Mkwamo wa Bunge kikanuni bila kambi Rasmi ya Upinzani

Mkwamo wa Bunge kikanuni bila kambi Rasmi ya Upinzani

Mimi naona mnajiumiza vichwa bure tu.

Tanzania tayari ni FAILED STATE.

Mambo yote yanawezekana isipokuwa MAENDELEO TU, UTAWALA WA SHERIA, UTU, DEMOKRASIA na UBINADAMU.

Mwambe alirudi bungeni bila chama.

Mikutanaoya kisiasa ilipigwa marufuku miakayote mitano.

Watumishi wa umma hawakupewa annual increments miaka yote mitano.

Tundu Lissu kapigwa risasi GUNIA eneo lenye ulinzi mkali wa polisi na mpaka sasa hata sisimizi hajakamatwa.

Hussein mwinyi kasimikwa kijeshi kama Rais wa Zanzibar.

CAG alitumbuliwa.

Mahakama zinakataa kesi.

Sasa hilo jambo dogo la PAC na LAAC ndio linawauiza vichwa ??????
Shangaa na wewe! The genius Magufuli anaweza yooote kasoro Hilo Tu?.
 
A lawless country. There is nothing physical that can stop them acting any way they wish. "Walifunga mtandao na tukaufyata". They are next to God!!
They are not next to God. They are probably more than God.

You can criticize God and live freely but try to criticize Magufuli at your own peril.
 
Na ndio maana Ndugai aliahirisha bunge ili wabunge wakafanye shopping, kupiga selfie viunga vya bunge na wengine kuanzisha connection mpya huku nyie mawakili maslahi mkiangalia namna ya kutengua kanuni kisheria ili mlazimishe bunge lisonge 'kizombiezombie'.

Jiwe ni nuksi na laana ya Taifa.
Hoja ya kuahirisha bunge si ngeni,labda Kama umeanza kuangalia leo bunge
Halafu si umesusia matokeo wewe?kumbe unapiga chabo!!
 
Bashir Yakub hivi tatizo liko wapi, kama wameweza kuiba kura kifala namna hii, bila chembe ya aibu, si waendeshe bunge at their own leisure, kwani nani atawauliza? Kama wamefanya ubatili huu wa kura bila kuulizwa, na hili waendelee wanavyotaka. simple! lawlessness country!

Job aliapa Hakuna mpinzani atakaerudi bungeni why anawashwawashwa na kuikana ndoto yake iliyotimia.
 
Na Bashir Yakub, WAKILI

Kanuni ya 135(11) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za June 2020, inasema kuwa " Wenyeviti wa Kamati ya Hesabu za serikali(PAC), na Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) wanatakiwa kutoka Kambi Rasmi ya Walio wachache Bungeni".

Kwanza kwa Kanuni hizi mpya hakuna kitu kinaitwa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, bali imebadilishwa na kuitwa Kambi rasmi ya walio wachache Bungeni.

Kanuni niliyotaja hapo juu inatafsiri kuwa hapawezi kuwa na kamati PAC na LAAC bila kambi rasmi ya walio wachache bungeni.

Na ili iwepo Kambi rasmi ya walio wachache bungeni ni lazima wabunge wa upinzani wafikie 12.5% ya wabunge wote kwa mujibu wa kanuni ya 21.

Mkwamo wa bunge la sasa ni kuwa wabunge wote wa upinzani hawafiki 12.5% ili waweze kuunda hiyo kambi rasmi.

Na kama hawawezi kuunda hiyo kambi maana yake kamati ya PAC na LAAC haziwezi kuwepo kwakuwa haziwezi kupata mwenyekiti aliyetakiwa atoke katika hiyo kambi.

Na bahati mbaya Kanuni hazisemi nini kifanyike iwapo Kambi rasmi haipo, au ikiwa upinzani haujafikia 12.5%.

Je inawezekana Bunge kuendeshwa bila Kamati muhimu na za lazima kama PAC ya hesabu za serikali na LAAC ya hesabu za serikali za mitaa?

Jibu ni hapana haiwezekani. Jambo moja kati ya matatu litatokea.

Moja, hiyo idadi ya 12.5% ilazimishwe ipatikane ili Kambi Rasmi ya Waliowachache Bungeni iwepo ili Wenyeviti wa PAC na LAAC wapatikane.

Mbili, itumike kanuni ya 174 ambayo inatoa uhuru kwa mbunge yeyote, waziri, au mwanasheria mkuu wa serikali kuleta Hoja ya kuomba Kanuni yoyote katika Kanuni za Kudumu KUTENGULIWA kwasababu na malengo maalum.

Maana yake mleta hoja ataomba Kanuni ya 135(11) inayolazimisha wenyeviti wa PAC na LAAC kutoka kambi rasmi ITENGULIWE, na baada ya hapo mwongozo mpya utatolewa.

Tatu, itumike Kanuni ya 2(2) inayomtaka Spika kutumia Sheria nyingine, Maamuzi ya mabunge yaliyopita, mila na desturi za mabunge, ikiwa kuna jambo au shughuli imejitokeza lakini haijaelezwa kwenye kanuni.

Nauona mkwamo huu ukimalizwa na moja kati ya haya matatu.

Wasalaam.
Kanuni inaweza kubadishwa sioni shida hapo
 
Aisee

Acha uongo na unafiki

Lissu ndio ana final say kwenye chama cha chadema?

