Media ya Tanzania ina changamoto ya specialization, ukisema waandishi wa habari inamaanisha ni print media hata sheria ya magazeti ya
1976 ilihusu print media
only, sheria mpya ya habari ni ya print media only! idara ya Habari Maelezo, ina deal na print media only, halafu waandishi wa electronic wanaitwa watangazaji, wana sheria yao, sheria yautangazaji iko chini ya TCRA, siku zijazo tutaboresha TEF,mwenyekiti akiwa print, makamo mwenyekiti awe from electronic media.
P
Kwa uelewa wangu, Mwandishi wa Habari ni Mwandishi wa Habari; hakuna kitu kama utangazaji vs uandishi wa habari wa magazeti etc, na ndiyo maana hakuna shahada ya Utangazaji per se hapa Tanzania. Pia, sikubaliani kwamba Sheria ya Huduma za Habari inawahusu print media journalists pekee, labda kama sikukuelewa bro.
Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inagusa vyombo vyote vya habari na wataalamu wake bila kujali wanafanya kazi katika vipengele vitatu vikuu, yaani vyombo vya habari vya magazeti, vya elektroniki, au vinginevyo.
Sheria ulizozitaja, kama vile EPOCA ya mwaka 2020 na Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, zinawahusu waandishi wa habari wote kutokana na uwepo wa muunganiko wa vyombo vya habari, ambao unawalazimu kuwa na uwepo katika majukwaa yote.
Sasa, kwa nini TEF, kwa miaka mingi, imekuwa chombo kinachotawaliwa zaidi na wahariri wa vyombo vya uchapishaji ambao wamejinyakulia uongozi wa chombo hiki kinachosemekana kuwasimamia/kuwawakilisha waandishi wote wa habari Tanzania? Mbona majority ya Editors wa Electronic media nchini hawamo humo TEF (Zaidi ya editors wa vituo vya redio 230 plus vituo vya TV 50 naa-hivi vyombo almost 300 editors wake ni members wa TEF!? na lini walikuwa viongozi wa juu wa TEF)...Halafu TEF mbona viongozi wake huwa ni walewale tu!
Hatuoni wahariri kutoka redio za mikoani au hata za kitaifa wakishika nafasi za juu katika TEF.
Kwa nini basi msikipachike jina TEF kuwa chama cha wahariri wa vyombo vya habari vya uchapishaji pekee!?.... ili wahariri wa vyombo vya utangazaji na mtandaoni nao waweze kuanzisha vyama vyao vya wahariri wao?
Binafsi kama mdau wa habari na mfuatiliaji wa tasnia yenu pendwa bado sijaridhika na mfumo wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania ambavyo havionekani kuwakilisha maslahi ya waandishi wote. Vyama ni vingi hakuna mwamvuli wa chama kimoja chenye nguvu cha journalists, why!?
Mnatakiwa kuwa na vyama ambavyo vinajumuisha kila mmoja. Jifunzeni TLS nk
Kwa nini tusiamini kwamba baadhi ya vyama hivi ni kichaka cha baadhi ya waandishi wa zamani kuchuma maslahi binafsi na hamtaki kuongeza wanachama zaidi?
Waandishi wanadhibitiwa na mamlaka mbili za udhibiti ambazo ni Idara ya Habari Maelezo na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Ikiwa kweli TEF ina nia ya kuleta mabadiliko katika uandishi wa habari Tanzania, basi inapaswa kuwa chombo kinachowaleta pamoja wahariri wote, iwe ni wa magazeti, redio, televisheni, au mitandaoni kwa kupitia hizo Regulatory bodies mbili zinazowasimamia waandishi wote Tanzania...Maelezo akisimamia vyombo vya machapisho na TCRA akisimamia vyombo vya habari vya mtandaoni na elektroniki ongeeni nao hawa muone mnawaunganisha vipi waandishi wa Tanzania....You guys are so divided, mkipona hapo waandishi wa habari mtajiongezea tija sana...hivi sasa kila Mwandishi kivyake. N'yadikwa