Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

Tulishayasema, nayakasemwa, na yanaendelea kusemwa.....DITO na JK ni MAPACHA..hata Fomu za urais JK alichukulia pale Kibaha kwa DITO...DITO akaengineer kampeni hadi JK kashinda kwa kishindo...ATI AWE ANA HATIA..nani kasema TZ kuna haki?

Well, DITO alishajiandaa kupekea kujiti kwa Malecela cha makamu mwenyekiti, wa CCM...JK ndo Chairman, okay yamemkuta hayo yalomkuta...LAKINI HANA HATIA TZ!

Ditopile aaga Keko kwa vurugu kortini

na Happiness Katabazi

MWANZO wa ngoma ni lele. Vurugu, kejeli na mbwembwe zisizo na msingi zilizoanza kufanywa na ndugu na jamaa wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri na kupigiwa chapuo na vituko vyake mwenyewe, jana vilitawala eneo la Mahakama Kuu, wakati shauri la mauaji ya bila kukusudia lilipofikishwa hapo kwa ajili ya kusikilizwa kwa ombi la dhamana.

Ndugu na jamaa hao wa Ditopile ambaye amekuwa katika mahabusu ya Keko tangu Novemba mwaka jana, wakisaidiwa na polisi waliokuwa katika sare na mavazi ya kiraia, walianzisha vurumai kubwa kuwazuia wanahabari kumkaribia au kumpiga picha mwanasiasa huyo ambaye alipewa dhamana.

Vurugu hizo ambazo zilisababisha waandishi kadhaa kujeruhiwa na wengine kuharibikiwa vitendea kazi vyao, zikiwamo kamera, ziliambatana na kurushiana makonde na maneno kati ya wanahabari hao kwa upande mmoja na jamaa na ndugu wa Ditopile, waliokuwa wakisaidiwa na polisi.

Matukio hayo yaliyokwenda sambamba na kuwamwagia maji wanahabari na kutoa maneno ya kuidhalilisha serikali na hata viongozi wake wakuu, yalifanywa na baadhi ya ndugu na jamaa hao wa Ditopile waliothibitisha pasipo shaka kuwa walikuwa ni watu wasio na staha, walioshindwa kujiheshimu, wapungufu wa hekima, waliokosa subira na walioamua kwa makusudi kuidharau mahakama na taaluma ya habari.

Vurugu hizo zilianzia ndani ya jengo la mahakama majira ya saa 8:59 na kumalizikia nje ya geti la mahakama hiyo saa 9:50 alasiri, wakati Ditopile aliyekuwa katika ulinzi mkali huku akiwa amevaa kofia yake ya ‘pama’ akitoka nje ya jengo la Mahakama Kuu.

Wanahabari wa Tanzania Daima waliokuwapo eneo la Mahakama Kuu katika Barabara ya Kivukoni walikuwa miongoni mwa watu waliokumbwa na zahama hiyo ambayo ilisababisha Joseph Zablon, ambaye ni mpiga picha kujeruhiwa sehemu za mdomoni.

Kikubwa kilichoonekana kuwakera polisi, ndugu na jamaa za Ditopile ni wajibu wa kikazi wa wanahabari hao kufanya juhudi za kumfikia mwanasiasa huyo aliyekuwa amezingirwa kwa lengo la kumficha, huku yeye mwenyewe akiwa amejiinamia.

“Tokeni zenu, sisi ndio wenye nchi…siku zote nazi haishindani na jiwe ni lazima itapasuka. …ni mtu wa karibu sana na Dito ambaye ni ndugu yetu, mnafikiri atakubali rafiki yake asote muda wote, haiwezekani na ndiyo kaishapata dhamana, yupo huru na nyie ‘wambea’ endeleeni kuandika weeee! Hadi kalamu zenu ziishe wino…ndiyo hivyo, kaisharejea uraiani.

