Mkwasa jiuzulu mwenyewe, usisubiri kutimuliwa

Mkwasa jiuzulu mwenyewe, usisubiri kutimuliwa

Kwa kweli mi mwenyewe nilihamasika kuangalia game but leo ndio mwisho wa kuangalia. Taifa stars
 
mkwasa bado ni kocha mzuri tu, tatizo tff wazembe sana, inabidi wajue kucheza mpira nje na ndani ya uwanja, ila yamekaa kuwaza mapato tu
 
Ukweli Mkwasa uwezo wake mdogo ndio maana yanga walimpa ukocha usaidizi lakini mbali ya mkwasa mwingine wa kubeba lawama ni malinzi hii timu ilikuwa inafanya vizuri chini ya kim poulsen yeye akakurupuka na kuleta kocha bomu ndio hapo wapika majungu wakapata nafasi ya kupiga debe kocha awe mzalendo,halafu atueleze hiyo kamati tuliyounda imetusaidia niniwakati tuna cheza na malawi mechi zote mbili algeria walituma mtu wao kutusoma na kujua mapungufu yetu isi tulibaki na kuunda kamati
 
Pssssssss....aaaah
 
Attachments

  • 1447798217513.jpg
    1447798217513.jpg
    16.5 KB · Views: 294
Ukweli Mkwasa uwezo wake mdogo ndio maana yanga walimpa ukocha usaidizi lakini mbali ya mkwasa mwingine wa kubeba lawama ni malinzi hii timu ilikuwa inafanya vizuri chini ya kim poulsen yeye akakurupuka na kuleta kocha bomu ndio hapo wapika majungu wakapata nafasi ya kupiga debe kocha awe mzalendo,halafu atueleze hiyo kamati tuliyounda imetusaidia niniwakati tuna cheza na malawi mechi zote mbili algeria walituma mtu wao kutusoma na kujua mapungufu yetu isi tulibaki na kuunda kamati

hahaha mkuu umemaliza sana harafu nivituko vikubwa sana yaani kocha msaidizi anapewa ukocha mkuu?? wakati akiwa yanga huwa anakuwa chini ya MTU??

mpira unamambo mengi sana sisi bado sana tatizo mpira nao umekuwa na siasa nyingi sana ndani yake
 
Tangu nipate akili sijawahi kuona Timu ya taifa letu ikila kichapo cha mbwa mwizi kama hiki , unalipwa hela nyingi ili ufanye kazi lakini umeshindwa , tungeweza kufungwa ila si kwa kipigo cha kufedhehesha namna hii , ondoka mwenyewe usisubiri maandamano , umeshindwa mkuu .

Jamani, Huto tu milioni 12 kaanza kututafuna juzi tu!!!
Acheni hizo bana.
 
sasa mkwasa ndio alisababisha yule mpumbavu akapewa red?sisi watanzania ni malofa kweli leo nimeamini wachezaji baadhi wamecheza chini ya kiwango kabisa kana kwamba kuna walichopewa sielew nini kilitokea kuna michezaji ndio imetuangusha akiwepo yule punguani aliekula umeme mapema kabisa kwa faulu ya kisengerema sana
 
Mnaomlaumu kocha Mkwassa kwa matokeo mabaya ya timu ya Taifa hamjui historia ya michezo nchini kwa ujumla wake. Mlitaka kocha afanye nini au miujiza ga
 
Umesema mwenyewe hujawahi kuona timu ikifungwa goli kama hizo!!
hapo inatosha kujua wewe sio shabiki wa mpira wala huujui mpira,timu nyingi tena kubwa kubwa zimepigwa zaidi ya hizo goli,
sijaona sababu ya mkwasa kujiuzulu kwa hicho kipigo,kama tungekuwa tumefungwa hizo bao na comoro au Djibout hapo sawa,Algeria ni timu bora kabisa kwa afrika ,hata brazil angekuwa anacheza nao basi hana uhakika wa kuwafunga 100%
 
Tangu nipate akili sijawahi kuona Timu ya taifa letu ikila kichapo cha mbwa mwizi kama hiki , unalipwa hela nyingi ili ufanye kazi lakini umeshindwa , tungeweza kufungwa ila si kwa kipigo cha kufedhehesha namna hii , ondoka mwenyewe usisubiri maandamano , umeshindwa mkuu .

Jamani kwani mkwasa alicheza hata saudi Arabia inapigwaga nane bila world Cup
 
Mnaomlaumu kocha Mkwassa kwa matokeo mabaya ya timu ya Taifa hamjui historia ya michezo nchini kwa ujumla wake. Mlitaka kocha afanye nini au miujiza ga
Timu imepigwa kwa kiwango cha aibu bado mnataka tumchekee kocha ?
 
Umesema mwenyewe hujawahi kuona timu ikifungwa goli kama hizo!!
hapo inatosha kujua wewe sio shabiki wa mpira wala huujui mpira,timu nyingi tena kubwa kubwa zimepigwa zaidi ya hizo goli,
sijaona sababu ya mkwasa kujiuzulu kwa hicho kipigo,kama tungekuwa tumefungwa hizo bao na comoro au Djibout hapo sawa,Algeria ni timu bora kabisa kwa afrika ,hata brazil angekuwa anacheza nao basi hana uhakika wa kuwafunga 100%
ni lini Tz imewahi kutandikwa kwa kiwango hiki ?
 
Kiukweli kocha lazima alaumiwe,huwezi sema ati tumwache ilihali mapema tu kapanga beki dhaifu na kipa ovyo kabisa.Kipa gani anaanguka hasimami amelegea kama chapati.Huwezi acha kumlaumu kwa kuchagua kikosi kwa ushabiki wa Azam na Yanga.Timu ndogo ndizo zenye wachezaji wa viwango.Mpira wetu umejaa rushwa hivyo timu kubwa si za kuziamini kuunda timu ya taifa.
 
Huwezi kuwashinda waarabu bila ya kutofanya fitna.TFF wameshindwa kuweka utaifa mbele ili timu walau icheze shinyanga,ili waarabu wachoke na safari barabarani.TFF wapiga pesa tu! Wao wanajali kujaza uwanja na kupata pesa tu.Nchi haijawekeza kwenye academy za kila mkoa ili kuibua vipaji alafu eti uwashinde Algeria!! Huu ni mda sahihi kujitathimini,wizara ya michezo iweke malengo ya kweli na siyo dili tu.Aibu hii ni yetu sote japo Azam na Yanga waliunda timu.Poleni sana ndg zangu watanzania.
 
Back
Top Bottom