Mkwala, Debora na Ahoua ni wabovu, waondoke.

Mkwala, Debora na Ahoua ni wabovu, waondoke.

1. Mukwala ana chachawa sana hajatulia kabisa. Sijui ndio uwezo wake ulipoishia au ni kitete tu. Naona kama
anatumia nguvu nyingi sana kuliko maarifa/akili na ana haraka ya kutaka kukubalika na mashabiki wa Simba
matokeo yake anaharibu. Kuanzia mechi ya Yanga na hata hii ya leo na Coastal angetulia angefunga goli sio
chini ya mbili.
2. Benchi la ufundi lijitathimini. Simba sasa hivi ina wachezaji wenye kasi sana lakini timu nzima inacheza
taratibu sana. Hata pale Simba inapopokonya mpira wakati timu pinzani haijajipanga badala wapige
"counter attack" wao bado wamekaririri lazima waanze kupiga pasi fupi fupi kutokea nyuma.
3. Kusajili mshambuluaji mwingine kabla dirisha halijafungwa haikwepeki. Kwa daraja walilofika Simba sasa hivi Afrika Mukwala anapaswa awe mshambuliaji namba mbili. Ni lazima apatikane mshambuliaji anayeweza
kumaliza mechi mwenyewe hata kama timu nzima imekamatwa.
4. Debora bado namuona ni mchezaji mzuri ila naona kama benchi la ufundi linakosea namna ya kumtumia. Kwa upande wangu namuona kama namba 10 zaidi na sio namba 8. Nasubiri siku Kagoma na Okejepha
watakapocheza pale katikati halafu Debora akasogea juu kidogo namba 10 ndio nitapata nafasi ya
kumtathimini vizuri.
5. Ahoua nimemwangalia takribani mechi tatu sasa. Kilichokuwa kinasemwa juu ya ufundi wake ni tofauti kiasi
fulani na anachokionyesha uwanjani. Lakini walau leo kidogo kuna vitu fulani kaonyesha vimenishawishi
nimuone ni mchezaji mzuri. Mimi kwa upande wangu nampa muda nimuone zaidi maana inawezekana ni
aina ya wale wachezaji wakifika kwenye timu mpya wanachelewa "kuadopt" kutokana na vyakula, hali ya
hewa, mazingira, utamaduni, n.k.
6. Mutale mimi namuona ni bonge la mchezaji ila kakosa pacha pale mbele. Kwa kasi ile akipata pacha sahihi
ambaye anaweza kucheza vizuri "one two" wala Simba isingepata shida kwenye hizi mechi tatu zilizopita..
Huyu Mutale watu wanaosema ni machachari na sio hatari siku Simba ikipata mshambuliaji wakati kama
alivyokuwa Mugalu ambaye alikuwa anaweza "kuwahold" mabeki hata wawili kwa mpigo na bado akaficha
mali mpaka wenzake wafike/wapite hapo naamini ndio watu wataamini kama Mutale ni mali pale Simba.

Katika mechi mbili zilizopita niliiona kama Simba imebadilka kitabia ikiionyesha kuwa inatafuta matokeo na hata magoli zaidi. Walikuwa "aggresive" kweli kweli. Lakini leo dhidi ya Coastal wamenishangaza sana baada ya kupata goli moja timu ikarudia tabia zake zile zile za msimu uliopita za kuridhika na goli moja. Chonde chonde viongozi na hata benchi la ufundi wasipoifanyia kazi hiyo tabia mapema basi ubingwa watausikia tu kwenye redio hata kwenye mashindano ya Afrika hawatafanya vizuri. Wakumbuke kuwa sasa hivi kila timu ipo vizuri na mwishoni mwa msimu si ajabu magoli yakaamua mshindi hivyo ikitokea wamekutana na timu kibonde basi waitumie nafasi hiyo kufunga goli nyingi sio kuridhika na goli chache.

Ni mtizamo tu.
Sahihi kabisa, umepita mule mule. Hilo la mwisho ni la kusisitiza sana. Ni muhimu sana ufanisi kuongezea pale mbele, utaijengea timu confidence. Hii timu ikishapata confidence tu mambo mengine yatakaa sawa.
 
Simba timu ya siasa na propaganda utajikuta mashabiki wanajipa moyo timu haina muunganiko
Msimu uliopita mlisema Simba mbovu Yanga nzuri, lakini wote tulitolewa robo fainali Champion League. Hapo nani alimzidi mwenzake kwa ubora?
 
Back
Top Bottom