Mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini auliwa na M23

Mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini auliwa na M23

Rwanda ikemewe vikali na jumuiya ya kimataifa iache kuharibu amani ya Drc.
Shida pale ilipo DRC akishika maeneo nae anatumika na vibaraka wake ndo maana M23 anajikusanyia watu tu anafanya kama anawasaidia na wanawaelewa.....jamaa wasingekua na nguvu kuliko jeshi la serikali kama uraiani mambo yangekua sawa......yani hapo kila mtu anapeleka madini kwa watu wake......akimiliki M23 eneo ana soko lake anapeleka madini tena hukohuko kwa wazungu na wanapata silaha za kisasa kabisa, pia jeshi la serikali likichukua maeneo wanapeleka madini pia hukohuko kwa wazungu sema Drc alichofeli serikali yake ilikua ina base sana na Kinshasa na maeneo mengine ya kati huko huku mashariki akipatelekeza kwa vikundi mbalimbali....na wananchi wa kule wanajua serikali ikichukua maeneo yao ya madini ,,watachimba watauza ulaya na pesa itarudi kuneemesha Kinshasa na matajiri wake
 
Maj Gen anakufaje kizembe hivyo? Tatizo la Africa vyeo vingi jeshini haviendani na uwezo wa muhsika
ukisoma taarifa utagundua majeshi ya kigeni yapo huko kutalii na kuwacholesha majeshi ya serikali , Waafrika tuwatimue hawa na kuchukua migodi na maliasili zote ziwe chini ya Serikali
 
Nchi za Africa hazina uwezo.
DRC ilishatekwa kama Africa yote ilivyotekwa, Kwa sasa ni mali ya walioiteka.
Dunia hii haihitaji huruma ya watu wengine ili usurvive, it's survival of the fittest.

Africa yenyewe yote imetekwa Iko chini ya maharamia, maharamia ndio player wa game all over.

Africa tuna njaa, hatuna nguvu, hatuna akili aka wanasesere.
baada ya kuyajua yote haya bado huna solutiontv , hapo ndo bwana Zanzibar-ASP anawalumu viongoz wa waafrika pamoja na waafrikaya kwa ujumla
 
ukisoma taarifa utagundua majeshi ya kigeni yapo huko kutalii na kuwacholesha majeshi ya serikali , Waafrika tuwatimue hawa na kuchukua migodi na maliasili zote ziwe chini ya Serikali
Kuna msemo alitumia Kagame majuzi, kwamba anajua kuwatambua viongozi na wajinga. Akaongeza kwamba, mjinga akikabidhiwa uongozi, ni janga kubwa. Sasa viongozi wengi Africa wala hawapo kuongoza, ni vibaraka tu. Kuna nchi moja ukanda wa Sahel, eti ilimchagua raisi, nadhani ana miaka kama 90. Unajiuliza kama huyu atalisaidia nin taifa,huku hata kujitawaza inaonekana hawezi.
 
Kiini haswa cha huo mgogoro ni Interahamwe waliokimbilia DRC na kuanza kuua Wanyamlenge, na sasa wanajiita FLDR.

FLDR wanapigana bega kwa bega na Majeshi ya Serikali ya DRC.

Hata hayati Baba wa taifa aliwahi kuongelea huu mgogoro.

Tuache chuki dhidi ya jamii ya Kitutsi.
unawajua watusi kwanza ? huko Rwanda watusi wameua marais wawili wahutu , je nan anamchukia mwenzie ?
 
unawajua watusi kwanza ? huko Rwanda watusi wameua marais wawili wahutu , je nan anamchukia mwenzie ?
Haya, ebu dadavua mambo mzee! Naona unaijua historia vizuri. Lakini ukitoka hapo uende na Burundi.
 
Kuna msemo alitumia Kagame majuzi, kwamba anajua kuwatambua viongozi na wajinga. Akaongeza kwamba, mjinga akikabidhiwa uongozi, ni janga kubwa. Sasa viongozi wengi Africa wala hawapo kuongoza, ni vibaraka tu. Kuna nchi moja ukanda wa Sahel, eti ilimchagua raisi, nadhani ana miaka kama 90. Unajiuliza kama huyu atalisaidia nin taifa,huku hata kujitawaza inaonekana hawezi.
hakika mkuu , bado hatuna reasoning. leaders
 