“Au hamna habari kwamba Ditopile alikuwa Best Man wa …na hadi sasa ni marafiki, na nyie waandishi wa habari kwa akili zenu zilivyo ndogo mnafikiri anapenda anavyokaa jela…duniani hakuna haki, haki ipo mbinguni, utawala huu ni kujuana na wakubwa, mambo yatakunyookea,” ni maneno yaliyokuwa yakitoka kinywani mwa mmoja wa watu waliokuwa wamejumuika katika kundi la ndugu na jamaa wa Ditopile.

Alipotoka katika eneo hilo, Ditopile aliingizwa katika gari dogo aina ya Toyota Ballon, lenye namba za usajili T723ADF, la rangi ya fedha, lililokuwa likisindikizwa na Land Rover (Defender) ya Polisi yenye namba za usajili, T212AMV.

Muda mfupi baadaye, polisi waliokuwa katika eneo hilo, waliwaeleza waandishi wa habari kuwa, msafara huo kwanza ulielekea Keko kuchukua vitu mbalimbali vya mwanasiasa huyo, kabla ya kwenda nyumbani kwake.

Baada ya msafara huo kuondoka saa 9:30, ndugu wa Ditopile na askari kanzu waliobaki mahakamani hapo waliendelea kutupiana makonde na waandishi wa habari huku ndugu hao wakiendelea kutoa lugha ya matusi na kumwaga maji kwenye kamera za wapiga picha ili ziharibike.

Sekunde chache, hali ilibadilika baada ya mamia ya raia ambao waliungana na waandishi wa habari kuwafokea askari ambao awali walikuwa wakisaidia kumficha Ditopile asipigwe picha na kuwazuia waandishi wasimfikie.

“Polisi gani nyie, mnafanya kazi kwa kujipendekeza badala ya kulinda usalama wa raia na kutuliza ghasia lakini nyie ndio mmekuwa chanzo cha vurugu…na kwa taarifa yenu, kwa picha hii mliyoionyesha hapa tumeamini kabisa hapa hakuna kesi,” alisikika akisema mwananchi mmoja aliyekuwa mahakamani hapo na akajitambulisha kwa jina la Dk. Hassan Zubeir.

Miongoni mwa wanahabari waliopata athari kutokana na vurugu hizo ni mpiga picha wa magazeti ya Majira, Business Times na Spoti Starehe, Patrick Spear, ambaye mbali ya kamera yake kuharibiwa alichaniwa vifungo vya shati lake.

“Vurugu hizi zinazofanywa na ndugu wa mtuhumiwa kila kukicha, tena mahakamani, zinaipaka matope serikali na Jeshi la Polisi, na serikali ikae ikijua tayari wananchi wengi wana wasiwasi wa haki kutendeka…haiwezekani hawa ndugu kila kukicha wanafanya vurugu mahakamani na hawachukuliwi hatua,” alisema Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la TheCitizen, Mpoki Bukuku.

Awali kabla ya vurugu hizo, Ditopile alipandishwa kizimbani saa 5:20 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku mahakama ikiwa imefurika mamia ya wananchi waliokuwa na shauku ya kujua kulikoni.

Mmoja wa mawakili wa Ditopile, Profesa Jwani Mwaikusa, aliiomba mahakama impatie dhamana mteja wake kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika na kwamba mteja wake ni mtu anayejiheshimu na kuaminika mbele ya jamii, hivyo hawezi kuruka dhamana.

Upande wa Mwanasheria wa Serikali, ulidai mahakamani hapo kuwa haukuwa na pingamizi kuhusu ombi hilo, kwa kuwa dhamana ni haki ya kila mtu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kuzichambua, Jaji Augustine Mwarija, alitoa dhamana kwa masharti ya bondi ya sh milioni 60. Mshitakiwa alitakiwa kutoa bondi ya sh milioni 20 na wadhamini wawili ambao kila mmoja wao alitakiwa kutoa bondi ya sh milioni 20 kila mmoja.

Mtuhumiwa alitakiwa kukabidhi hati yake ya kusafiria polisi na akatakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya polisi, na akatakiwa pia awe akiripoti kwa Kamanda wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Ditopile aliletwa mahakamani hapo saa 2:54 asubuhi na msafara wa polisi na akapitishwa kwenye mlango unaotumiwa na majaji.

