Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,203
- 1,422
Ni vizuri umesema kabisa kwamba mtoa hoja alikuwa mlevi. Kwa bahati mbaya kuna Watanzania wanaopumbazwa na hoja kama hizo. Jambo la msingi ambalo tunabidi kujiuliza Watanzania ni kwamba ni mazuri gani Lissu atatufanyia kuzidi yale Magufuli ameonyesha tayari kuwa anaweza kuifanyia nchi? Ile misemo tu aliyokuwa akiitoa Lissu Bungeni inatosha kuonyesha kwamba mtu huyu, Mungu apishe mbali, kama atachukua nchi, ataiuza.Alikua akitembea huku akipepesuka njia nzima mida ya saa tatu usiku.
Alikua akiongea peke yake muda mwingi,lakini kila aliyekutana nae alimshirikisha furaha yake bila kujali anamshirikisha Nani.
Alipokutana na Mimi,simjui hanijui,sikumpuuza Kama wengine walivyokua wakimpuuza.
Maneneo aliyokua akiyarudiarudia kwa furaha ya kilevi, Ni haya.
"Aaah nitampigia kampeni Dar es salaam yote".
Nikamuuliza Nani?
Akajibu" tayari wameshampitisha nakwambia"
Nikamuuliza Tena wamempitisha Nani?
Akanijibu kwa kunifokea" si Lissu!"
Nikamuuliza,wewe utamchagua Lissu?akajibu,"Tayari nimeisha Anza kumpigia kampeni kwenye vilabu viwili na ninaenda kwingine,nitafanya hivi Dar es salaam yote."
Na huko nilikotoka wamenielewa na wamekubali kumpigia,na huko nakoenda watanikubalia tu kwa sababu wananijua Sana,najulikan a Sana.
Kwa Nini unajulikana?
Akaanza kufunguka.
Kaka yangu amekufa.
Kabla hajafa alikua na nyumba nzuri tu Kimara.
nyumba yake ya Kimara ilibomolewa hakulipwa,
Familia ikakosa mahala pa kuishi.
Akarudi nyumbani mke na watoto akaacha kwangu,Mimi nimepanga chumba kimoja cha kuishi na ninafanya kazi ya kutembeza mitumba.
Kaka alikua mfanyabiashara wa korosho,akanyang'anywa korosho zake huko Mtwara kwa sababu hakua na shamba.
Kaka yangu akachanganyikiwa kabisa,akaugua "stroku" Hadi mauti yakamkuta.
Mke wake yaani Shemeji yangu yeye naye aliachishwa kazi kwa sababu eti walimwambia Hana Cheti,wakati aliajiliwa na serikali hiyihiyo,Sasa Kama Hana cheti walimwajilije? Aliuza mlevi.
Baada ya kuachishwa kazi na mme wake kunyang'anywa korosho na kwa kuwa nyumba Yao ilibomolewa bila kulipwa, na yeye kufukuzwa kazi Shemeji yangu nae akaanza kuumwa "Stroku"na yeye kafa.
Sasa nimebaki Mimi na watoto wao wanne,wawili wameacha kusoma chuo,wawili nawasomesha mimi ila Shule waliokua wanasomeshwa na wazazi wao niliwatoa.
Maisha yangu yamekua magumu,Sasa nimeamua kulewa tu,
Sina kazi,nilisomea ufundi wa mashine ( fitter Turner)
Nimemaliza chuo 2014 nimetafuta kazi miaka mitano sijapata.nimeamua kutembeza mitumba na kulewa tu.nina mke na watoto wawili wangu na wa Kaka wanne,jumla Nina watoto sita.
Nitamchagua Lissu na nitampigia kampeni vilabu vyote Dar es salaam.
Vilabu vyote nilivyopitia kabla hajapitishwa na baada ya kupitishwa wanamkubali Lissu.
Nilimtia moyo nikampa Sha 10,000=,nikaondoka yangu
Hiyo ndio hali halisi huko mitaani.
Ona mfano aliokuwa akiupigia kelele Bungeni kuhusu mchanga wa makenikia. Alikuwa akiwatetea Acacia kwa nguvu zote eti tu kwa kuwa kulikuwa na mkataba. Magufuli akaingilia kiti kuupitia upya mkataba, na mambo yakaboreshwa. Sasa hatuibiwi kama ilivyokuwa zamani na kiwango tunacholipwa sasa na makampuni ya madini kimeongezeka. Hilo ni bao moja kwa Magufuli dhidi ya Lissu ambaye kwake tungeendelea kuliwa tu.
Jingine alilolisemea Lissu Bungeni ni kuhusu Ziwa Nyasa kuwa lote ni la Malawi kufuatana na makubaliano na Mkoloni wa Kiingereza wa sijui mwaka gani. Lissu anasimamia kidete mikataba inayonufaisha nchi za nje at the expence of Tanzania. Ni dhahiri nchi itauzwa kama Lissu akiingia madarakani. Jambo la maana ni kuupitia upya mkataba uliokubaliwa kwa kuwa ni wa kipuuzi kusema kwamba ziwa lote mpaka ufukoni liwe la nchi nyingine sisi tusiwe hata na ule ufuko wa watu wetu kwenda kuogelea. Lissu hana maslahi ya Tanzania. Anaangalia mikataba iliyopo badala ya kusema tuipitie upya kuiboresha. Hilo ni bao la pili la Magufuli dhidi ya Lissu.
