Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jiji limekushinda, Jitafakari! Ni pachafu sana

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jiji limekushinda, Jitafakari! Ni pachafu sana

Hao WATOTO wa vigogo wanapeana ajira tu ili wasikae Jobless.

Ingekuwa ni kufanya kazi, wangeweka mtu anayefanya KAZI na siyo kulipa fadhila au kuwapa rushwa watu watulie.
Ukiwa kwenye familia ya viongozi wa CCM lazima utafanikiwa ingawa ni kifisadi zaidi
 
Getrude mongela alupigania uhuru wa nchi hii lazima tumuenzi...
Kumuenzi mtu ni kumpa vyeo vya kufanya maamuzi !???

Ndio maana wananchi wanaumia.

Hili waliliona waingereza wakaamua kuifanya familia ya Malikia "Ceremonial"
 
Linapokuja suala la usafi wa hilo jiji la Mwanza, RC anaweza kubeba lawama kutokana na nafasi yake, lakini watendaji wengine kama mkuu wa wilaya, wakurugenzi nk ni wahusika pia. Na sasa hivi hakuna wapinzani wa kuleta changamoto kwa watendaji, basi tegemeeni uchafu maradufu.
 
Kwani comparison ya Mongela na Magesa kwenye mizani ya jiji la Mwanza imekaaje?
 
Mkuu wa mkoa utamsingizia ngebe . Mipango ya usafi ni ya halmashauri ya jiji la mwanza na manispaa ya Ilemela. Tamko la kuruhusu wamachinga kila sehemu lilitolewa na boss akiwa mwanza. Mongela afanyeJe sasa ?!. Ukitaka jiji la mwanza liwe Safi mpaka wamachinga wapangwe au waonfolewe ktkt ya jiji.
 
Mkuu wa mkoa utamsingizia ngebe . Mipango ya usafi ni ya halmashauri ya jiji la mwanza na manispaa ya Ilemela. Tamko la kuruhusu wamachinga kila sehemu lilitolewa na boss akiwa mwanza. Mongela afanyeJe sasa ?!. Ukitaka jiji la mwanza liwe Safi mpaka wamachinga wapangwe au waonfolewe ktkt ya jiji.
Mkuu wa Mkoa anaangalia eneo pana zaidi ya Jiji la Mwanza, Ukerewe, Sengerema, Magu, Kwimba, Misungwi na Buchosa kumlaumu kwa usimamizi wa usafi wa Jiji ni kumuonea tu, Wanaokusanya mapato ni Mkurugenzi na wanatoa tenda za ukusanyaji taka/ usafi kwa ujumla ni Mkurugenzi/ Meya na Baraza la Madiwani. Mku wa Mkoa kumuingiza humo naweza sema ni chuki tu....
 
Yes, Mwanza Jiji kuna shida siyo siri...

Lakini mimi siwezi kusema moja kwa moja kama tatizo liko kwa RC au la...

Lakini ukweli ni kuwa, ukiingia Mwanza jijini katikati, mambo ni hovyo na shaghala bagala kabisa...

Ukiachilia uchafu wa taka taka zilizozagaa ovyo, pia kuna ishu ya wachuuzi na wafanya biashara ndogondogo za kupanga barabarani...

Ukiingia ktk barabara za Mwanza kwa sasa, haieleweki magari yatembelee wapi, waenda kwa miguu watembelee wapi na baiskeli na pikipiki zitembelee wapi...

Ni kwamba, hawa wafanya biashara barabara zote zimekuwa ni maeneo ya biashara mpaka inakera kwa kweli...

Imefika mahali hata polisi wa usalama barabarani wanashindwa kufanya kazi yao ya usalama Wa vyombo vya moto, raia na mali zao kwa sababu ya muingiliano huu...

Kuna kila dalili na sababu kuwa, hili Luna kibali cha wanasiasa...

Sasa hii ni mbaya na hatari sana kama tunaweza kuingiza siasa ktk mambo hata yahusuyo usalama na maendeleo ya wananchi...

Kufanya mambo yetu ovyo hovyo bila utaratibu kamwe siyo ustaarabu hata kidogo bali ni ujinga na kichocheo cha umasikini zaidi...

Kama tunataka kupiga hatua za maendeleo yetu haraka, tutoke na tuachane na siasa za namna hii. Siasa za kutazama maslahi ya kundi dogo tu na kuacha mamilioni ya wananchi wakitaabika...

Mwanza ipo shida na udhaifu Mkubwa wa usimamizi wa sheria za mipango ya miji. Huu si ujanja. Ni ujinga na dalili za watu wasiostaarabika...
 
Mkuu wa Mkoa anaangalia eneo pana zaidi ya Jiji la Mwanza, Ukerewe, Sengerema, Magu, Kwimba, Misungwi na Buchosa kumlaumu kwa usimamizi wa usafi wa Jiji ni kumuonea tu, Wanaokusanya mapato ni Mkurugenzi na wanatoa tenda za ukusanyaji taka/ usafi kwa ujumla ni Mkurugenzi/ Meya na Baraz ala Madiwani. Mku wa Mkoa kumuingiza humo naweza sema ni chuki tu....
Yes, Mwanza Jiji kuna shida siyo siri...
Natamani mleta post ajifunze kitu kutoka kwenu.

Wamachinga ni chanzo cha hali ya mwanza ilivyo.
 
Hiyo picha ya kwanza ni mtaani kwangu hapo nkurumah road mtaa wa Uturn alafu mita chache kutoka hapo ndipo ilipo bohari ya madawa ya MSD, yani pachafu sana mwanza!
 
Yani Mkuu wa Mkoa akashughulike na uchafu wa mitaani, viongozi wa halmashauri wanafanya nini?
Unaandika kama mtu asiyejua mgawanyo wa kazi! Hayo mambo ya usafi ni jukumu la halmashauri, Jiji na manispaa, siyo RC. Ina maana hata Magu, Ngudu, Misungwi nako takataka zisipozolewa basi inabidi mkuu wa mkoa aende kusimamia uzoaji? Poor you!
 
Back
Top Bottom