Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi apata ajali ya gari

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari katika Barabara ya Tanga- Segera eneo la Hale Wilayani Korogwe.

Kaimu RPC wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo "Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa Dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, Dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea"

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo DC Mwanukuzi "Majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo DC na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu na majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi"

Millard Ayo
 
kila tusikiapoajali za gari za serikali mwendo kasi,hivi ni dereva anaamuwa kukimbiza gari au boc,au ofisi inamwagiza?Ifike wakati madereva wachukuliwe hatua kama madereva a magari binafsi.Pole kwa majeruhi.
 
gari za wakubwaa huwa zinaendeshwa mwendo wa 80 - 140 km/hr, anyway get well soon
 
kila tusikiapoajali za gari za serikali mwendo kasi,hivi ni dereva anaamuwa kukimbiza gari au boc,au ofisi inamwagiza?Ifike wakati madereva wachukuliwe hatua kama madereva a magari binafsi.Pole kwa majeruhi.
Mara nyingi ni mabosi hua wanawaamrisha madereva watembee. Unakuta ameshachelewa sasa anamwambia dereva kanyaga saa mbili nna kikao ofisin.
 
Kwa mwendo kasi wa haya magari ukiringanisha na ajali zunazotokea naweza sema ni ajali chache sana haya magari ukiendesha yanakufanya ujisahau hata ukiwa 120km/h bado unaona uko na mwendo mdogo kutokana na ukaaji wake barabarani na upokeaji amri za dereva.
Hata ikiwa ni gari binafsi kama hizi za serikali utakimbia tu na tena walioko nje ndio wataona hilo ila ulioko ndani wala huhisi chochote .
 
Back
Top Bottom