Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Katika harakati za mtu mweusi, nikaenda Ifakara, Morogoro.

Sasa kufika hapo mchongo ukanitaka asubuhi niende Mlimba Morogoro pale Kihansi Hydropower. Nauliza wenyeji wanasema kwa “bus” ni kama masaa 2 hivi. Nikaona sio mbaya.
View attachment 3109716
Nikaamka saa 3 kujiandaa kufika saa 4 nipo stendi. Nikapanda Noah, kutoka hapo saa 5 hivi nafika Mlimba saa 10 jioni.

Njia ni vumbi mwanzo mwisho kuanzia Ifakara kilometa zote 150+, namaliza mishe kurudi naambiwa eti hamna gari hadi kesho.

Nikasema hamna siwezi kulala huku. Nikapanda Bajaji hadi Chita. Kufika pale hamna usafiri tena, nikasubiri ikaja bajaji nyingine inaishia Mngeta, kisha kama zali nikapata Noah inaishia Kisegese.

Hapo ishafika saa 3 usiku, kuna boda ndio akakubali kunipeleka Ifakara kwa 25,000/= aisee.

Wenye magari kule wana ringa sana.
Siku likitokea la kutokea huko kwa wakwe zangu siendi.
 
Bora umekuja kipindi hichi ukija wakati wa masika utahadithia ukitoka stand mwisho wa raha ni ng'ambo lumemo baada ya hapo ni tabu tupu na ukifika kisegese nd mwisho wa gari maana hapo kunakuwa na dimbwi hatari mtakuta gari nyingne ng'amb ya kuwachukua na sio mlimba tu hata malinyi n hvyo hvyo masika hapafai kule ni bonde kweli kweli
 
Wilaya ya Sikonge hiyo mzee
Ahahahaha napajua vizuri.
Kuna basi moja la saa 7 kama sikosei inaitwa SARDINI / SADINI hilo likienda leo linarud kesho alfajiri..

Ndani kuna chawa, viroboto kama wote, na siti zake ni 2 by 3 mlango mmoja.. ndani kunapakiwa kila aina ya mzigo.

Sasa usiombe ukae siti za nyuma nyuma alafu unataka kushuka😂 utachagua ushukie dirishani au utambae juu ya siti kama buibui.
 
Back
Top Bottom