Hahahahahaha nimeipenda hiyo ndugu. Unadhani M23 kiuharisia ni waasi wenye nguvu ya kulivaa taifa hivi hivi? Hapa inasemekana M23 ina msaada wa Rwanda, Uganda na Kenya. Burundi ilikuwa upande wa DRC, imeshanyoosha mikono na kuondoka. Ripoti ya Umoja wa mataifa, mpaka sasa inasema machimbo ya madini karibia yote yameshakuwa mali ya M23, wachimbaji wanafanya kazi kwa kasi ya ajabu, baada ya kulipwa vizuri. Je, unadhani madini yakiuzwa hawapati pesa? Kuhusu siraha, asikudanganye mtu, hakuna vita visivyo na wafadhili. Wauzaji wa siraha ni wengi, wanachokitaka ni pesa tu. Wamepora siraha nyingi sana, wasaliti jeshini hawakosi. Na ukisikia kwa makini sif za M23,ina snippers na ma Commando wa kutumia tu mikono yao, visu na shoka. Je, hawa watu unadhani ni wa mchezo? Taarifa za chini chini zilizopo, japo kama kweli nchi moja wapo inayohusishwa kama kweli inahusika, kinachosubiliwa ni neno anzeni tu. Maana giza lililopo Goma,inasemekana limetengeneza mazingira ya watu kuingia. Na cha ajabu, kundi la wazalendo, nguo wameshavua na hawataki tena kujihusisha na vita, bado kukabidhi siraha tu.
Hii kuna mkongo aliwahi niambia.

Ukisikia vita mahali ujue wanachimba madini.
 
Haya, ebu dadavua mambo mzee! Naona unaijua historia vizuri. Lakini ukitoka hapo uende na Burundi.
Kote shida ni watusi , kasome historia uone wameua viongoz wahutu mara kadhaa ila wahutu walikuwa kimya , watusi ni kama ccmu , the more unakaa kimya the more wanazid kukuonea , uzur wa watusi wanapenda maendeleo sio kama ccmu
 
hakika mkuu , bado hatuna reasoning. leaders
This time natamani ningezaliwa Burkina Faso basi niwe mkulima ijulikane. Huku ubanwe, kule ubanwe, eti uko kwenye nchi yako na unatakiwa uwe mzalendo, lakini kipaumbele anapewa mchina na mhindi wanaokutemea usoni, ukisema unawekwa ndani. Kwa hii issue ya DRC, inaenda kuibua mengi sana, bila kusahau mzungu kudhalilishwa na ngozi nyeusi hadhalani.
 
Kukubali au kukataa ni ngumu mzee. Mashariki mwa DRC kabla ya mipaka ya wakoloni, na kipande cha Uganda, kulikuwa Rwanda. Mpaka leo, wakazi wa maeneo hayo bado wanaongea kinyarwanda pure kabisa. Na wana ndugu nchini Rwanda. Mganda au Mkongo anaeongea kinyarwanda, huwezi mtofautisha na mnyarwanda wa Rwanda. Kwa hiyo, hata mnyarwanda akiwepo, si rahisi kumtofautisha na wakazi hao wa nchi hizo. Na hiki kimekuwa kitendawili kwa yeyote. Haya nayaongea kama mimi. Serikali ya Rwanda ihusike isihusike, haijulikani. Ila sasa, ukiangalia kinachoendelea pale, hakina tofauti na Russia vs Ukraine. Mataifa mbalimbali yapo, japo kwa inovyoonekana, kuna muasi furani anatembeza kichapo hadi watu wanarukwa na akili.. Hakika nae anapoteza, ila si kwa kiasi kikubwa. Mkongo, Mrundi, wanalia
Hao wanaojifanya wakongo siku kagame na mu7 wakiondoka madarakani ndio utajua uraia wao
 
Kote shida ni watusi , kasome historia uone wameua viongoz wahutu mara kadhaa ila wahutu walikuwa kimya , watusi ni kama ccmu , the more unakaa kimya the more wanazid kukuonea , uzur wa watusi wanapenda maendeleo sio kama ccmu
Kwa hiyo hali ikiwa hivyo unadhani kinatokea kitu gani? Ushabiki huo mi siafikiani nao. Je, mtutsi au mhutu wa chini kabisa asiejua hili wala lile yeye anauliwa ili nini kitokee? Sasa ndo maana huyo mzungu akaona kama majinga yanaweza kuuwana yenyewe, nikomae na mambo yangu yenyewe yaendelee kuwa nyani tu. Je, uliwahi kufuatilia utusi na uhutu ulitoka wapi? Maana usije ukahisi ni makabila ya enzi kama yalivyo mengine ya kibantu!!!
 
