Kazi ipo kweli kweli...!!
Hivi hapa Tanzania, umeshawahi kusikia mtu binafsi (individual) ana mamlaka ya kuweka mipaka ya wilaya, yaani mtu binafsi anaamua mpaka kati ya wilaya fulani na wilaya nyingine upite hapa..!!
Hii ni kazi ya serikali (wizara ya ardhi na tamisemi). Lakini kule Kisarawe hii ni kazi ya wafugaji wa wilaya hiyo.
Wanaamua mpaka wa wilaya yao ya Kisarawe uwe hapa... hivyo 'wanajimegea' maeneo makubwa ya wilaya jirani huku mkuu wa wilaya akiangalia tu..!!
Amini usiamini hii imetokea Tanzania hii hii yetu, tena mwaka huu huu 2016.
Kazi ipo...!!!