Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Aliyewahi kuwa mkuu wa ujasusi Rwanda na Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Gen Kayumba anasema matatizo yote yanayotokea mashariki ya Congo yanasababishwa na kagame.

Anasema Congo hamna tena tatizo la Banyamulenge ,lilishakwisha zamani na wana haki sawa na wanahudumu hata sasa katika serikali ya Congo.
Anasema kagame amekuwa Congo zaidi ya miaka 30 akiwaua wahutu wa Fdrl baada ya Genocide mpaka leo, na kwamba hana kisingizio tena kuhusu Fdrl nchini Congo.

Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.

Anakiri ndani ya Rwanda wahutu wamefungwa minyororo na kufuri hawana pakuongelea na hawana mtetezi.

Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.

Kumbuka huyu Mtusi kama ilivyo kwa kagame.

Hapa chini nimeweka interview yake yote ya leo wakati akihojiwa akiwa uhamishoni nchini Afrika Kusini.


View: https://x.com/Sentletse/status/1885998079419003033?t=XrJ7G6I2xDOUSU6Sr__OXg&s=19

Glad watching and listening to General Nyamwasa , thank you Gen. 🙏🙏🙏
 
Balozi wa india? Sema aliyewahi kuwa balozi wa rwanda nchini india na mkuu wa ujasusi rwanda
 
Kwamantiki hyo naona M23 wametumwa na PK kwa lengo la kuiba madini kama inavozoeleka... lakini pia anawafata Wahutu waliopo Congo kwenda kuwadhibiti..lakini pia anaoneka anampango wa siri wakuja kumega sehemu ya Congo..lakini pia anaonekana ni kibaraka wa wazungu..lakini pia anafanya hvo ilikuona nani anasiraha kali zaidi yake upande wa Afrika mashariki na kati..lakini pia kubwa zaidi kisasi na Wahutu bado kipo..lakini pia anaonekana anatamaa kubwa kupita kiasi...Mwisho kabisa anaonekana ni Kirusi cha Afrika mashariki na kati ambacho kinapaswa kuuliwa au kutolewa kisije kuleta machafuko makubwa ya nchi hizi...Nimemchambua nimemaliza tukiendelea kumlea tusijutie baadaye.
Umemaliza, yote. Inasemekana Rwanda inaelekea Bukavu.
 
Ye anasema anachofnya Kagame ni msukumo wa walio nyuma yake ambae ni wakubwa na mimi namuuliza kwanini akubali kutumika?
Mkuu hata asipotumika yeye somebody else will do it na sio hiyari, matatizo ya wakongo yatatatuliwa na wakongo. Mfano sasa hivi Tishekedi kualika watu kupigania nchini kwake kwa madai ya kuiondoa M23, haioni hatari ya kuondolewa yeye kabla ya hao waasi kama halioni hilo hafai kuiongoza 🇨🇩. Wale wanaotaka EAC yeye mwenyewe kawakataa anawataka hao waliokuwepo huko. Na kwa vile tatizo halisi haliongelewi watu wanafata upepo na mkumbo basi vita hii itadumu historia haidanganyi.
 
Huyo jamaa alitakiwa aende uhamishoni Ulaya au Marekani, hapo alipo sio salama kabisa kwani ameshakoswakoswa mara kadhaa.

Alichokisema ni kweli kabisa Kagame ndio mzizi wa fitina kwenye eneo lote la maziwa makuu na bila kumuondoa amani haitakuwepo kwenye eneo lote hili.
 
Snowden
Mkuu ukiwa ugenini huna ulinzi huna bacl up huna inforner wako uko alone unajificha sana...kosa kujulikama unapoishi.....miaka inaenda huwajui new recruits huwa wanauawa kirahisi sana hata na wahudumu wananunuliwa.....sukia tu ukiwa uhamishonii.....lolote laweza kutokea....PK ana pesa chafu kupoteza....hata miaka 10 anakutumia watu tuu wengine wanasoma wengine biashara....wengine wanawanunua watu wako karobuuu watajua tu....traces kupewa pesa zako watajua address yako....au kwenda bank kutoa pesa kula matumiziiii......sikia tuu mkuuu....watu 10 wapewe kaxi track wewe miaka 5 mingi watajua kitu tuuu
 
Back
Top Bottom