Vilevile Lissu alizungumzia kuhusu maji ya ziwa Victoria kwamba tusiyaguse kwa kuwa yatapunguza maji yanayokwenda Misri kufuatana na mkataba kati ya Msri na mkoloni wa Kiingerea wakati akitutawala. Sasa sisi raia wetu wabaki na shida ya maji eti tu kwa kuwa Misri wataathirika. Magufuli amelikabiri hilo na sasa maji yanakaribia kufika Shinyanga, Tabora na Dodoma. Hizi ndizo juhudi za kutetea maslahi ya nchi yako. Mikataba mibovu inapitiwa upya kwa maslahi ya nchi. Lissu yeye anajikita kwenye mikataba iliyopo badala ya kutumia ujuzi wake wa sheria kurekebisha mambo. Hili ni bao la tatu la Magufuli.
Suala la Lowassa nalo ni mfano mwingine. Wakati Lowassa akiwa bado CCM, Lissu alikuwa akisema kwa nguvu sana kwamba Lowassa ni fisadi kubwa lisilostahili kabisa uongozi wa nchi. CCM walikubaliana na hoja hizo wakamuengua Lowassa. Lowassa alipojiunga na upinzani mara habari za ufisadi zikaisha. Lowassa akawa msafi. Ni dhahiri kwamba kwa Lissu na chama chake hakuna suala la kuangalia maslahi ya nchi bali watimize tu dhamira ya kuridhisha uchu wao wa madaraka. Bao la nne la Magufuli.
Turudi kwenye hoja za mlevi uliyemkariri. Hoja ya kubomolewa nyumba kupisha mipango ya maendeleo ya kitaifa hufanyika po pote ulimwenguni. Inawezekana kuna urasmi wa kulipa fidia. Hilo ni jambo la kiutawal ambalo huwezi kumlalamikia mkuu wa nchi. Ndiyo maana akigundundua watumishi wanaoshindwa kuendena na kasi yake wanatumbuliwa. Wasioelewa mambo wanalalamika. Kuhusu korosho, kulikuwa na matapeli yananunua korosho kwa watu na kuzilangua serikalini kwa mara kadhaa zile hela alizopewa mkulima. Serikali ikakata hiyo kwa kuamua kumlipa mkulima moja kwa moja kwa bei ya juu kuliko aliyokuwa akipewa na matapeli wa kati. Hapa pia kulikuwa na matatizo ya urasmu na wakulima wengine wamecheleweshwa kulipwa. Lakini kwa kuangalia sera yenyewe, ni kweli mtu unaweza kuikosoa? Kuhusu vyeti feki. maelfu ya watu walibainika kwamba hawana vyeti kama walivyodai wakati wa kuajiriwa. Kiutendaji, kuna watu waliosumbuliwa hasa waliosoma zamani sana. Lakini hakuna mtu aliyekuwa na cheti, hata kama ni zamani sana, aliyefukuzwa kwa kuwa tu amekipoteza cheti chake. Utaratibu uliwekwa wa kuthibitisha kupata kwako kwa cheti ambacho umekipoteza. Sasa kuna ubaha gani kufukuzwa mfanyakazi asiye na cheti kinachostahili? Mhusika atalalamika lakini kitendo husika inabidi kupongezwa. Hii pia inahusu wafanyakazi hewa. Watu walikuwa wanadai kuna wafanyakazi kadhaa ambapo si kweli. Mwisho wa mwezi anakwapua mishahara ya 'wafanyakazi' hao. Magufuli akaingilia kitu na kuwangámua hao na kulitatua tatizo hilo. j
Jee, Watanzani tulalamike kwamba mianya ya kujipatia mali imezibwa? Huu ni upuuzi usio na maslahi kwa nchi. Kuhusu kumaliza chuo cha ufundi nakukosa ajiri kwa miaka mitano huu ni ujinga wa mhusika. Robo tatu ya mafundi mchundo wanabidi kuweza kujiajiri wenyewe, Ni kweli wanahitaji mtaji lakini hili ni jambo la kujitatulia mwenyewe hata kwa akuungana na ndugu zako au wenzako uliokuwa ukisoma nao. Hiyo ni kabla ya kurudi serikalini kama hayo yameshindikan.Tunajumlisha hoja zote za mlevi mkaririwa kuwa ni goli la tano la Magufuli.
Matokeo ya pambano kati ya Magufuli na Lissu, kwa kuangalia mifano michache tu niliyoiainisha hapo juu, ni 5-0 in favour of Magufuli. Watu waelimishwe ukweli huu kuepuka kupambazwa na hoja sisizokuwa na tija kama alizokuwa akizotoa mlevu. Bahati mbaya hata mtoa mada ulichochea moto kwa kutoa Sh. 10,000 ambazo zitampa hisia kwamba anatenda mazuri.