Muda mfupi baada ya majaji na viongozi wa mahakama hiyo kubaini mchezo huo, waliwafokea polisi hadharani na kusema kitendo hicho kimefanywa kinyume cha taratibu za mahakama.

Naye Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Philophr Lyimo, alikiri kutokea kwa tukio hilo na akasema mahakama hiyo imekerwa na tabia ya polisi hao na kuongeza kuwa, tayari ameshawasiliana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, ili aweze kuwachukulia hatua askari wake.

“Ule mlango unatumiwa na majaji, hata sisi tumeshindwa kuelewa ni kwa nini wamempitisha katika mlango ule na huku Ditopile ni mtuhumiwa kama mtuhumiwa mwingine….siyo siri tumekerwa na tumeshawaambia kabla ya saa sita leo mchana (jana) wajieleze.

“Hii ni mahakama na watu wanakuja kutafuta haki hapa. Sasa polisi wanapofanya mambo kama haya ambayo nasema yana lengo la kuichafua mahakama yetu, hatuwezi kuyavumilia. Ni lazima wachukuliwe hatua,” alisema Lyimo.
 
Nguvu ya mtandao yadhiirika, hawa wanamtandao ni hatari kwelikweli, nadhani kwa nguvu waliyonayo hata muungwana hawezi kuwadhibiti, kama wameweza kufanya watakavyo mahakama kuu ya tanzania .......

Yetu macho....
 
Tulishayasema, nayakasemwa, na yanaendelea kusemwa.....DITO na JK ni MAPACHA..hata Fomu za urais JK alichukulia pale Kibaha kwa DITO...DITO akaengineer kampeni hadi JK kashinda kwa kishindo...ATI AWE ANA HATIA..nani kasema TZ kuna haki?

Duh.....It's amazing and Unbelievable but it's true**
 
Nguvu ya mtandao yadhiirika, hawa wanamtandao ni hatari kwelikweli, nadhani kwa nguvu waliyonayo hata muungwana hawezi kuwadhibiti, kama wameweza kufanya watakavyo mahakama kuu ya tanzania .......

Yetu macho....
Unapowataja wanamtandao Hivi muungwana unamueka kundi gani?
 
Tanzania itafika pale inapotaka KUFIKA hili swala wala lisiwapeni shida. 'KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA.'
 
Tulikwisha kusema ukiwa na watawala wenye uhahakika na nafasi yao watafanya chochote bila woga. Tumefanya makosa sisi watanzania kuwaamini CCM kupita kiasi; sasa wanaweza kufanya lolote bila aibu maana wana uhakika na kura zenu mwaka 2010. Hadi pale watanzania watakapojua kuwa watanzania wana uwezo wa kubadili serikali, wataendelea kutuchezea. Nasi tutaendelea kuliakulia kama vile hawa viongozi wanajichaguaga wenyewe!
 
85956.jpg

Alleged relatives of Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (inset) confront members of the press within the High Court grounds in Dar es Salaam yesterday. (Photo: Selemani Mpochi).
 
Ditopile aaga Keko kwa vurugu kortini

na Happiness Katabazi

MWANZO wa ngoma ni lele. Vurugu, kejeli na mbwembwe zisizo na msingi zilizoanza kufanywa na ndugu na jamaa wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri na kupigiwa chapuo na vituko vyake mwenyewe, jana vilitawala eneo la Mahakama Kuu, wakati shauri la mauaji ya bila kukusudia lilipofikishwa hapo kwa ajili ya kusikilizwa kwa ombi la dhamana.

Ndugu na jamaa hao wa Ditopile ambaye amekuwa katika mahabusu ya Keko tangu Novemba mwaka jana, wakisaidiwa na polisi waliokuwa katika sare na mavazi ya kiraia, walianzisha vurumai kubwa kuwazuia wanahabari kumkaribia au kumpiga picha mwanasiasa huyo ambaye alipewa dhamana.

