TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Hamim Buzohera Gwiyama afariki dunia

TANZIA Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita, Hamim Buzohera Gwiyama afariki dunia

Ww hutakiw kuhoji haya maswali ok!
Mambo haya yanafikirisha:

1. Hawakuwahi kufa wakuu wa wilaya 2 ndani ya wiki 3.
2. Hawakuwahi kufa wabunge 3 ndani ya wiki 3.
3. Rais hakuwahi kubakia kwao kwa zaidi ya mwezi mzima.
4. Hatukuwahi kupata ugonjwa shughuli zote za shule zikastishwa.
5. Hatukuwahi kuwa na mazishi ya kusimamiwa na serikali.
6. Hatukuwahi kuwa na mazishi waombolezaji wasiozidi 10
7. Nk nk

Yote haya yanatokea katika kipindi hicho hicho.

Kweli haya hayahusiani na haka kaupepo?

Rais Magufuli dereva wetu kwa hakika unatupeleka kubaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
REST IN PEACE Mr Gwiyama, Hapa ndipo ninataka niwe na kipajia kama kile cha Mzee Mohammed Said katika kuandia Tazia ( na sio Taanzia kutokana na maelezo ya siku za karibuni) ili tuweze kuelewa Taifa limepoteza mtu wa namna gani. Kijana kutoka Magharibi ya nchi akiwa amejaliwa akili iliyotimamu. Nilikutana na Hamim kwa Mara ya kwanza kuwe Mkoani Ruvuma, akiwa kijana wa Form five katika shule ya wavulana Songea yaani box two. Tulitengeza uhusiano wa kuheshimina na kusaidiana katika kipindi hicho cha miaka miwili aliyokuwapo hapo. Gwiyama alikuwa mtaalam nzuri sana wa lugha na kipindi kile shule zikiwa na debate clubs, Ndugu alikuwa ni nzuri sana kwenye hii kitu na katika mwaka waliofanya vyema vizuri na wengi walipata nafasi ya kwenda chuo kikuu ni mwaka wao ambao karibu darasa zima la HGL waliamiana chuo kikuu na wale wa HGE walienda Economics wakiwa na watu kama wakina DR Banda, Dr Joseph (RIP), ambapo kumwetoa mawakili wengi na watu wenye nafasi zao katika idara mbalimbali kama akina Wakili A Mgongola, Dr Ndumbaro naibu waziri na wachumi wengi tu walioko kwenye mawizara mbambali. Ila Bwana Hamimu aliamua kujiunga na chuo cha IFM katika maswala ya uhasibu ambapo kwenye mwaka wa 1996 alimaliza ADA na akaendelea kupiga mitihani ya bodi ya uhasibu na hapa alipokuwa akisomea mitihani hii tukawa karibu tena maana mimi nilikuja Dar na nikatika watu waliomaliza CPA mitihani kwa single seat yaani wakati ule PIII na PIV akatunukiwa shahada ya juu ya uhasibu akiwa kijana mdogo hata hajaoa kwa kipindi kile. Kitu ambacho kilimfanikisha kuwa miongoni mwa maCFO wadogo nchini katika makampuni mbalimbali na kwenye miaka ya 1999 akaamua kuchukua pia muda kufundisha somo ya uhasibu tena mwaka wa 3 kwenye chuo kile kile alichopata elimu yaani IFM. Alikuwa mtu wa kupenda kusikiliza mcheshi na alikuwa anajua kusimamia kile alichokiamini kwa garama yoyote hata kama ingemgarimu maisha yake. Alikuwa kiongozi kwa watu waliokuwa karibu naye, alikuwa na upendo wa ajabu. Kwa kuwa yule aliyemuumba anakuwa na expire date tunamshukuru kwa kumleta mja wake kwetu na tukajifunza hayo tuliopata kujifunza na sasa amepumzika. Tunawaombea Mungu awape familia yake nguvu na mkeo Maua Mungu akutie nguvu sana akupe Subira katika kipindi hiki kigumu ila naamini kwa kumtanguliza Mungu mtapita salama. AMEN
 
Back
Top Bottom