Hapa tunajadiliana na watu ambao hawana hata ABC ya uongozi. Ni watu waliojaa mahaba na mapenzi kwa chama. Ninyi hamna msaada kwa Taifa.
Watu wamebaki kwa kusema mbona utawala uliopita ulimweka fulani na fulani, wanachoshindwa kujua ni kuwa binadamu yeyote mwenye akili hatafuti kushindanishwa katika uovu. Halafu kuna hoja za kijinga kabisa kuwa mbona Ridhiwani alikuwa mbunge. Lakini Ridhiwani hakupewa ubunge na Baba yake bali alichaguliwa na wananchi. Huyo dada angekuwa amepata nafasi kwa kuchaguliwa na wananchi, kusingekuwa na hoja. Kama huyo binti angekuwa kwenye nafasi ya kitaalam kusingekuwa na shida. Lakini yeye amepewa nafasi ya kisiasa na mtu mwenye maslahi naye, ambaye kwa vyovyote vile au uteuzi wake, au mwenendo wake, au hatua dhidi yake au maumuzi yoyote dhidi yake, yanaweza kuathiriwa na mahusiano ya kifamilia.
Kama ni kweli haya yanayotamkwa, basi huyu atakuwa ndiye kiongozi wa kwanza Tanzania kumteua mwanafamilia kwenye nafasi ya kisiasa.