Pre GE2025 Mkuu wa Wilaya ya Tanga akabidhi madaftari 1,000 yenye picha ya Rais Samia. Uchawa umefika kwa watoto wetu!

Pre GE2025 Mkuu wa Wilaya ya Tanga akabidhi madaftari 1,000 yenye picha ya Rais Samia. Uchawa umefika kwa watoto wetu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Japhar Kubecha akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya kwa kushirikiana na Taasisi ya Watoto Foundation wamekabidhi madaftari zaidi ya 1000 katika Shule tatu za msingi kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Jiji la Tanga.

Akiongea wakati wa kukabidhi madaftari hayo DC Kubecha amesema kuwa dhumuni la kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika sera ya elimu bila malipo kwa kutoa madaftari yenye picha ya Rais wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yatachochea juhudi za Watoto wa kuke kusoma ili kuweza kutimiza ndoto zao..

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watoto Foundation Ally Pingizi amesema kuwa ugawaji wa madaftari hayo ni harambee ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Watoto kusoma kwa bidi na kuwa na upendo na Rais Samia.

Madaftari hayo yenye picha ya Rais wamegawa bure kwa Shule ya Pongwe, Majani mapana, na Usagara kwa Watoto wenye mahitaji maalumu na wasio jiweza.

JPM alikuwa haitaji haya mambo ufanisi wake wa kazi ulikuwa inajieleza wazi, Yan ilifika hatua upinzani kulikuwa na hoja ya udikiteta tu
 
Baada ya kugawa pikipiki nchi nzima, sasa hivi wanagawa madaftari ya mama huko mashuleni. Kwanini haya madaftari yaje mwaka huu 2025? Tunawafundisha nini watoto wetu?
IMG_5404.jpeg
 
Kumbe Ile tetesi ya kumuweka kwenye pesa ilikuwa kweli kwa hii miangaiko

Watoto wenyewe hawataki kusikia kuhusu Samia, tatizo Samia hafanyi field analysis!!

Watoto wengi nchi hii wanampenda Sana Jk,na Hatari Magufuli
 
Nchi ina mambo ya kipuuzi puuzi... Hatutoendelea kamwe kwa ujinga huu
 
Haina shida mbona hata mbowe alitoa posho na nauli kwa wajumbe na hatujamchagua
 
Back
Top Bottom