Mkwamo wa Bunge kikanuni bila kambi Rasmi ya Upinzani

Ndio maana nilisema kwenye baadhi ya uzi zangu kuwa, I'm so sure bwana Tundu Lisu lengo lake ni kuua upinzani na sio kuujenga

Analazimisha CHADEMA wasipeleke wabunge viti maalum wakati anajua fika kuwa bunge litatengua kanuni na maisha yataendelea kama kawaida

Kutokuwepo kwako bungeni hakuna chochote ambacho kitakwama
 
Wanakosa $900m kutoka kwa mabeberu
 
Wafanye vyovyote wanavyotaka, hilo bunge wameachiwa wakomae nalo.
Wameachiwa wakomae wakati mlikatiliwa na Wananchi kutokana na Sera zenu Sera hivyo ikiwa ni pamoja Ushoga
 
Bunge la 'Hapa kazi' mnataka wapinzani wa kazi gani ?
 
Wewe una uhakika gani kama kura ziliibwa na kama ziliibwa ulimkamata nani
 
Asante sana Mkuu. Ubarikiwe kwa Hoja yako Murwaa.
 
Mimi naona mnajiumiza vichwa bure tu.

Tanzania tayari ni FAILED STATE.

Mambo yote yanawezekana isipokuwa MAENDELEO TU, UTAWALA WA SHERIA, UTU, DEMOKRASIA na UBINADAMU.

Mwambe alirudi bungeni bila chama.

Mikutanaoya kisiasa ilipigwa marufuku miakayote mitano.

Watumishi wa umma hawakupewa annual increments miaka yote mitano.

Tundu Lissu kapigwa risasi GUNIA eneo lenye ulinzi mkali wa polisi na mpaka sasa hata sisimizi hajakamatwa.

Hussein mwinyi kasimikwa kijeshi kama Rais wa Zanzibar.

CAG alitumbuliwa.

Mahakama zinakataa kesi.

Sasa hilo jambo dogo la PAC na LAAC ndio linawauiza vichwa ??????
 
Ambacho umesahau ni kimoja nacho ndicho kinawapasua vichwa Ndugai na mbumbumbu wenzie,
2.4T haitaletwa kusapoti bajeti kama kamati hizo hazitaongozwa na wapinzani halisi na 1/3 ya wajumbe wake kuwa opposition MPs.
 
Kwa hiyo, mkuu, ulitaka watanzania wabunge wa vyama ambavyo kimtazamo havina nia njema na Tanzania kisa kuna hitajika wenyeviti wa kamati za LAAC na PAC kutoka kambi rasmi ya upinzani!? Mleta mada kaliweka vizuri, hiyo kanuni itatenguliwa.
 
Sipika sio mbumbumbu na wabunge jielewe hebu badilika
 
Kwa sasa hamna sheria, bali utashi wa rais ndio sheria. Huu mchezo wa kutoheshimu sheria wazi wazi, nilianza kuuona wakati wa bunge la katiba, na sasa imekuwa ni muendelezo. Sasa hivi kukitokea mkwamo wowote wa kisheria, rais anasema tu hizo sheria zinatukwamisha na hii ni nchi huru, hivyo ndani ya dakika tano hiyo sheria inabadilishwa kuendana na utashi wa rais. Ukiona sheria inafuatwa ni Ile inayowabana wapinzani na wala sio watawala. Hivyo kwa sasa bwana Yakubu, ujue sheria zako ulizosomea zitakuwa zinatekelezwa kidictator.
 
Kwa hiyo, mkuu, ulitaka watanzania wabunge wa vyama ambavyo kimtazamo havina nia njema na Tanzania kisa kuna hitajika wenyeviti wa kamati za LAAC na PAC kutoka kambi rasmi ya upinzani!? Mleta mada kaliweka vizuri, hiyo kanuni itatenguliwa.
Why all that trouble, si wafanye wanavyotaka tu, nani atawauliza?
 
Kwa hiyo, mkuu, ulitaka watanzania wabunge wa vyama ambavyo kimtazamo havina nia njema na Tanzania kisa kuna hitajika wenyeviti wa kamati za LAAC na PAC kutoka kambi rasmi ya upinzani!? Mleta mada kaliweka vizuri, hiyo kanuni itatenguliwa.

Sasa kulitakia mema taifa kumekuwa na maana tofauti kabisa na uhalisia. Ili ionekane unalitakia taifa mema, inatakiwa uwe unamsujudia rais na kusifia kila atakacho, na ukienda kinyume na utashi wa rais na kumkosoa hasa hadharani, basi tafsiri ya wazalendo academia ni kutokulitakia taifa mema! Taifa letu kwa sasa limeguezwa kuwa la wazalendo wa mdomoni na sio moyoni, kiasi kwamba imekuwa ngumu kutofautisha mzalendo na mjinga.
 
Waliyofanya ya uchaguzi ndio yalikuwa magumu, haya ya PAC na LAAC ni madogo sana.

Acheni wafu wazikane, wala msiumize vichwa.

Shughuli ni hii safari mpaka 2025, sijui tutafika vipi. Maana hapo si CCM wala CHADEMA miguu itatuishia nguvu. Inshaallah!
 
Kwa jeuri waliyonayo, watengua kanuni 135(ii). Tusubiri kuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…