Mlikutana wapi wewe na mke/mume au mpenzi wako?

Mlikutana wapi wewe na mke/mume au mpenzi wako?

She is my neighbor "a little far from home"
Nilimfundisha hesabu alipo kua form 2 hapo mimi nimemaliza form 4.
Kamaliza form 6 tukaanza ku date rasmi till now.

Mama Zetu ni marafiki sana toka kitambo
Nakumbuka siku moja Mama aliwahi nitamkia "ingekua ni zile Zama zetu za kuchaguliwa mke ningependa uje uoe kwa flani 'kwao uyo binti', ila mwanangu najua wakati bado ila Muangalie binti wa kwa flani napendezwa nae hata ukianza nae urafiki sio mbaya miaka minne mi tano sio mbali " .
Kimoyoni nikajisemea mother ungejua.
Ila sasa nahis Mama anafaham japo hana uwakika.

Kati ya wanaume wenye binti mrembo basi nami ni mmoja wapo, she is beautiful very beautiful she is smart too.
Mungu mlinde mrembo wangu.
Leta mrejesho ndugu yangu. Muda umeshaenda sana
 
Siku moja nilienda lodge na demu wangu,tulipofika mapokezi nikamkuta jamaa mmoja yupo pia na demu wake,hatujuani,
Baada ya kupewa vyumba nikatoka kwenda kununua chakula nje(kitimoto),yule jamaa aliyekuwa na demu nadhani aliogopa kwenda maeneo yale yanayouzwa kitimoto akamtuma yule mwanamke wake,tukakutana tunaagiza nyama pale tukasalimiana tena na utani wa hapa na pale kwamba kwa msosi huo leo lazima nyasi zing'oke,akacheeka cheka pale tukapeana namba za simu,tukaanza kuwasiliana taratibu mapenzi yakaanza,hadi leo hii ndio naishi nae ndani kama mume na mke
Kwl maisha hayana formula
 
Walikuja wageni kutoka nje ya nchi kanisani kwetu tukatambulishwa kanisani ilikuwa jpili moja hivi wanawake kama saba hivi ,tukaambiwa watakuwa Tanzania kwa mwezi mmoja sikuwa na hili wala lile hata sikuwaza ukaribu nao maana sikuwa hata na mpango wa kuoa na church kulikuwa na pisi za hatari,jioni pastor akaniligia simu kuwa nimsadie kuwatembeza kwa kuwa English ilikuwa sio ishu kwangu so nikafanya.

Jtatu nimazuga job huyo kufanya kazi ya bwana Hahahaha mara pa nakuta wamevaa kitown sio kama jana church mmoja akasema aendeshe yeye na mm nikae kushoto kumuelekeza alikuwa binti pisi flani hivi mweusi ambao ndio ugonjwa wangu tukazoeana huwezi amini nilikuta hajaguswa kabla hajaondoka nikaweka wazi kwa wazazi na pastor alifurahi sana ingawa hakujua nimesha haribu,alivyokwenda kwao wakazingua kumbe niliacha mbegu ikabidi arudi tz kwa ndoa kwa sasa tuna watoto wawili na miaka 11ya ndoa ,ni wife material sio ndugu kila mtu anasema wewe USSR kweli ulioa ndoa hupanga Mungu kabisa


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Mke wangu tulikutana kanisani kwa mara ya kwanza sikuwa namfahamu kabla, sasa tuna watoto.wawili.
 
Hii haiwahusu 👉team Chaputa 👉haiwahusu wazee wa kwa wahaya 🤣

Binafsi wangu nilikutana nae ule wakati wa covid 19 mtakumbuka kuna kaupepo kalipita hivi akiugua tu mwenzako kesho yake unafata wewe hapa siongeleii corona kuna homa fulani hivi ilipita nakumbuka pale kibaruani tuliugua wote 16.(mtakumbuka mafua yalikuwa yanakuwa makali viungo vya mwili vyote vina Pata fatigue, appetite inashuka na joto la mwili linakuwa juu)

Mimi ndo nilikua mtu WA mwisho kabsa kuugua nikapewa likizo

Nikiwa hospitali sasa yule nurse wa zamu Kila akipita Akiniona anasisitiza sana Kuzingatia mlo.
(nikawaza Huyu nurse kanipenda au ndio ethics za Kazi tu) kumbe ilikuwa kweli mwanamama alivutiwa namimi /tulikuwa tunachemistry fulani hivi

Nikachukua siku Tatu tukazoeana mimi ni extrovert easy to aproach stranger by nature
(mtoto si kinyonge kafungasha HITACHI sio mchezo size ya kati) mimi nikanogewa sana na uchangamfu hadi discharge inafika nikataka kuikataa 🤣

Nikachukua Namba yake bahati nzuri Ile mwezi nne 2020 akapata likizo basi mambo mengine yalibaki historia

Wewe wa kwako ulikutana nae wapi!??
 
Kuna thread kama hii miaka miwili au mmoja ulio pita tulisha same tulikutana nao wapi pitia kulee ujue
 
Mimi wangu alikuja kufanya field ofisini kwetu,,akiwa anasoma certificate ,,,mpka saizi ni mama wa wanangu watatu
 
Back
Top Bottom