Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Kwa vile tumekubali watawala wavunje sheria hata kunyima stahiki za viongozi waliopita,basi ujue kama Taifa tunakazi kubwa ya kuvuka daraja.Na kitu kimoja kikubwa kinaitwa sheria ya dhahabu inasema'USICHOPENDA KUTENDEWA USIMTENDEE MWENZAKO" maana kuna siku utakuja tendwa usijue sababu.Na ukumbuke kila siku MKUKI MTAMU KWA NGURUWE NA KWA BINADAMU MCHUNGU.Leo furahia anachotendewa Maalim Seif kesho yako huwezi ijua.
Nakumbuka Rais Chiluba alipoingia madarakani alimtendea mambo kama haya Mzee Kaunda lakini naye alipo achia madaraka yakamkuta makubwa zaidi na ndio yalichangia hata kuondoka duniani mapema. Tujifunze kuacha sheria iongoze mambo yetu na hakuna atakayemlaumu mtu na sio kiburi na hisia kutuongoza.