Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi apata ajali ya gari

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi apata ajali ya gari

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari katika Barabara ya Tanga- Segera eneo la Hale Wilayani Korogwe.

Kaimu RPC wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo "Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo, Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa Dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, Dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea"

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo DC Mwanukuzi "Majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo DC na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu na majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi"

Millard Ayo

Mwendo kasi kwani wao hawana ving'amuzi? Usiku kwani RPC huko si alishapiga marufuku kusafiri usiku?
 
c7442ad9-1b96-4f75-ad83-c3f2b89f8a0e.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari katika Barabara ya Tanga-Segera eneo la Hale Wilayani Korogwe.

Kaimu RPC wa Tanga, David Mwasimbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Me 8, 2022.

“Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa Dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, Dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea,” – Mwasimbo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dk Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo DC Mwanukuzi.

“Majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo DC na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu na majeruhi mmoja tumempatia rufaa ya kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi,” amesema Dkt Gudemo


Source: Dar24
 
Pole zao.

Boss upo lakini dereva anafukia mashimo unamtazama tu.

Better umepona maana hata hiyo nafasi yako ni dili.
 
Pole sana kwake, hapo Segera kuna kona mbaya
Hale pamenyooka sana, mara nyingi gari za viongozi wa serikali hazina speed limit wala hazifuati sheria za barabarani hence kuwasababishia wengine ajali.

Ngoja waipate nao!
 
Mara nyingi ni mabosi hua wanawaamrisha madereva watembee. Unakuta ameshachelewa sasa anamwambia dereva kanyaga saa mbili nna kikao ofisin.

Pia hawazingatii uchovu wa madereva wao kama wanaweza kuendesha wakiwa wamechoka.
 
Back
Top Bottom