Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika na Diwani wa Cheyo kufikishwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia kumfikisha mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo M. Buswelu kwa tuhuma za Ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Pia, Sekretarieti hiyo itamfikisha mbele ya Baraza hilo, Yusuph H. Kitumbo, Diwani wa Kata ya Cheyo, Manispaa ya Tabora mkoani Tabora kutokana na tuhuma hizo

Taarifa ya Sekretarieti imesema Baraza linatarajia kufanya Kikao cha Uchunguzi wa kina Juni 4 na 7, 2024 Saa 3 asubuhi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Malalamiko yaliyowasilishwa ambapo Wananchi wanaalikwa kuhudhuria kikao hicho.
 
Huenda utundu wao wa kurefusha kamba umewaponza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…