Vurugu hizo ambazo zilisababisha waandishi kadhaa kujeruhiwa na wengine kuharibikiwa vitendea kazi vyao, zikiwamo kamera, ziliambatana na kurushiana makonde na maneno kati ya wanahabari hao kwa upande mmoja na jamaa na ndugu wa Ditopile, waliokuwa wakisaidiwa na polisi.

Matukio hayo yaliyokwenda sambamba na kuwamwagia maji wanahabari na kutoa maneno ya kuidhalilisha serikali na hata viongozi wake wakuu, yalifanywa na baadhi ya ndugu na jamaa hao wa Ditopile waliothibitisha pasipo shaka kuwa walikuwa ni watu wasio na staha, walioshindwa kujiheshimu, wapungufu wa hekima, waliokosa subira na walioamua kwa makusudi kuidharau mahakama na taaluma ya habari.

Vurugu hizo zilianzia ndani ya jengo la mahakama majira ya saa 8:59 na kumalizikia nje ya geti la mahakama hiyo saa 9:50 alasiri, wakati Ditopile aliyekuwa katika ulinzi mkali huku akiwa amevaa kofia yake ya ‘pama’ akitoka nje ya jengo la Mahakama Kuu.

Wanahabari wa Tanzania Daima waliokuwapo eneo la Mahakama Kuu katika Barabara ya Kivukoni walikuwa miongoni mwa watu waliokumbwa na zahama hiyo ambayo ilisababisha Joseph Zablon, ambaye ni mpiga picha kujeruhiwa sehemu za mdomoni.

Kikubwa kilichoonekana kuwakera polisi, ndugu na jamaa za Ditopile ni wajibu wa kikazi wa wanahabari hao kufanya juhudi za kumfikia mwanasiasa huyo aliyekuwa amezingirwa kwa lengo la kumficha, huku yeye mwenyewe akiwa amejiinamia.

“Tokeni zenu, sisi ndio wenye nchi…siku zote nazi haishindani na jiwe ni lazima itapasuka. …ni mtu wa karibu sana na Dito ambaye ni ndugu yetu, mnafikiri atakubali rafiki yake asote muda wote, haiwezekani na ndiyo kaishapata dhamana, yupo huru na nyie ‘wambea’ endeleeni kuandika weeee! Hadi kalamu zenu ziishe wino…ndiyo hivyo, kaisharejea uraiani.

“Au hamna habari kwamba Ditopile alikuwa Best Man wa …na hadi sasa ni marafiki, na nyie waandishi wa habari kwa akili zenu zilivyo ndogo mnafikiri anapenda anavyokaa jela…duniani hakuna haki, haki ipo mbinguni, utawala huu ni kujuana na wakubwa, mambo yatakunyookea,” ni maneno yaliyokuwa yakitoka kinywani mwa mmoja wa watu waliokuwa wamejumuika katika kundi la ndugu na jamaa wa Ditopile.

Alipotoka katika eneo hilo, Ditopile aliingizwa katika gari dogo aina ya Toyota Ballon, lenye namba za usajili T723ADF, la rangi ya fedha, lililokuwa likisindikizwa na Land Rover (Defender) ya Polisi yenye namba za usajili, T212AMV.

Muda mfupi baadaye, polisi waliokuwa katika eneo hilo, waliwaeleza waandishi wa habari kuwa, msafara huo kwanza ulielekea Keko kuchukua vitu mbalimbali vya mwanasiasa huyo, kabla ya kwenda nyumbani kwake.

Baada ya msafara huo kuondoka saa 9:30, ndugu wa Ditopile na askari kanzu waliobaki mahakamani hapo waliendelea kutupiana makonde na waandishi wa habari huku ndugu hao wakiendelea kutoa lugha ya matusi na kumwaga maji kwenye kamera za wapiga picha ili ziharibike.

Sekunde chache, hali ilibadilika baada ya mamia ya raia ambao waliungana na waandishi wa habari kuwafokea askari ambao awali walikuwa wakisaidia kumficha Ditopile asipigwe picha na kuwazuia waandishi wasimfikie.

