Mkuu wa Wilaya na Wakuu wa Shule za Sekondari Wanena Kuhusu Umuhimu wa Mfuko wa Jimbo

Mkuu wa Wilaya na Wakuu wa Shule za Sekondari Wanena Kuhusu Umuhimu wa Mfuko wa Jimbo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MKUU WA WILAYA (DC) NA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WANENA KUHUSU UMUHIMU WA MFUKO WA JIMBO

Jana, Ijumaa, 24.3.2023, Wakuu wa Shule za Sekondari za Musoma Vijjini, na Bodi zao, walianza kuchukua vifaa vya ujenzi vilivyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo.

*Manunuzi yalifanywa na Halmashauri yetu (Musoma DC) kama ifuatavyo:

Jumla ya Fedha: Tsh 75,796,000
*Saruji Mifuko (50%) 1,613
*Mabati (40%) 947
*Nondo (10%) 337

Vifaa hivyo vitatumika kuanza ujenzi na ukamilishaji wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry & Biology) kwenye Sekondari zilizogawiwa vifaa hivyo (rejea taarifa yetu ya awali kuhusu suala hili kwa kutembelea Tovuti ya Jimbo letu: www.musomavijijini.or.tz)

Kuwepo kwa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zetu zote 25 za Kata ni sehemu ya matayarisho ya kuanzisha HIGH SCHOOLS za Masomo ya Sayansi kwenye baadhi ya Sekondari hizo.

Tafadhali wasikilize:
*DC Mhe Dkt Khafan Haule
*Wakuu wa Sekondari

Kwenye VIDEO CLIPS zilizoambatanishwa hapa, wakieleza umuhimu ya uwepo wa Maabara za Masomo ya Sayansi kwenye shule zetu, umuhimu wa uwepo wa Mfuko wa Jimbo, na shukrani zinazotolewa kwa Serikali yetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 25.3.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-25 at 17.19.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-25 at 17.19.15.jpeg
    100.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom