Mkwasa: Wachezaji wa Yanga wamepoteza uwezo wa kumiliki mpira

Mkwasa: Wachezaji wa Yanga wamepoteza uwezo wa kumiliki mpira

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kocha msaidizi wa Young Africans, Charles Boniface Mkwasa amesema amegundua mambo mawili, baada ya kuanza mazoezi ya kikosi cha klabu hiyo jana jioni.

Kikosi cha Young Africans kilianza mazoezi ya kwanza jana jioni katika uwanja wa shule ya sheria, jirani na kituo cha daladala cha Ubungo Mawasiliano (Simu 2000), jijini Dar es salaam.

Mkwasa amesema jambo la kwanza ambao ameliona kwa wachezaji wake kuwa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu zaidi, wakati shughuli za michezo zilipokua zimesimama kupisha vite dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Amesema wachezaji wengi kati ya walioanza mazoezi hawa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu kuliko kucheza mpira.

“Kwa maana hiyo ni shida ya kwanza ambayo imeonekana kwetu katika mazoezi ya leo (Jana) ambayo tutakwenda kulifanyia kazi,” alisema.

“Tatizo hilo limetokana na wachezaji kuonekana kufanya mazoezi ya nguvu kama ‘beach’ na maeneo mengine.”

“Jambo la pili ambalo nimeliona wachezaji wangu wengi wamepoteza uwezo wa kumiliki mpira kwani mchezaji akiwa na mpira mguuni inakuwa ngumu kuwa salama kwa asilimia kubwa na badala yake hupoteza.”

“Wakati huo huo nimeona wachezaji wakipoteza pasi mara kwa mara na limetokana kupoteza uwezo wa umiliki mpira.”

“Kama benchi la ufundi tumeliona hilo na tunazidi kulifanyia kazi ili kila kitu kwenda sawa,” alisema kocha huyo mzawa.

Leo asubihi kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sheria, jijini Dar es salaam.

Leo asubihi kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa shule ya sheria, jijini Dar es salaam.
 
Wachezaji wako stressed...ugonjwa huu unatisha
 
Mwezi wa 3 tar 18 mpaka mwezi wa tano tar 20+ ni kama miezi miwili. Ligi inapoishaga mwezi wa tano hadi wa nane ni miezi miwili
 
Hawajawahi kuwa na uwezo wa kumiliki mpira kwahiyo wasitutanie
 
Hivi hawa wachezaji si mnasema walienda nyumbani na programm za mwalimu ina maana programm ndio ziliekeza wachezaji wajikite kwenye mazoezi ya physic sana (kwenda mchangani na mabio sana) au wachezaji walikiuka maagizo ya wakufunzi au foot work ya wachezaji wetu n mbovu toka awali kutokana na sajiri zetu mbovu zisizosingatia matakwa ya wa waalimu .....Sijui nna waza nini! !!
 
Watoa taarifa ndiyo huanzisha porojo, wasomaji nao hukurupuka kwenye hizo porojo.

Nenda app rasmi ya klabu ya Yanga msikilize ww mwenyewe Mkwassa anaongea nn?
Alichosema kila klabu lazima ikutane nacho na hata timu za taifa wachezaji wanapokutana kazi kubwa ya mwl huwa hiyo.

UMILIKI WA MPIRA KWA PAMOJA - TEAM WORK ndo ulikuwa ujumbe wa Mkwassa mengine ni kijiwe KINOGE.
 
Timu za Tanzania hakuna timu inaweza kukaa na mpira dakika 3 au kupiga angalau pasi 20 huku timu nyingine ikitafuta
 
Back
Top Bottom