Mkwasa jiuzulu mwenyewe, usisubiri kutimuliwa

Hivi upo ugenini alafu unawaanzisha maguri, ulimwengu na samatta kwa pamoja unaaAKILI KWELI???
Tupigweeee tu maana hatujielewi.....
 
Kakosa nini? juzi alibadilisha kikosi kidogo mkaleta masiasa yenu mkamchimba biti. Sasa amewawekea wale mnaowapenda mwanzo mwisho yakatokea yaliyotokea. Wakulaumiwa ni wachezaji wa ALGERIA kwa nini wamejazia vile? kwa nini wana nguvu za miguu na maarifa kibao? kwa nini asilimia kubwa wanacheza ligi kuu duniani? kwa nini wanajua kupiga foul kiutaalamu namna hiyo? kwa nini wakifika kwenye koli hawalengi nje ya goli? Lawama zoote muwatupie hao na sii kocha mkwasa ambaye hana kiwanda cha kutengeneza wachezaji anaowataka zaidi ya kuwatumia hawa waliopo ambao uwezo wao ndio ulishaagota.
 
Nakushauri wewe ndio uachane na soka.
 
Ni hivi , kama kuna anayemhurumia mkwasa kwa ajili ya mshahara anaopewa ( ambao hakuwahi kuupata tangu Mungu aumbe dunia ) basi tufanye hivi , afukuzwe lakini tuendelee kumlipa , si mnamhurumia ! Nakuhakikishia kwamba chini ya mkwasa tutakuja kupata aibu zaidi ya hii .
 
Nakushauri wewe ndio uachane na soka.

Sing'oki kizembe mkuu , haiwezekani kuiacha aibu itambe , atang'oka mkwasa kwanza , malengo ya timu yoyote ya soka ni ushindi , si chenga twawala .
 
Sing'oki kizembe mkuu , haiwezekani kuiacha aibu itambe , atang'oka mkwasa kwanza , malengo ya timu yoyote ya soka ni ushindi , si chenga twawala .
Hata aje Guardiola tatizo la soka letu si kocha.
 
Siku zote Kocha ndio hulaumiwa hata kama makosa ni ya wachezaji coz kocha ndio "Leader" wa team,ni kama vile Kampuni ikipata hasara au uzalishaji ukipungua kwa uzembe tu, ni Meneja wa kampuni ndio hulaumiwa na sio wafanyakazi,


BUT tatizo la Taifa stars sio kocha ni "Foundation"
 
Suala hapa sio kufungwa magoli mangapi. Tatizo letu ni kuwa na timu bora ambayo itashiriki mashindao kwa ufanisi. Maadui wakubwa wa soka la Tanzania ni yanga na simba pamoja na tff ambayo inataka tuwe na timu bora bila kufuata taratibu za kuipata. Hata aje kocha wa aina gani kwa utaratibu huu hatuwezi kuwa na timu ya taifa iliyo bora
 
Umefika wakati wa kuiondoa timu yetu ya taifa kwenye michuano ya kimataifa ili kuepuka aibu zisizo za lazima .
 
Kocha yeyote wa bongo akipewa Taifa star halafu afungwe chini ya 7 basi utetezi wake au point of reference itakuwa kwa Mkwasa.
Tena usiombe imkute kocha kama Julio utasikia akisema mimi nimejitahidi sana yupo kocha alishafungwa 7.
 
7-0 dah raha sanaa

World cup imejaa maajabu sana. Brazil alipigwa 7-1 akiwa nyumbani na kutolewa katika mashindano. Ujerumani na Brazil wote walikuwa ndani ya top 10 katika rankings za FIFA. Algeria na Tanzani tuko mbali mno hivyo kupigwa 7-0 ni haki yetu, tujifunze soka maana hatujajua bado, wakati Algeria ni ya 26 sisi tuko nafasi ya 135 katika rankings za FIFA. Range ni 109 si mchezo!
 

Sisi tuendeleze tu soka la mchangani a.k.a ndondo tutakuwa wazur sana kwny hilo....sio hili soka jingine la kupanda ndege
 
Hashim Rungwe msela njoo gombea na huku

Leo kapigiwa simu na Clouds FM eti akihojiwa kuwa tumesikia unaitaka timu ya taifa uifundishe akasema nimeona kwenye mitandao tu hata sijui hahaaaa nimecheka sana leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…