Major General Peter NKUBA CHIRIMWAMI, mkuu wa jeshi na mkuu wa mkoa wa Kivu Kasikazini, jana tarehe 23 Januari 2025, majira ya saa moja na dakika 44 usiku,alipokuwa amewatembelea wanajeshi wake kuwaunga mkono katika vita na kundi la waasi la M23, alimiminiwa risasi na kufariki hapo hapo.
Baada ya waasi hao kukalia mji mdogo wa SAKE, MONUSCO na SAMIDRC waliamua kuwafuata mjini humo kuwafukuza. Kama ilivyo vitani, hairuhusiwi kufyatulia risasi wanajeshi wa umoja wa mataifa.
Hivyo, baada ya kuwa na taarifa kwamba makundi hayo yatakuja, walijigawa(M23), na kuacha barabara nyeupe. Lakini waliitahadhalisha MONUSCO kwamba ikiachia risasi, na yenyewe itashughulikiwa.
SAMIRDC ambayo imeundwa na Afrika Kusini,Tanzania na Malawi, M23 ilisema yenyewe lazima wazichape. Basi katika uwepo wake kiongozi huyo, huku maeneo yaliyozingira barabara hiyo itokayo Goma kwenda SAKE, ndipo risasi zikaanza kulindima.
Baada ya kifo cha kiongozi huyo, maiti yake haikukamatwa, maana wenzake walimuchukua na kuondoka nae.
Pamoja na hayo, nchi za ugaibuni zimewaomba raia wake waishio mjini Goma kuhakikisha wanaondoka humo, na kwamba msaada wa haraka unaweza tolewa kwa waliopo Kinshasa tu. Siku ya jana,wengi wao walipaki mizigo wakielekea nchini Rwanda.
Mpaka sasa, mapigano yanaendelea.