“Polisi gani nyie, mnafanya kazi kwa kujipendekeza badala ya kulinda usalama wa raia na kutuliza ghasia lakini nyie ndio mmekuwa chanzo cha vurugu…na kwa taarifa yenu, kwa picha hii mliyoionyesha hapa tumeamini kabisa hapa hakuna kesi,” alisikika akisema mwananchi mmoja aliyekuwa mahakamani hapo na akajitambulisha kwa jina la Dk. Hassan Zubeir.

Miongoni mwa wanahabari waliopata athari kutokana na vurugu hizo ni mpiga picha wa magazeti ya Majira, Business Times na Spoti Starehe, Patrick Spear, ambaye mbali ya kamera yake kuharibiwa alichaniwa vifungo vya shati lake.

“Vurugu hizi zinazofanywa na ndugu wa mtuhumiwa kila kukicha, tena mahakamani, zinaipaka matope serikali na Jeshi la Polisi, na serikali ikae ikijua tayari wananchi wengi wana wasiwasi wa haki kutendeka…haiwezekani hawa ndugu kila kukicha wanafanya vurugu mahakamani na hawachukuliwi hatua,” alisema Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la TheCitizen, Mpoki Bukuku.

Awali kabla ya vurugu hizo, Ditopile alipandishwa kizimbani saa 5:20 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku mahakama ikiwa imefurika mamia ya wananchi waliokuwa na shauku ya kujua kulikoni.

Mmoja wa mawakili wa Ditopile, Profesa Jwani Mwaikusa, aliiomba mahakama impatie dhamana mteja wake kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika na kwamba mteja wake ni mtu anayejiheshimu na kuaminika mbele ya jamii, hivyo hawezi kuruka dhamana.

Upande wa Mwanasheria wa Serikali, ulidai mahakamani hapo kuwa haukuwa na pingamizi kuhusu ombi hilo, kwa kuwa dhamana ni haki ya kila mtu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kuzichambua, Jaji Augustine Mwarija, alitoa dhamana kwa masharti ya bondi ya sh milioni 60. Mshitakiwa alitakiwa kutoa bondi ya sh milioni 20 na wadhamini wawili ambao kila mmoja wao alitakiwa kutoa bondi ya sh milioni 20 kila mmoja.

Mtuhumiwa alitakiwa kukabidhi hati yake ya kusafiria polisi na akatakiwa kutotoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya polisi, na akatakiwa pia awe akiripoti kwa Kamanda wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Ditopile aliletwa mahakamani hapo saa 2:54 asubuhi na msafara wa polisi na akapitishwa kwenye mlango unaotumiwa na majaji.

Muda mfupi baada ya majaji na viongozi wa mahakama hiyo kubaini mchezo huo, waliwafokea polisi hadharani na kusema kitendo hicho kimefanywa kinyume cha taratibu za mahakama.

Naye Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Philophr Lyimo, alikiri kutokea kwa tukio hilo na akasema mahakama hiyo imekerwa na tabia ya polisi hao na kuongeza kuwa, tayari ameshawasiliana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana, ili aweze kuwachukulia hatua askari wake.

“Ule mlango unatumiwa na majaji, hata sisi tumeshindwa kuelewa ni kwa nini wamempitisha katika mlango ule na huku Ditopile ni mtuhumiwa kama mtuhumiwa mwingine….siyo siri tumekerwa na tumeshawaambia kabla ya saa sita leo mchana (jana) wajieleze.

“Hii ni mahakama na watu wanakuja kutafuta haki hapa. Sasa polisi wanapofanya mambo kama haya ambayo nasema yana lengo la kuichafua mahakama yetu, hatuwezi kuyavumilia. Ni lazima wachukuliwe hatua,” alisema Lyimo.

