Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Katika harakati za mtu mweusi, nikaenda Ifakara, Morogoro.
Sasa kufika hapo mchongo ukanitaka asubuhi niende Mlimba Morogoro pale Kihansi Hydropower. Nauliza wenyeji wanasema kwa “bus” ni kama masaa 2 hivi. Nikaona sio mbaya.
Nikaamka saa 3 kujiandaa kufika saa 4 nipo stendi. Nikapanda Noah, kutoka hapo saa 5 hivi nafika Mlimba saa 10 jioni.
Njia ni vumbi mwanzo mwisho kuanzia Ifakara kilometa zote 150+, namaliza mishe kurudi naambiwa eti hamna gari hadi kesho.
Nikasema hamna siwezi kulala huku. Nikapanda Bajaji hadi Chita. Kufika pale hamna usafiri tena, nikasubiri ikaja bajaji nyingine inaishia Mngeta, kisha kama zali nikapata Noah inaishia Kisegese.
Hapo ishafika saa 3 usiku, kuna boda ndio akakubali kunipeleka Ifakara kwa 25,000/= aisee.
Wenye magari kule wana ringa sana.