alikuwa muovu tu.
 
Hao wanyonge mbona maisha yao hayakubadilika, au wao wameumbwa kuwa wanyonge tu? Na dhalimu alikuwa na kipaji cha kuhadaa watu wamuone mtu mwema, wakati alikuwa muovu tu.
Kawaulize kwa nini walimlilia vile aliwafaa lipi?
 
Mungu ambariki RC Martin Shigella na viongozi wengine walioonesha mshikamano na upendo kwa kumbukizi ya mwamba na fimbo chungu kwa majizi ya CCM, CDM, ACT na baadhi ya viongozi serikalini wenye maadili potofu kwa maslahi yao binafsi.

Kidogo kidogo sahani zitameguka

Zitameguka kwa ajili ya yule dhalimu?
 
Back
Top Bottom