Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Martin Gifhin mkuu wa shirika la afya duniani amesema ikiwa umoja wa mataifa umeshindwa kuizuia Israel isiendelee kuua watu wasio na hatia Gaza basi hakuna haja ya kuwepo umoja huo.
Maelezo hayo ameyatoa leo na kunukuliwa na vyombo vya habari kikiwemo aljazeera baada ya kupokea taarifa ya idadi kubwa ya wagonjwa kufariki kwenye hospitali mbali mbai za Gaza baada ya kukatiwa huduma zote za kihospitali ikiwemo umeme,maji na chakula pamoja na madawa.
Mapema akitoa taarifa yake leo,meneja wa hospitali ya alshifaa amesema wagonjwa wote 22 kwenye vyumba vya mahututi wamekufa kutokana na kukosa huduma na hewa ya oxygen.
Hayo yakitokea Gaza hospitali nyengine zimeendelea kuvamiwa kule ukanda wa magharibi sambamba na mashambulizi ya kijeshi kwenye kambi kadhaa za wakimbizi kwani idadi kubwa ya wapalestina wa maeneo hayo wanaishi kwenye kambi za wakimbizi kama vile Jenin na Tulkarem.