Tetesi: Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli

 
Kesho waziri wake nae akiteua ndugu yake ataweza hata kumuhoji kama yeye keshaanza kuonyesha mfano mbaya?

Kama anazo Sifa na Vigezo Kwa nini asimchague?!! Tena Ana uhakika na tabia yake na uwezo wake tofauti na mwingine ambaye hata Kama anazo Sifa Kwa maana ya makaratasi siyo rahisi kujua uwezo na tabia Zake...... ,
 
Sifahamu ulilenga tufahamu kitu gani - funguka zaidi kwa hata hivyo si vibaya wala kosa mtoto wa kiongozi kuwa kiongozi. Akiwa na sifa ateuliwe hata kuwa katibu mkuu au balozi
 
Poor arguement. Conflict of interest haiangalii sifa ya mhusika huangalia tu mazingira yaani kuna mazingira ambayo yanaweza kuwa yametoa upendeleo kutokana na mhusika kuwa na maslahi na mhusika.

Sifa ulizozitaja inawezekana kweli anazo lakini je hizo sifa ni yeye tu aliye nazo? Hakuna wengine walio na sifa kama yeye au kumzidi. Ni nini kilichomtofautisha yeye na hao wengine? Kwa kuwa hatujui, ndiyo maana kimaadili haitarajiwi kumpa kitu chochote chenye manufaa mtu ambaye wewe una maslhai naye kwa kupitia nafasi uliyopewa na umma. Hapa uteuzi huu unafanana kabisa na angalizo alilolitoa Mwalimu kuhusiana na corruption. Mwalimu alisema, 'corruption ipo katika mataifa mengi lakini mbaya zaidi ipo Africa. Asia mtoto wa Rais au mjomba wake atapewa tenda ya kutengeneza barabara, na barabara itatengenezwa, tena kwa viwango sahihi. Corruption ya Africa, tenda ya barabara atapewa mtoto au mjomba wa Rais, hela italipwa na barabara hamtaiona, lakini zote ni corruption.' Kama huyu mteule ana uwezo na sifa, kazi itafanyika lakini haitafuta ukweli kuwa kuna ukosefu wa maadili.
 
Naona hapo hakuna shida hawezi kuwa kama yule mnyama aliyegawa mikia ikaisha akajisahau kikwetu ndilila mpaka kesho inalilia mkia
 
MAKUBWA HAYA MFUNGO MWEMA JAMAN WANA JF WALIOFUNGA
 
Wanajeshi wastaafu bana, anyway hivyo unataka kuhalalisha uwepo wa janete ndani ya mawaziri uganda? Au yule makamu wa rais kule so unasema inaruusiwa nasi kufanya kama alivyofanya mkulu daaah sijui tumelishwa nini jamen
 
Very well said.
 
Kama ingekuwa ww unaishi na ndugu yako, sifa zoooooooote anazo, utaacha kumsaidia ?
Kuwa kiongozi ni kujitoa, ni kuwa sadaka. Ukitaka kuwa kiongozi ujue kuna mambo utayakosa na kuna ambayo utapata ambayo wengine hawapati. Hali kadhalika familia yako nzima. Bila ya kujali kama sifa anazo au hana, huu ni ukosefu mkubwa wa uadilifu katika uongozi. Lakini kwa sababu ni Afrika, yupo sahihi sana.
 
Usishangae sana mtu anabebwa taratiiiibu mwishowe utamkuta ni Katibu Mkuu au Balozi wetu kule Vienezulla.
 
Kwa hiyo?
 
Wanajeshi wastaafu bana, anyway hivyo unataka kuhalalisha uwepo wa janete ndani ya mawaziri uganda? Au yule makamu wa rais kule so unasema inaruusiwa nasi kufanya kama alivyofanya mkulu daaah sijui tumelishwa nini jamen


Kwa nini unamshikilia Museveni tu lakini haumuongelei JF Kennedy aliyemteua kaka yake Robert Kennedy kuwa Mwanasheria Mkuu wa USA?
Kama hiyo haitoshi Raisi wa Poland ambaye sasa ni marehemu Lech Aleksander Kaczyński alimteua kaka yeke kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo hapo vipi? Kwa nini umemshikilia Museveni tu kama mfano lkn hawa Wazungu unakwepa kuwaongelea?
 
Isitoshe sio baba yake wa kumzaa shida iko wapi hapo?. Tatizo tunalolikataa wananchi ni kubeba mtu asiyebebeka...huyo dada anayo elimu nzuri tu...
Hata kama angekuwa baba yake wa kumzaa - hakuna shida yoyote kama mteuliwa anakidhi vigezo na masharti. Hacheni vitina za kishamba jamani
 
Kama sifa na vigezo anavyo ulitaka aachwe ugewe we we acha wivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…