Mkuu wa Wilaya ya Bukoba apingana na wananchi wake, aunga mkono kumegwa kuunda mkoa wa Chato

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba apingana na wananchi wake, aunga mkono kumegwa kuunda mkoa wa Chato

Wahaya ni wakabila sana. Wilaya za muleba, bukoba na misenyi ndizo za wahaya na wanyambo wakiwa karagwe na kyerwa.

Ngara ina wahangaza na washubi, washubi wapo rulenge.

Biharamulo ya wasubi, ingawa kwa sasa imekaliwa na wasukuma kwa maeneo ya vijijn.

Magufuli alilazimika kutumia nguv ya uwazr kudai wilaya ya chato na chato kuihamishia mkoa wa geita kwa wasukuma. Alikuwa amepga hesabu kuwa mbelen kamati za siasa za wilaya na mkoa zingemchafua asipate ubunge pale wahaya wa chato walipokuwa wanaliwinda jimbo.

Taasis za uma zkiongozwa na asiye mhaya kwa wilaya za wahaya huwa hapewi ushrkiano.

Wahaya achen ukabira.
Hawapewi ushirikiano kwa sababu wanahujumu mkoa. Mtu kama huyu Mosses Machali amejaa chuki tupu kwa wahaya unategemea asimamie miradi ya maendeleo ya mkoa?
 
Wenyewe wanasemaje?

Habari za leo Friends of Bukoba.

Hii hapa ni video ya watetezi wa Mkoa wa Kagera zidi ya hujuma za Mkoa wa Chato.



Tunawashukuru wote walioshiriki ikiwa ni pamoja na:

(1) Mh. Bernedetha Mushashu (Mbunge viti maalum)

(2) Mh. Charles Mwijage (Muleba Kaskazini)

(3) Mh. Dr. Oscar Kikoyo (Mbunge Muleba Kusini)

(4) Mh. Jackson Rweikiza (Mbunge Bukoba Vijijini)

Shukrani kwa wote walioshiriki katika kupinga kumegwa kwa Mkoa wa Kagera ili kuunda Mkoa wa Chato. Hawa wenzetu wamepigana sana kutetea maslahi ya Mkoa wa Kagera na hasa zile wilaya zinazobaki zisizohofishwe kiuchumi, kisiasa na utamaduni. Kama mtakavyoona kwenye hiyo video, sasa mambo yote yanakwenda ngazi za juu za serikali kwa majadiriano na maamuzi. Kulingana na mtazamo wangu kuhusu maandishi na hotuba za watetezi mbalimbali, petition ya FOB, na hoja hafifu za wawakilishi wa Wilaya za Biharamulo na Ngara, katika mantiki ya kawaida sioni jinsi mtu anavyoweza kuruhusu kumegwa Mkoa wa Kagera. Itabidi uwe kipofu au kiziwi kufanya hivyo baada ya mambo yaliyoandikwa na kusemwa. Hata Hivyo, katika mfumo wa kerikali kama ya Tanzania ambapo mtu mmjo ana mamlaka kamili ambayo siyo lazima yategemee mawazo ya wengine au kundi (absolute power) lolote linawezekana. Therefore, keep our "fingers crossed".

ANGALIZO
Jambo la kushangaza sana katika hii video ni kuona Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (Mr. Moses Machali) akiwa msemaji mkuu na mkeleketwa wa kuunga mkono kumegwa kwa Mkoa wa Kagera na kumaanisha kwamba wale waliotoa hutuba za kupinga mkoa isimegwe ni wakabila. Nimejaribu kuangalia huyu mtu ni nani. Huyu ni mtu mwenye umri wa miaka 40, mzaliwa wa Kigoma na alikuwa Mbunge wa Kasulu. Alikuwa mwana chama wa CHADEMA (2007 - 2010), NCCR-Mageuzi (2010 - 2015), ACT Wazalendo (2015 - 2016) na CCM (2016-).

Hii ni rekodi mbuvu sana kwa mtu mwenye umri wa miaka 40. Mtu mwenye msimamo, busara na imani thabiti katika kitu chochote huwezi kuhama kirahisi namna hiyo. Kwa mantiki hii, huwezi kuwa kiongozi wa kundi au jumuiya yoyote kama mtazamo wako unakinzana ma matakwa au mahitaji ya kundi and jumuiya hiyo. Hii ndiyo maana ameshindwa kujua kwamba kama Mkuu wa Wilaya ya Bukoba ambayo ni moja ya wilaya zinazopinga kumegwa Mkoa wa Kagera kwa vile zitaathalika kiuchumi, hawezi kusimama hadhalani na kutoa hutuba kuunga mkono kudhohofishwa kwa Mkoa mama wa Wilaya yako. This cannot happen in public!

Unaweza kuwa na mtazamo tofauti na vilevile unaweza usiipende sehemu na watu ambao umekabidhiwa kuwaongoza, lakini inabidi ufiche hiyo nia yako kama inakinzana na matakwa ya watu wako. Je, huyu mtu anamtazamo gani kuhusu maendeleo ya Wilaya ya Bukoba na Mkoa wa Kagera kwa masuala mengine zaidi ya Mkoa kumegwa? Is this a person you can trust to defend you and resolve your problems? Ningekuwa Rais wa Tanzania, huyu mtu ningemuondoa kwenye hiyo nafasi siku hiyohiyo kwa vile ameonyesha kwamba hana maslahi ya sehemu na watu anaowaongoza.

Deogratias

Canada
MADINI HAYAENDI KOKOTE LAZIMA YABAKI KAGERA.
 
Back
Top Bottom