Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Aliyewahi kuwa mkuu wa ujasusi Rwanda na Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Gen Kayumba anasema matatizo yote yanayotokea mashariki ya Congo yanasababishwa na kagame.

Anasema Congo hamna tena tatizo la Banyamulenge ,lilishakwisha zamani na wana haki sawa na wanahudumu hata sasa katika serikali ya Congo.
Anasema kagame amekuwa Congo zaidi ya miaka 30 akiwaua wahutu wa Fdrl baada ya Genocide mpaka leo, na kwamba hana kisingizio tena kuhusu Fdrl nchini Congo.

Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.

Anakiri ndani ya Rwanda wahutu wamefungwa minyororo na kufuri hawana pakuongelea na hawana mtetezi.

Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.

Kumbuka huyu Mtusi kama ilivyo kwa kagame.

Hapa chini nimeweka interview yake yote ya leo wakati akihojiwa akiwa uhamishoni nchini Afrika Kusini.

View: https://x.com/Sentletse/status/1885998079419003033?t=XrJ7G6I2xDOUSU6Sr__OXg&s=19

soon watampa silaha huyohuyo aende akamnyooshe kagame, na kagame anamwogopa sana huyo jamaa kwa sababu walikuwa wote, anajua uwezo wake sana.
 
Mkuu ukiwa ugenini huna ulinzi huna bacl up huna inforner wako uko alone unajificha sana...kosa kujulikama unapoishi.....miaka inaenda huwajui new recruits huwa wanauawa kirahisi sana hata na wahudumu wananunuliwa.....sukia tu ukiwa uhamishonii.....lolote laweza kutokea....PK ana pesa chafu kupoteza....hata miaka 10 anakutumia watu tuu wengine wanasoma wengine biashara....wengine wanawanunua watu wako karobuuu watajua tu....traces kupewa pesa zako watajua address yako....au kwenda bank kutoa pesa kula matumiziiii......sikia tuu mkuuu....watu 10 wapewe kaxi track wewe miaka 5 mingi watajua kitu tuuu
Mkuu unamsemea Leutenant General, former Chief of Staff wa jeshi, jasusi, Balozi. Haya unayoandika hapa sio ya wewe kumfundisha yeye, ni ya yeye kutufundisha sisi.

Uliyoandika almost yote kayafanya kama maagizo au mikakati yake kwa ngazi za kati mpaka ngazi ya juu jeshini. Mpaka anafikia kutuhumiwa kumpa challenge Kagame unahisi alikuwa level za kuwa boya mwoga; kutoroka mamlaka, mpaka anasalimika kuuwawa. Unahisi ni kiazi kama unavyomuandika hapa?

Nasema hivi, zipo level ambazo mtu akifikia plus matendo aliyofanya kumtishia kifo ni kujisumbua tu. Anakijua kifo kukuzidi, ameshuhudia vifo, ameshiriki kuua, ameagiza kuua. Sasa kuanza kumuelekeza Rwanda wanaua hivi na vile wakati ndio kazi zake hapo unanishangaza.
 
Muda ni.mwalim mkuu ugenini bila ulinzi rasmi ni shida...kumbuka kuna mtu anakusaka akuue....uliowafundisha ndio wanakusaka wakuue.....sawa àcha tuone...namuombea maishacmarefu tujye mengi
 
Wewe bana na huyo JPM wako. Si umfuate huko umsaidie kuendelea kukusanya kuni.
20250131_160335.jpg
 
Nyamwasa walikuwa pamoja na Kagame muda wote kuanzia miaka ya 1990's mpaka 2010 ilipoonekana Kagame anataka kumuondoa kabisa serikalini akakimbilia Africa Kusini ndipo akaanza kutoa hizi tuhuma zake.
Sawa nakubali.

Ninachokuuliza mkuu, kama Lt. Gen. Nyamwasa anayosema unadai ni porojo kisa ana kesi za UN, je madai ya Kagame nayo ni porojo kisa ana kesi za UN?

Na hayo makosa anayotuhumiwa nayo na UN Nyamwasa kwani aliyafanya akiwa individual mfanyabiashara? Si alikuwa chini ya RPF inayoongozwa na Kagame, si ni agenda za kina Kagame zile.
 
Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.
Hili nimelisoma kwenye makala nyingi sana..... kiufupi Kagame anatamani mno kuwa na Ushawishi huko Drc kuizidi Uganda na Burundi mahasimu wake wa kikanda.

zitto junior JokaKuu
 
Muda ni.mwalim mkuu ugenini bila ulinzi rasmi ni shida...kumbuka kuna mtu anakusaka akuue....uliowafundisha ndio wanakusaka wakuue.....sawa àcha tuone...namuombea maishacmarefu tujye mengi
Bado hunielewi mkuu. Ninacholenga kumaanisha ni kwamba Lt. Gen. Nyamwasa sio level ya mtu wa kumtishia na kifo.

Hawa kina Kagame na Rwigyema wangeogopa vitisho vya Habyarimana si wangelima viazi mbatata mpaka uzeeni? Hawakuogopa, mwishowe aliyekufa ni Rwigyema na wengine kina Kagame wakabaki.

Nyanwasa anajua risk factors zote kabla hata hatujamjua.
 
Ni nani huyu mkuu? Fuatilia historia yake. Si kila kisemwacho ni ukweli au uongo. Huyu bwana kumbuka alikimbia nchi. Alikuwa mwanajeshi! Automatically ni traitor. Unategemea angesema lipi jema? Sawa,huenda anayoyasema anazo taarifa za uhakika.
Mtoa mada naona arekebishe heading yake
Tuambie wewe unaye jua kuliko yeye m23 wanasadiwa na nani?
 
Mnasahau hapo aliposema Rwanda inaiba madini yenyewe bila msukumo au ushirikiano wa taifa lolote la nje!
Kwahiyo hii point unaikubali na hauwezi kuiita ni porojo, ila nyinginezo zinazomuweka Kagame hatiani unaona ni porojo kisa Nyamwasa ana tuhuma UN.

Wacha inyeshe tujue panapovuja.
 
Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.
Hata ripoti za UN na mataifa makubwa kama US,UK, France, Germany wanakiri hili......RDF inapigana bega kwa bega na M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.
Huyu PK ataleta vita vibaya vya kikanda kama vile vya vita ya pili ya Congo.....
Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.
Rwanda is a ticking time bomb

T14 Armata zitto junior JokaKuu
 
Na mi nimekiongea Humu, Banyamulenge Wapo Against M23, so kisingizio cha kwamba wao wanasaidia raia wa Congo Mashariki hakina tena mantiki, M23 ni Rwanda 100% hawana legitimacy yoyote ya wao kuwepo Congo.
Kabisa mkuu....

M23 ni 'project' ya Rwanda ndani ya Drc hao wacongo wanaoiongoza wanatumika tu na Kagame kama ilivyokuwa kwa kina Bosco Ntaganda na Laurent Nkunda.
 
Back
Top Bottom