TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Esther Mahawe afariki Dunia

TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Esther Mahawe afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2025-01-14 at 16.07.11_9926ed7e.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe Esther Mahawe amefariki Dunia katika Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro kwa mujibu ya taarifa za awali zilizotolewa na ndugu wake wa karibu.
Snapinsta.app_463884599_1473719409976566_5468320198256054015_n_1080.jpg

Screenshot 2025-01-14 152149.png
RAIS SAMIA ATOA POLE
Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika Hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.

Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina.

Pia soma ~ RC Daniel Chongolo ashiriki katika mazishi ya aliyekuwa DC wa Mbozi, Ester Mahawe
 

Attachments

  • Screenshot 2025-01-14 152149.png
    Screenshot 2025-01-14 152149.png
    666.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom