Mlikutana wapi wewe na mke/mume au mpenzi wako?

Leta mrejesho ndugu yangu. Muda umeshaenda sana
 
Kwl maisha hayana formula
 
Mke wangu tulikutana kanisani kwa mara ya kwanza sikuwa namfahamu kabla, sasa tuna watoto.wawili.
 
Hii haiwahusu 👉team Chaputa 👉haiwahusu wazee wa kwa wahaya 🤣

Binafsi wangu nilikutana nae ule wakati wa covid 19 mtakumbuka kuna kaupepo kalipita hivi akiugua tu mwenzako kesho yake unafata wewe hapa siongeleii corona kuna homa fulani hivi ilipita nakumbuka pale kibaruani tuliugua wote 16.(mtakumbuka mafua yalikuwa yanakuwa makali viungo vya mwili vyote vina Pata fatigue, appetite inashuka na joto la mwili linakuwa juu)

Mimi ndo nilikua mtu WA mwisho kabsa kuugua nikapewa likizo

Nikiwa hospitali sasa yule nurse wa zamu Kila akipita Akiniona anasisitiza sana Kuzingatia mlo.
(nikawaza Huyu nurse kanipenda au ndio ethics za Kazi tu) kumbe ilikuwa kweli mwanamama alivutiwa namimi /tulikuwa tunachemistry fulani hivi

Nikachukua siku Tatu tukazoeana mimi ni extrovert easy to aproach stranger by nature
(mtoto si kinyonge kafungasha HITACHI sio mchezo size ya kati) mimi nikanogewa sana na uchangamfu hadi discharge inafika nikataka kuikataa 🤣

Nikachukua Namba yake bahati nzuri Ile mwezi nne 2020 akapata likizo basi mambo mengine yalibaki historia

Wewe wa kwako ulikutana nae wapi!??
 
Kuna thread kama hii miaka miwili au mmoja ulio pita tulisha same tulikutana nao wapi pitia kulee ujue
 
Mimi wangu alikuja kufanya field ofisini kwetu,,akiwa anasoma certificate ,,,mpka saizi ni mama wa wanangu watatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…