Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

Mara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.

Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happy es Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura

Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe

Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.[/QU
Watanzania tuache majungu,popote ulipo chapa kazi.Kila mtu atavuna alichopanda,na yeye aliwekeza nguvu najitiada zake kujenga network yake,mwache ale matunda ya jitiada zake.
 
Kesho waziri wake nae akiteua ndugu yake ataweza hata kumuhoji kama yeye keshaanza kuonyesha mfano mbaya?

Kama anazo Sifa na Vigezo Kwa nini asimchague?!! Tena Ana uhakika na tabia yake na uwezo wake tofauti na mwingine ambaye hata Kama anazo Sifa Kwa maana ya makaratasi siyo rahisi kujua uwezo na tabia Zake...... ,
 
Sifahamu ulilenga tufahamu kitu gani - funguka zaidi kwa hata hivyo si vibaya wala kosa mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi. Akiwa na sifa ateuliwe hata kuwa katibu mkuu au balozi
 
Wakuu wa wilaya kama wateule wengine wa rais serve at the pleasure of the president. Rais ana dira na viwango alivyopanga. Katika vigezo vitatu alivyo sema katibu mkuu kiongozi sijaona kugombea ubunge maalum kama kigezo. You are not telling the truth.

Suala la conflicts of interest ni legitimate argument lakini inanonekata Happy ana sifa za kutosha. Niambie ktk vigezo vilivyotajwa na Katibu Mkuu Kiongozi ni kigezo gani hana? Speaking of kuwa na Masters degree; yes, I will take that as an accomplishment.
Poor arguement. Conflict of interest haiangalii sifa ya mhusika huangalia tu mazingira yaani kuna mazingira ambayo yanaweza kuwa yametoa upendeleo kutokana na mhusika kuwa na maslahi na mhusika.

Sifa ulizozitaja inawezekana kweli anazo lakini je hizo sifa ni yeye tu aliye nazo? Hakuna wengine walio na sifa kama yeye au kumzidi. Ni nini kilichomtofautisha yeye na hao wengine? Kwa kuwa hatujui, ndiyo maana kimaadili haitarajiwi kumpa kitu chochote chenye manufaa mtu ambaye wewe una maslhai naye kwa kupitia nafasi uliyopewa na umma. Hapa uteuzi huu unafanana kabisa na angalizo alilolitoa Mwalimu kuhusiana na corruption. Mwalimu alisema, 'corruption ipo katika mataifa mengi lakini mbaya zaidi ipo Africa. Asia mtoto wa Rais au mjomba wake atapewa tenda ya kutengeneza barabara, na barabara itatengenezwa, tena kwa viwango sahihi. Corruption ya Africa, tenda ya barabara atapewa mtoto au mjomba wa Rais, hela italipwa na barabara hamtaiona, lakini zote ni corruption.' Kama huyu mteule ana uwezo na sifa, kazi itafanyika lakini haitafuta ukweli kuwa kuna ukosefu wa maadili.
 
Naona hapo hakuna shida hawezi kuwa kama yule mnyama aliyegawa mikia ikaisha akajisahau kikwetu ndilila mpaka kesho inalilia mkia
 
MAKUBWA HAYA MFUNGO MWEMA JAMAN WANA JF WALIOFUNGA
 
Na pia kama Raisi Magufuli kulingana na maneno yako hana tofauti na Raisi Museveni pia hana tofauti na JF Kennedy Raisi wa 35 wa USA ambaye alimteua kaka yake Robert kuwa Mwanasheria Mkuu wa USA (Attorney General), hivyo usiishie kutoa mifano ya nchi masikini tu kutaka kuthibistiha unachokiamini tolea mifano pia na Wazungu wenu!
Wanajeshi wastaafu bana, anyway hivyo unataka kuhalalisha uwepo wa janete ndani ya mawaziri uganda? Au yule makamu wa rais kule so unasema inaruusiwa nasi kufanya kama alivyofanya mkulu daaah sijui tumelishwa nini jamen
 
Ngoja nichangie fasta kabla Uzi huu haujapigwa ban. Mleta Uzi umetuletea mada fikirishi. Tukumbuke JK alisema serikali yake haina ubia na mtu lkn matokeo yake tumeyaona, maswahiba kwa utitiri na ndugu. Mwingine aliwekwa getini kazi yake ni kukuunganisha Bwana Mkubwa then unamlipa 5m ili upige picha na bosi wake kuwatishia TRA ofisini.

