Kwahiyo wakigawa Congo ndo amani inahakikishwa?......Find how to co- exit in peace, period.
Jamani, sijui mtu aongeeje.
1. Fuatilia wanavochambana viongozi wa South Afrika wastaafu, wanarudia historia ya mwaka 1885. Hivyo hawaoni sababu ya Ramaphose kupeleka wanajeahi huko.
2. Hawavumi lakini,…………. Rwanda ilisema Congo imefanya jitihada zote kusogeza karibu na mipaka yake kundi la waasi la FDLR. Leo hii Chirimwami alikua kiungo mkubwa kati ya FDLR na Serikali ya DRC. Leo yuko wapi? Omega na jamaa zake wakubwa wako wapi? Mpaka sasa, ni kwamba kundi hilo ni kama linawlekea kumalizwa, au kama lina watu wengine, kati yao na mipaka ya Rwanda, kuna distance kubwa. Atakaeweza kurusha kombola na arushe tu. Sera ya Rwanda kwa sasa ni kwamba nchi ni ndogo. Hivyo, adui wake anafuatwa huko aliko, Rwanda haina uwanja wa vita. Na juzi raisi alisema hivi, kama mnauliza sababu ya Rwanda kuingia DRC, mbona hamuulizi sababu ya Rwanda kutkwenda DRC!! Wazungu midomo wazi. Fananisha hii vita na Russia na Ukraine. Maana leo hii ni kwamba imelenga kukomboa watu waCongo waongeao kinyarwanda.
3. M23, ni watu ambao wamejikuta wanaitwa wa Congo, baada ya wakoloni kugawa mipaka na kujikuta maeneo wanayokaa yanapewa Congo. Mpaka 1994, hakukuwa na tatizo lolote. Wakimbizi wa Rwanda walipoenda Congo, walihakikisha mtutsi aliekimbia nao au hao hao waliowakuta kwao Congo wanawamaliza. Vita vikaanza hivyo, wengine wakakimbilia Uganda na Rwanda. Uganda pia hao watu wapo. Ila sasa, usisahau. Mapolini, watutsi wafugaji, unadhani mifugo yao itaenda wapi!?
4. Mpaka mzungu anatia timu miaka 20 na kitu, unadhani alikosa nguvu ya kumaliza mzozo huo? Hapo kuna bonge la dili. Asilimia kubwa ya pato la wanasiasa na wazungu wengi, ni hapo hapo. Ulizia Iphone wanatumia madini ya wapi!
Kama mpaka hapo hujaelewa, wakuache tu ulivyo.