Kwanza kwa madaraka ya Lissu chadema Mnyika ana power zaidi yake...

Sasa sijui Lissu lini kaishika Chadema hostage ifanye anachotaka,plus maamuzi yote ya Chadema ni vikao na kura zinapigwa...sasa sijui kura ya Lissu ni kama ghorofa ina cancel all others?

Sijui Lissu anawatisha nini namna hii....

Such a group of dishonest lunatics!
Mahojiano ya Lisu na kubenea pale airport ulisikia?

Lisu ndio kashikilia chadema wasipeleke wabunge wa viti maalumu
 
Ambacho umesahau ni kimoja nacho ndicho kinawapasua vichwa Ndugai na mbumbumbu wenzie,
2.4T haitaletwa kusapoti bajeti kama kamati hizo hazitaongozwa na wapinzani halisi na 1/3 ya wajumbe wake kuwa opposition MPs.
Labda huo wasiwasi uwe ni siri ya watu fulani. Pongezi nyingi zinaendelea kutolewa kwa kuendesha uchaguzi kwa pesa za ndani ili kuepuka mabeberu wenye ajenda zao dhidi ya taifa; miradi mikuu ya kimkakati inatekelezwa kwa pesa za ndani; wananchi wanaaminishwa pesa zipo nyingi tu, kinachohitajika ni "connection" ili mheshimiwa azitoe na kupeleka kokote yanakohitajika maendeleo! Kwa jeuri ya aina hii iliyofikisha kupanga matokeo ya uchaguzi wanavyotaka, ni nani tena mwenye wasiwasi wa kukosa hizo 2.4T? Unafikiri huyo Ndugai ana habari na masuala ya uchumi?
 
Acha bangi wewe

Tunaongelea vikao na maamuzi ya chama yanatoka wapi?

Na kati ya Lissu,Mnyika na Mbowe nani na nani ana madaraka zaidi ya mwenzake?

Stop Lissu phobia hii
Jibu swali basi kama ujasikia tafuta
 
Na Bashir Yakub, WAKILI

Kanuni ya 135(11) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za June 2020, inasema kuwa " Wenyeviti wa Kamati ya Hesabu za serikali(PAC), na Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) wanatakiwa kutoka Kambi Rasmi ya Walio wachache Bungeni".

Kwanza kwa Kanuni hizi mpya hakuna kitu kinaitwa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, bali imebadilishwa na kuitwa Kambi rasmi ya walio wachache Bungeni.

Kanuni niliyotaja hapo juu inatafsiri kuwa hapawezi kuwa na kamati PAC na LAAC bila kambi rasmi ya walio wachache bungeni.

Na ili iwepo Kambi rasmi ya walio wachache bungeni ni lazima wabunge wa upinzani wafikie 12.5% ya wabunge wote kwa mujibu wa kanuni ya 21.

Mkwamo wa bunge la sasa ni kuwa wabunge wote wa upinzani hawafiki 12.5% ili waweze kuunda hiyo kambi rasmi.

Na kama hawawezi kuunda hiyo kambi maana yake kamati ya PAC na LAAC haziwezi kuwepo kwakuwa haziwezi kupata mwenyekiti aliyetakiwa atoke katika hiyo kambi.

Na bahati mbaya Kanuni hazisemi nini kifanyike iwapo Kambi rasmi haipo, au ikiwa upinzani haujafikia 12.5%.

Je inawezekana Bunge kuendeshwa bila Kamati muhimu na za lazima kama PAC ya hesabu za serikali na LAAC ya hesabu za serikali za mitaa?

Jibu ni hapana haiwezekani. Jambo moja kati ya matatu litatokea.

Moja, hiyo idadi ya 12.5% ilazimishwe ipatikane ili Kambi Rasmi ya Waliowachache Bungeni iwepo ili Wenyeviti wa PAC na LAAC wapatikane.

Mbili, itumike kanuni ya 174 ambayo inatoa uhuru kwa mbunge yeyote, waziri, au mwanasheria mkuu wa serikali kuleta Hoja ya kuomba Kanuni yoyote katika Kanuni za Kudumu KUTENGULIWA kwasababu na malengo maalum.

Maana yake mleta hoja ataomba Kanuni ya 135(11) inayolazimisha wenyeviti wa PAC na LAAC kutoka kambi rasmi ITENGULIWE, na baada ya hapo mwongozo mpya utatolewa.

Tatu, itumike Kanuni ya 2(2) inayomtaka Spika kutumia Sheria nyingine, Maamuzi ya mabunge yaliyopita, mila na desturi za mabunge, ikiwa kuna jambo au shughuli imejitokeza lakini haijaelezwa kwenye kanuni.

Nauona mkwamo huu ukimalizwa na moja kati ya haya matatu.

Wasalaam.
Mkuu wala usihofu; kwa CCM kutengua kanuni ni kazi ya dk tatu tu...na makofi ya ndiyoooooo.

Aafu cha kushangaza hata wananchi hawana munkari nalo... maana watu ni walewale na mambo ni yaleyale...!!
 
Mimi navyoona, litakuwa ni bunge la kutengeza matatizo halafu kuyatatua ili kutenegeza kick na kuweka kamvuto kidogo. Ila wameanza kuumbuka.
 
Back
Top Bottom