Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Katika yale makampuni yaliyotajwa katika sakata la kuchota EPA wamiliki wao ni nani anafanya biashara na Watanzania? Na hapa nina maana wamiliki wanaojulikana siyo by extension or by proxy.
Mkuu ndio maana naangalia mada hii na kuona kuna uhusiano mkubwa na ile ya Chenge kumsaidia RA kuhamisha mali nje kwa kuwa tunasema tuisusie Vodacom kwa kuhusisha RA na ufisadi na pale anahamisha mali kwa kuhofi uchunguzi wa kifisadi, tunaweza kujadili na kuona kama kweli anajiamini ni safi kwanini akimbize mali? Kuna mtumishi wa BoT ambaye hajaguswa kabisa bado yuko BoT (Peter Noni) na mkewe ni kiongozi CCM lakini ni tajiri kupindukia na sasa tunaambiwa hisa zake kamuuzia Rostam kwa haraharaka na RA naye anazikimbiza... Sasa hatushituki? najua kina Mwanyika, IGP na Hosea hayo hawayaoni, sisi je?