JPM amedai hana wa kumlipa fadhila lkn tumeona swahiba Kitwanga na yule mbunge wa Mwanza wakiteuliwa uongozini. Sasa tunajadili "mtoto wake" wa kufikia. Kwanza alikuwa Tanroad wizara ya "baba" kabla hajawa Rais. Sote tunajua urafiki wa KARIBU Kati na baina ya Magu na Bosi wa Tanroad. Utasemaje "mtoto" hakubebwa toka huko hadi sasa U-DC?

Hoja si uwezo maana wenye uwezo kama huo ni wengi. Hoja ni nchi iliyooza kwa nepotism namna hii kwa mtu uliyetangaza kwenda tofauti ni lazima tuhoji. Na je, ni huyo pekee? Huko Tanroad alishindanishwa na nani?? Mods, sasa mpige tu ban Uzi huu.
Very well said.
 
Kama ingekuwa ww unaishi na ndugu yako, sifa zoooooooote anazo, utaacha kumsaidia ?
Kuwa kiongozi ni kujitoa, ni kuwa sadaka. Ukitaka kuwa kiongozi ujue kuna mambo utayakosa na kuna ambayo utapata ambayo wengine hawapati. Hali kadhalika familia yako nzima. Bila ya kujali kama sifa anazo au hana, huu ni ukosefu mkubwa wa uadilifu katika uongozi. Lakini kwa sababu ni Afrika, yupo sahihi sana.
 
Wengi wamezoea kumuita "Happy Magufuli" kwa sababu amekulia na kulelewa na huyu mzee na hata kumsomesha.Nafikiri alianza na Ualimu Kigurunyembe Morogoro,baadae akaenda UDOM akasoma BBA na kisha alienda nje ya nchi kufanya Masters

Mara ya mwisho alikuwa Tanga TANROADS....Watu wa TANROADS Tanga wanampata(Wizara ya Baba)
Kweli kapata Wilaya ya Kisarawe
Usishangae sana mtu anabebwa taratiiiibu mwishowe utamkuta ni Katibu Mkuu au Balozi wetu kule Vienezulla.
 
Mara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.

Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happy es Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura

Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe

Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.
Kwa hiyo?
 
Wanajeshi wastaafu bana, anyway hivyo unataka kuhalalisha uwepo wa janete ndani ya mawaziri uganda? Au yule makamu wa rais kule so unasema inaruusiwa nasi kufanya kama alivyofanya mkulu daaah sijui tumelishwa nini jamen


Kwa nini unamshikilia Museveni tu lakini haumuongelei JF Kennedy aliyemteua kaka yake Robert Kennedy kuwa Mwanasheria Mkuu wa USA?
Kama hiyo haitoshi Raisi wa Poland ambaye sasa ni marehemu Lech Aleksander Kaczyński alimteua kaka yeke kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo hapo vipi? Kwa nini umemshikilia Museveni tu kama mfano lkn hawa Wazungu unakwepa kuwaongelea?
 
Isitoshe sio baba yake wa kumzaa shida iko wapi hapo?. Tatizo tunalolikataa wananchi ni kubeba mtu asiyebebeka...huyo dada anayo elimu nzuri tu...
Hata kama angekuwa baba yake wa kumzaa - hakuna shida yoyote kama mteuliwa anakidhi vigezo na masharti. Hacheni vitina za kishamba jamani
 
Kama sifa na vigezo anavyo ulitaka aachwe ugewe we we acha wivu
 
Back
Top Bottom