Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Mad Max next time ukija ni pm mzee mimi ni afisa usafirishaji almaarufu kama boda boda hapa ifoza mpk idete mzee tubadilishane mawazo.
Lakini siku ukifika tena ifoza ulizia califonia ni wapi hata ukachungulie🤣🤣
Ahahahaa!! We jamaa Califonia akachungulie nini? Ugeni wangu uliochanganyika na uenyeji kuna siku nimekaa Califonia napiga maji ya Devi. Kama unavyojua kibofu kikaanza fujo.

Nimeenda washroom nilichokutana nacho ni balaa 🤣 acha niishie hapa.
 
Hapa nilishuka ili nimpishe abiria mwingine ashuke, wauza ndizi na karanga wapo serious walijaa mlangoni hadi kushuka mtiti.
PXL_20240927_100810171.MP.jpeg
 
Nilikuwa hapo mwezi wa sita 2024 unataka niweke risiti za mafuta nilizoweka kwenye vituo vya mafuta huko Ifakara??

Point yangu ni barabara ya kwenda Mlimba, barabara ya kwenda Malinyi halikadhalika Magenge.
Huko ndio kwetu unajua maana ya jina langu?? Asili yake ndio huko.
Ukisema mlimba au mahenge hapo sawa ila sio ifoza to moro twn
 
Ahahahaa!! We jamaa Califonia akachungulie nini? Ugeni wangu uliochanganyika na uenyeji kuna siku nimekaa Califonia napiga maji ya Devi. Kama unavyojua kibofu kikaanza fujo.

Nimeenda washroom nilichokutana nacho ni balaa 🤣 acha niishie hapa.
Na ndio maana nkamwambie achungulie tu na asiwe mtendaji mkuu🤣🤣🤣
 
Ndio maana watu wa Morogoro bado wanalia sana na barabara,

Barabara zote zipo Morogoro mjini tu ndanindani hamna kitu

Halafu mkoa nao mi mkubwa sana, masaa manne mtu unasafiri ndani ya mkoa mmoja tu. Huu mkoa unatakiwa ugawanywe, watu wa ifakara na Mlimba wako mbali mno na Morogoro mjini, wako karibu na Njombe kuliko Morogoro mjini
Ulanga iko karibu na Namtumbo mkoa wa Ruvuma, kuliko Morogoro enyewe.
 
Kilamsa hazifiki mlimba
nlikua na mwanamke wangu mmoja miaka hio inabidi kila mwez aumwe aje St francis nimpachike mbolibo
 
Katika harakati za mtu mweusi, nikaenda Ifakara, Morogoro.

Sasa kufika hapo mchongo ukanitaka asubuhi niende Mlimba Morogoro pale Kihansi Hydropower. Nauliza wenyeji wanasema kwa “bus” ni kama masaa 2 hivi. Nikaona sio mbaya.
View attachment 3109716
Nikaamka saa 3 kujiandaa kufika saa 4 nipo stendi. Nikapanda Noah, kutoka hapo saa 5 hivi nafika Mlimba saa 10 jioni.

Njia ni vumbi mwanzo mwisho kuanzia Ifakara kilometa zote 150+, namaliza mishe kurudi naambiwa eti hamna gari hadi kesho.

Nikasema hamna siwezi kulala huku. Nikapanda Bajaji hadi Chita. Kufika pale hamna usafiri tena, nikasubiri ikaja bajaji nyingine inaishia Mngeta, kisha kama zali nikapata Noah inaishia Kisegese.

Hapo ishafika saa 3 usiku, kuna boda ndio akakubali kunipeleka Ifakara kwa 25,000/= aisee.

Wenye magari kule wana ringa sana.
Dah! Siku nyingine ukishuka hapo Kisegese, mwambie boda akulete Mofu ili uje ule samaki wa Mto Kilombero. Msimu huu samaki aina Ndipi, njuju na ngogo; ni wengi sana. Ni mwendo tu wa kula na ubwabwa.

Halafu ushukuru siku hizi kuna bajaj, kuna bodaboda, kuna Noah, kuna TATA, nk. Miaka ya 90, usafiri pekee wa huko ulikuwa ni treni ya Tazara, baiskeli, na malori ya mizigo yanayoenda kuchukua mpunga na mchele!

Abiria tulikuwa tunaning'inia juu ya machuma. Gari ikiyumba kidogo tu, unatamani kuirudisha kwa mikono!! Na kumbuka sasa hivi ni kiangazi! Masika ikifika ndiyo balaa zaidi.
 
Morogoro yote jau mkuu. Kutoka wilaya Moja kwenda nyingine kunakuwaga na gari Moja ukiikosa mpaka kesho Tena😂
Si kweli. Kutoka Moro to Ifakara magari yapo mpk saa Moja jioni. Au unapanda mabasi yanayotoka Dar, Arusha yanapita Moro mjini saa 1 mpk 2 hivi. Kwa siku hiyo route ina magari zaid ya 10-20 yaani ile to and fro. Barabara kwa sasa Mzee Magu kajenga rami kali sana na wakandalasi walikua hawa komesha ya wavaa makobazi, Waisrael. So, c wilaya zote jau. Hiyo njia ya Mlimba bado bado, ni ka-senta tu. Nadhani mkandalasi ndo kaingia saiti
 
Ndio maana watu wa Morogoro bado wanalia sana na barabara,

Barabara zote zipo Morogoro mjini tu ndanindani hamna kitu

Halafu mkoa nao mi mkubwa sana, masaa manne mtu unasafiri ndani ya mkoa mmoja tu. Huu mkoa unatakiwa ugawanywe, watu wa ifakara na Mlimba wako mbali mno na Morogoro mjini, wako karibu na Njombe kuliko Morogoro mjini
Masaa manne hayo yanasababishwa na ubovu wa barabara. Km 150 ni mwendo wa masaa mawil tu
 
Ahahahaa!! We jamaa Califonia akachungulie nini? Ugeni wangu uliochanganyika na uenyeji kuna siku nimekaa Califonia napiga maji ya Devi. Kama unavyojua kibofu kikaanza fujo.

Nimeenda washroom nilichokutana nacho ni balaa 🤣 acha niishie hapa.
Dah! Hiyo Califonia ndiyo Kahumba ya Ifakara hiyo!! Halafu zamani hata haikuwepo. Binafsi huwa nikija Ifakara, mara nyingi napenda kuweka kambi yale maeneo ya Posta. Kuna kuku wengi sana wa kuchoma nyakati za usiku.
 
Sehemu kibao tuu kwa Tz hii zipo hivyo Kaka, jaribu kutembeza zaidi utajionea, juzi kati nilikosa gari pale Tabora mjini usiku hata ya kunifikisha Dodoma,
Tena watu wa huko washazoea
 
Back
Top Bottom