Ditto amepewa dhamana.Hilo sio tatizo,kwa vile inaelekea kuna mwanya flani wa kisheria ambao unamwezesha mtuhumiwa wa mauaji (yawe ya kukusudia au la) apewe dhamana.Kilichoniacha mdomo wazi ni jinsi kesi hiyo ilivyokuwa fast-tracked.Hivi kuna watuhumiwa wangapi wanaojaza rumande zetu miezi nenda miezi rudi huku kesi zao zikiendelea kupigwa kalenda kwa kisingizio cha "upepelezi haujakamilika"?

Nilifahamu tangu mwanzo kuwa Ditto angepewa dhamana.Ukishaona mtuhumiwa analetwa mahakamani kwa balooni ilhali watuhumiwa wengine wanaletwa kwenye karandinga basi ujue hapo ipo namna.Pia jinsi Jamhuri ilivyoweza kutumia namna kubadilisha mashtaka kutoka "kuua kwa kukusudia" hadi kuwa "kuua bila kukusudia" wengi walishabaini kuwa hapo kuna namna ya kumtoa Ditto with least noises from wadanganyika.

Unaposikia DPP anataka "watu wasichonge" pale Ditto alipobadilihiwa mashtaka,huku kauli za mamlaka hiyo inayotakiwa kuithibitishia mahakama kuhusu makosa ya mtuhumiwa,zikiwa ni kama za kumtetea mtuhumiwa huyo basi ni dhahiri kuwa kesi ilikuwa inamalizwa kiaina na kilichoendelea mahakamani ni upotezaji tu wa fedha za wavuja jasho.Nasema hivyo kwa vile wajuzi wa mambo walishasema kuwa Ditto hawezi kufungwa hata kama atakutwa na hatia.Na leo ndugu zake wametamka bayana kuwa wao ndio wenye nchi,na Ditto kama best-man wa JK hawezi kutelekezwa.

Inasikitisha kuona nchi ikiwa na aina mbili ya sheria:kwa vigogo na kwa walalahoi.Majuzi mbunge kagundulika kuwa amefoji vyeti lakini jeshi la polisi linatuambia kuwa hajafanya kosa.Hivi jamani kugushi sio kosa la jinai siku hizi?

Hivi nchi yetu inapelekwa wapi?
 
Ngudu zanguni kwani htujuwi kwamba Tanzania kuna “Wahutumiwa” na “Vijihutumiwa”? Ditto ni “Mhutumiwa” na hakuhitaji karandinga wale kupita katika mlango wa kawaida huko Mahakamani.
Ditto alipomuuwa yule dereva tuliona Vigogo wengi kwenda kumhani yule kizuka. Sasa ni Vigogo wangapi watakwenda kwa Ditto kumpongeza kwa kupewa hiyo dhamana?
Vigogo wa CCM wako juu ya sheria ya nchi. Hii ndio maana ikatafutwa kile kipengele cha kubadilisha mashtaka yake kutoka” kuua kwa makusudi” kwenda “kuua bila ya kudhamiria”. Muuwaji ni muuwaji tu.
Ameuwa hadharani na ni kitendo kibaya mno.

UKIUWA MU MMOJA NI KAMAUMEUWA UMMAMZIMA. ADHABU YAKE APAIPATA HUKO AKHERA HATA KAMA ATASAMEHEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA. ATAKUTA HUKUMU YAKE INAMGOJEA.

Ni wangapi kati ya hao “Vijituhumiwa” ambao wataletwa mahakamni kwa mlango wa nyuma na kesha wapewe dhamana? Twakuuliza we rais yetu J.K.

Wataalamu wa mikataba hatuna nchini lakini “wataalamu” wa kubadilishe vipengele vya sheria tunao! Ni watanzania wangapi watauliwa kwa kutumia kipengele hiki” kuua bila ya kudhamiria”?

Kisheria nchi yetu imekwisha haribika.Majambazi pia yanaua “bila ya kudhamiria” kwani wanafyatua na kusambaza risasi ovyo ovyo bila ya kulenga mtu maalum!
 
Chama Chetu cha Mapinduzi kiko kwa ajili ya walala hoi nakutetea haki zetu wanyonge ama ?
 