Major General Peter NKUBA CHIRIMWAMI, mkuu wa jeshi na mkuu wa mkoa wa Kivu Kasikazini, jana tarehe 23 Januari 2025, majira ya saa moja na dakika 44 usiku,alipokuwa amewatembelea wanajeshi wake kuwaunga mkono katika vita na kundi la waasi la M23, alimiminiwa risasi na kufariki hapo hapo.

Baada ya waasi hao kukalia mji mdogo wa SAKE, MONUSCO na SAMIDRC waliamua kuwafuata mjini humo kuwafukuza. Kama ilivyo vitani, hairuhusiwi kufyatulia risasi wanajeshi wa umoja wa mataifa.

Hivyo, baada ya kuwa na taarifa kwamba makundi hayo yatakuja, walijigawa(M23), na kuacha barabara nyeupe. Lakini waliitahadhalisha MONUSCO kwamba ikiachia risasi, na yenyewe itashughulikiwa.

SAMIRDC ambayo imeundwa na Afrika Kusini,Tanzania na Malawi, M23 ilisema yenyewe lazima wazichape. Basi katika uwepo wake kiongozi huyo, huku maeneo yaliyozingira barabara hiyo itokayo Goma kwenda SAKE, ndipo risasi zikaanza kulindima.

Baada ya kifo cha kiongozi huyo, maiti yake haikukamatwa, maana wenzake walimuchukua na kuondoka nae.

Pamoja na hayo, nchi za ugaibuni zimewaomba raia wake waishio mjini Goma kuhakikisha wanaondoka humo, na kwamba msaada wa haraka unaweza tolewa kwa waliopo Kinshasa tu. Siku ya jana,wengi wao walipaki mizigo wakielekea nchini Rwanda.
Mpaka sasa, mapigano yanaendelea.
Hii habari ni kama sijaielewa.Huyu Makonda alienda kuwatembelea wanajeshi wakiwa field au? na je ina maana aliwazukia jamaa akiwa hana ulinzi?
 
Hii habari ni kama sijaielewa.Huyu Makonda alienda kuwatembelea wanajeshi wakiwa field au? na je ina maana aliwazukia jamaa akiwa hana ulinzi?
Makonda wa drc tena........
 
Kosa kubwa alilofanya DRC, ni kukingia kifua FDLR. Baada ya badhi wao kuhusika na mauaji, walipewa hifadhi, badae wakaanza kufadhiliwa. Eneo lenyewe limekaa kama vile halina mwenyewe, wakaanza kulitawala. Kilichofuata, ni kundi hili kuanza kuwanyanyasa watutsi wa Congo. Hapo ndipo mambo yalianza kuvurugika na kuleta utata. Af ujue, mali ya Congo ilishakuwa mali ya umma. Hivyo hata hao UN ni majizi tu. Bora viongozi waige mfumo wa Burkina Faso, vinginevyo, baada ya Congo, mi naona dalili za nchi nyingine kukumbwa na ghasia ya ukabila tena.
Pakitokea mwamba mmoja dikteta akashkilia kila kitu vizuri Congo ni nchi moja ina rasilimali kinoma. Usimamiz na hii vita ya mda mrefu inawacost.
Naona Jamaa wanatanua mipaka, hawajaishia tuu Kivu
 
Pakitokea mwamba mmoja dikteta akashkilia kila kitu vizuri Congo ni nchi moja ina rasilimali kinoma. Usimamiz na hii vita ya mda mrefu inawacost.
Naona Jamaa wanatanua mipaka, hawajaishia tuu Kivu
Kwani,katika kuzingila Goma, si tayari wapo Kivu kusini? Na Burundi ikaamua wanajeshi wake watoke tu huko! Inaonekana na wao hawajui hatma ya hii vitu. Na kwa mjibu wa vyanzo vya habari,, kuna mwanajeshi mmoja wa Burundi na wanajeshi alionao wameshatiliwa mashaka, hivyo mpango ni kujiunga na M23! Unategemea nini taarifa hizi zikiwa za kweli?
 
Unaigawaje nchi ya watu?
DRC ni mali ya wakongo, vita iishe na ardhi ibakie kwa wakongomani.
Hiyo vita inaweza kuisha ndani ya mwezi mmoja tu ikiwa nchi za Africa kwa umoja wake zikiamua iishe. Tatizo wakuu wa nchi za Afrika wamejaa unafiki.
Upo SAHIHI
 
Huyo Mkuu alikuwa anapigana bega kwa bega na Interahamwe.
 
Back
Top Bottom