Mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini auliwa na M23

Rwanda ikemewe vikali na jumuiya ya kimataifa iache kuharibu amani ya Drc.
Shida pale ilipo DRC akishika maeneo nae anatumika na vibaraka wake ndo maana M23 anajikusanyia watu tu anafanya kama anawasaidia na wanawaelewa.....jamaa wasingekua na nguvu kuliko jeshi la serikali kama uraiani mambo yangekua sawa......yani hapo kila mtu anapeleka madini kwa watu wake......akimiliki M23 eneo ana soko lake anapeleka madini tena hukohuko kwa wazungu na wanapata silaha za kisasa kabisa, pia jeshi la serikali likichukua maeneo wanapeleka madini pia hukohuko kwa wazungu sema Drc alichofeli serikali yake ilikua ina base sana na Kinshasa na maeneo mengine ya kati huko huku mashariki akipatelekeza kwa vikundi mbalimbali....na wananchi wa kule wanajua serikali ikichukua maeneo yao ya madini ,,watachimba watauza ulaya na pesa itarudi kuneemesha Kinshasa na matajiri wake
 
Maj Gen anakufaje kizembe hivyo? Tatizo la Africa vyeo vingi jeshini haviendani na uwezo wa muhsika
ukisoma taarifa utagundua majeshi ya kigeni yapo huko kutalii na kuwacholesha majeshi ya serikali , Waafrika tuwatimue hawa na kuchukua migodi na maliasili zote ziwe chini ya Serikali
 
baada ya kuyajua yote haya bado huna solutiontv , hapo ndo bwana Zanzibar-ASP anawalumu viongoz wa waafrika pamoja na waafrikaya kwa ujumla
 
ukisoma taarifa utagundua majeshi ya kigeni yapo huko kutalii na kuwacholesha majeshi ya serikali , Waafrika tuwatimue hawa na kuchukua migodi na maliasili zote ziwe chini ya Serikali
Kuna msemo alitumia Kagame majuzi, kwamba anajua kuwatambua viongozi na wajinga. Akaongeza kwamba, mjinga akikabidhiwa uongozi, ni janga kubwa. Sasa viongozi wengi Africa wala hawapo kuongoza, ni vibaraka tu. Kuna nchi moja ukanda wa Sahel, eti ilimchagua raisi, nadhani ana miaka kama 90. Unajiuliza kama huyu atalisaidia nin taifa,huku hata kujitawaza inaonekana hawezi.
 
unawajua watusi kwanza ? huko Rwanda watusi wameua marais wawili wahutu , je nan anamchukia mwenzie ?
 
unawajua watusi kwanza ? huko Rwanda watusi wameua marais wawili wahutu , je nan anamchukia mwenzie ?
Haya, ebu dadavua mambo mzee! Naona unaijua historia vizuri. Lakini ukitoka hapo uende na Burundi.
 
hakika mkuu , bado hatuna reasoning. leaders
 
Hii kuna mkongo aliwahi niambia.

Ukisikia vita mahali ujue wanachimba madini.
 
Haya, ebu dadavua mambo mzee! Naona unaijua historia vizuri. Lakini ukitoka hapo uende na Burundi.
Kote shida ni watusi , kasome historia uone wameua viongoz wahutu mara kadhaa ila wahutu walikuwa kimya , watusi ni kama ccmu , the more unakaa kimya the more wanazid kukuonea , uzur wa watusi wanapenda maendeleo sio kama ccmu
 
hakika mkuu , bado hatuna reasoning. leaders
This time natamani ningezaliwa Burkina Faso basi niwe mkulima ijulikane. Huku ubanwe, kule ubanwe, eti uko kwenye nchi yako na unatakiwa uwe mzalendo, lakini kipaumbele anapewa mchina na mhindi wanaokutemea usoni, ukisema unawekwa ndani. Kwa hii issue ya DRC, inaenda kuibua mengi sana, bila kusahau mzungu kudhalilishwa na ngozi nyeusi hadhalani.
 
Hao wanaojifanya wakongo siku kagame na mu7 wakiondoka madarakani ndio utajua uraia wao
 
Kote shida ni watusi , kasome historia uone wameua viongoz wahutu mara kadhaa ila wahutu walikuwa kimya , watusi ni kama ccmu , the more unakaa kimya the more wanazid kukuonea , uzur wa watusi wanapenda maendeleo sio kama ccmu
Kwa hiyo hali ikiwa hivyo unadhani kinatokea kitu gani? Ushabiki huo mi siafikiani nao. Je, mtutsi au mhutu wa chini kabisa asiejua hili wala lile yeye anauliwa ili nini kitokee? Sasa ndo maana huyo mzungu akaona kama majinga yanaweza kuuwana yenyewe, nikomae na mambo yangu yenyewe yaendelee kuwa nyani tu. Je, uliwahi kufuatilia utusi na uhutu ulitoka wapi? Maana usije ukahisi ni makabila ya enzi kama yalivyo mengine ya kibantu!!!
 
Hii habari ni kama sijaielewa.Huyu Makonda alienda kuwatembelea wanajeshi wakiwa field au? na je ina maana aliwazukia jamaa akiwa hana ulinzi?
 
Hii habari ni kama sijaielewa.Huyu Makonda alienda kuwatembelea wanajeshi wakiwa field au? na je ina maana aliwazukia jamaa akiwa hana ulinzi?
Makonda wa drc tena........
 
Pakitokea mwamba mmoja dikteta akashkilia kila kitu vizuri Congo ni nchi moja ina rasilimali kinoma. Usimamiz na hii vita ya mda mrefu inawacost.
Naona Jamaa wanatanua mipaka, hawajaishia tuu Kivu
 
Pakitokea mwamba mmoja dikteta akashkilia kila kitu vizuri Congo ni nchi moja ina rasilimali kinoma. Usimamiz na hii vita ya mda mrefu inawacost.
Naona Jamaa wanatanua mipaka, hawajaishia tuu Kivu
Kwani,katika kuzingila Goma, si tayari wapo Kivu kusini? Na Burundi ikaamua wanajeshi wake watoke tu huko! Inaonekana na wao hawajui hatma ya hii vitu. Na kwa mjibu wa vyanzo vya habari,, kuna mwanajeshi mmoja wa Burundi na wanajeshi alionao wameshatiliwa mashaka, hivyo mpango ni kujiunga na M23! Unategemea nini taarifa hizi zikiwa za kweli?
 
Unaigawaje nchi ya watu?
DRC ni mali ya wakongo, vita iishe na ardhi ibakie kwa wakongomani.
Hiyo vita inaweza kuisha ndani ya mwezi mmoja tu ikiwa nchi za Africa kwa umoja wake zikiamua iishe. Tatizo wakuu wa nchi za Afrika wamejaa unafiki.
Upo SAHIHI
 
Huyo Mkuu alikuwa anapigana bega kwa bega na Interahamwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…