LUYUNGU
umesha sema chama cha MAPINDUZI lazima ujue hayo mapinduzi ya aina gani na ndio maana wanakuambia
 
Nimezungumza na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar-es-Saalam Bw. Tibaigana kuhusu kitendo cha polisi kumpitisha kwa nguvu mshitakiwa Ditopile kwenye mlango wa majaji jambo ambalo halijawahi kutokea! Mahojiano yangu naye yatakuwa hewani this weekend usikose!!

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
luyungu
Unafahamu lakini maana ya mapinduzi? ndio maana tunasem mapinduzi DAIMA
 
Nimezungumza na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar-es-Saalam Bw. Tibaigana kuhusu kitendo cha polisi kumpitisha kwa nguvu mshitakiwa Ditopile kwenye mlango wa majaji jambo ambalo halijawahi kutokea! Mahojiano yangu naye yatakuwa hewani this weekend usikose!!

http://mwanakijiji.podomatic.com

Tunasubiri tumsikie amesema nini Lakini naona anatafutwa kondoo wa sadaka mwisho ya yote!
 
Admin!
na hii nayo ni muendelezo wa Ditopile au?tafadhali ifanyie maarifa ili tuendelee na mtiririko mzuri.Ombi.......................Please!
 
anawalaumu waandishi wa habari!
Ulitakaje?Huyu ndiye yule yule baada Mheshimiwa kuua alienda nyumbani kwake huyu ndiye aliyeandaa mazingira ya mwanzo ya kwenye maelezo kwa kuwatumia watu wake ili yaonyeshe muelekeo wa kuua bila kukusudia,huyu ndiye aliyeenda mahakama ambayo haina uwezo kisheria kuendesha kesi za namna hiyo yaani KISUTU kutoa maelezo ya awali.....................ili kesi ipelekwe Mahakama kuu kwa mwendo mdundo....................Sitaki kumuhukumu nasubiri hayo maelezo yake na waliomuhukumu wameshafanya hivyo na nusu ya historia imeshajiandika!
 
Let me guess!

Mwanakijiji:- Mheshimiwa ndugu Tibaigana, ilikuwaje hasa hadi kufikia mshitakiwa kupitishwa mlango wa jaji jambo ambalo ni kinyume cha taratibu na sheria za mahakama?

Tibaigana:- Aiseee Unajua tulipofika pale kortini kusema kweli umati ulikuwa mkubwa sana. hatukutegemea kabisa kwa hiyo, ili kumlinda mshtakiwa tuliona haja kubwa ya kufanya hivyo. Uamuzi wa haraka sana Ulitakiwa!

Mwanakijiji:- Je, katika kufanya hivyo mlifanya mawasiliano na ofisi ya mahakama kupata ruksa ya kutumia mlango huo?

Tibaigana:- Kijana ebu kwanza ondoa hilo swali, maana sasa wewe unataka kujaribu watu akili hapa. Nimesema ilikuwa ni uamuzi wa haraka, Unazijua wewe taratibu za mahakama? waulize hao waandishi wa habari kwa nini walivamia gari la mshtakiwa wakati akiletwa mahakamani?

Mwanakijiji:- Samahani mzee wangu lakini pamoja na hivyo kwani hii ilikuwa mara ya kwanza mshitakiwa kupelekwa mahakani?

Tibaigana:- Kijana itabidi tuanze upya haya mahojiano. Futa yote yalitotangulia na tafadhali sana kijana usije kuropoka ovyo. Hili ni swala zito sana kuliko umri wako. Unasikia?

Mwanakijiji:- ndio mzee nimekusikia na nimekwisha futa tuanze upya maswali.

Tibaigana:- Heee! heee! kijana ebu nipe kwanza hayo maswali kabla hujaanza kurekodi!
 
Mkandara, very close...but no.. kutishwa sitishwi!! Na, I'll never rerecord mtu ambaye amesema bila kufikiri!!
 
Back
Top Bottom