Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Mkuu wa Ujasusi wa Rwanda, Lt. Gen Kayumba Nyanwasa, asema Kagame ni chanzo cha matatizo yote Congo na maziwa makuu

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.
Ni nani huyu mkuu? Fuatilia historia yake. Si kila kisemwacho ni ukweli au uongo. Huyu bwana kumbuka alikimbia nchi. Alikuwa mwanajeshi! Automatically ni traitor. Unategemea angesema lipi jema? Sawa,huenda anayoyasema anazo taarifa za uhakika.
Mtoa mada naona arekebishe heading yake
 
Aliyewahi kuwa mkuu wa ujasusi Rwanda na Balozi wa Rwanda nchini India, Lt. Gen Kayumba anasema matatizo yote yanayotokea mashariki ya Congo yanasababishwa na kagame.

Anasema Congo hamna tena tatizo la Banyamulenge ,lilishakwisha zamani na wana haki sawa na wanahudumu hata sasa katika serikali ya Congo.
Anasema kagame amekuwa Congo zaidi ya miaka 30 akiwaua wahutu wa Fdrl baada ya Genocide mpaka leo, na kwamba hana kisingizio tena kuhusu Fdrl nchini Congo.

Anasema M23 wameiburiwa upya na Rwanda 2021 baada ya Tshikedi kuingia makubaliano na Burundi na Uganda, ndipo Kagame alichukia na kusema kama hajakaribishwa atajikaribisha mwenyewe.

Amekiri Rwanda inaiba madini Congo na kupeleka Rwanda kwa ajili ya kuyauza nje na anasema kila eneo wanaloshika M23 lenye madini, madini uanza kusafirishwa haraka kwenda Rwanda.

Anakiri RDF inatoa sapoti ya 100% kwa M23.

Anasema Rwanda akiikamata Kivu yote, ataivamia Burundi na huo ndio mpango.

Anakiri ndani ya Rwanda wahutu wamefungwa minyororo na kufuri hawana pakuongelea na hawana mtetezi.

Anakiri Rwanda ina wakimbizi wengi wahutu na watusi ambao hawakubalina na sera na utawala wa kagame, na kwamba kagame asipowasikiliza kuna hatarii ya kutokea Genocide nyingine Rwanda.

Kumbuka huyu Mtusi kama ilivyo kwa kagame.

Hapa chini nimeweka interview yake yote ya leo wakati akihojiwa akiwa uhamishoni nchini Afrika Kusini.


View: https://x.com/Sentletse/status/1885998079419003033?t=XrJ7G6I2xDOUSU6Sr__OXg&s=19

Duh aisee halafu PK akiambiwaga ukweli kuhusu hili anakuwa mkali kweli.... Tatizo ni nani wa kumfunga Paka kengele?
 
Kwamantiki hyo naona M23 wametumwa na PK kwa lengo la kuiba madini kama inavozoeleka... lakini pia anawafata Wahutu waliopo Congo kwenda kuwadhibiti..lakini pia anaoneka anampango wa siri wakuja kumega sehemu ya Congo..lakini pia anaonekana ni kibaraka wa wazungu..lakini pia anafanya hvo ilikuona nani anasiraha kali zaidi yake upande wa Afrika mashariki na kati..lakini pia kubwa zaidi kisasi na Wahutu bado kipo..lakini pia anaonekana anatamaa kubwa kupita kiasi...Mwisho kabisa anaonekana ni Kirusi cha Afrika mashariki na kati ambacho kinapaswa kuuliwa au kutolewa kisije kuleta machafuko makubwa ya nchi hizi...Nimemchambua nimemaliza tukiendelea kumlea tusijutie baadaye.
 
Back
Top Bottom