Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Mlimba Morogoro jau sana, ikifika saa 9 jioni haujageuka Ifakara ndio nitolee hadi kesho hiyo!

Nilikuwa huko juzi kati.
Niliona ile lami ya Ruaha kwenda Ifakara ipo poa.
Shida ipo Ifakara kwenda Mlimba.
Ifakara kwenda Malinyi
Ifakara kwenda Mahenge.
Mashimo na vumbi la kufa mtu.
Me wananiambia eti sahivi wamechonga barabara msimu wa mvua usipime.
 
Katika harakati za mtu mweusi, nikaenda Ifakara, Morogoro.

Sasa kufika hapo mchongo ukanitaka asubuhi niende Mlimba Morogoro pale Kihansi Hydropower. Nauliza wenyeji wanasema kwa “bus” ni kama masaa 2 hivi. Nikaona sio mbaya.
View attachment 3109716
Nikaamka saa 3 kujiandaa kufika saa 4 nipo stendi. Nikapanda Noah, kutoka hapo saa 5 hivi nafika Mlimba saa 10 jioni.

Njia ni vumbi mwanzo mwisho kuanzia Ifakara kilometa zote 150+, namaliza mishe kurudi naambiwa eti hamna gari hadi kesho.

Nikasema hamna siwezi kulala huku. Nikapanda Bajaji hadi Chita. Kufika pale hamna usafiri tena, nikasubiri ikaja bajaji nyingine inaishia Mngeta, kisha kama zali nikapata Noah inaishia Kisegese.

Hapo ishafika saa 3 usiku, kuna boda ndio akakubali kunipeleka Ifakara kwa 25,000/= aisee.

Wenye magari kule wana ringa sana.

Ukiona hivyo hilo ni eneo lenye mzunguko mdogo wa pesa.Hakuna biashara huko.au biashara ni ya msimu
 
Ndio maana watu wa Morogoro bado wanalia sana na barabara,

Barabara zote zipo Morogoro mjini tu ndanindani hamna kitu

Halafu mkoa nao mi mkubwa sana, masaa manne mtu unasafiri ndani ya mkoa mmoja tu. Huu mkoa unatakiwa ugawanywe, watu wa ifakara na Mlimba wako mbali mno na Morogoro mjini, wako karibu na Njombe kuliko Morogoro mjini
 
100k *300 days unapata milioni 30 sawa sawa na noah ngapi??
Hizi ni hesabu za online.....kwenye real world ya Mlimba hakuna kitu hicho.

Kinachofanya routes na mizinguko kuwa chache kama mleta mada anavyodai ni Uhaba wa Abiria.

Mtu mwenye bus lenye seat 20 hawezi kukubali kuendesha 150Km na abiria 10.

Ni hasara.

So eneo hilo hata ukipeleka Noah kwa siku huwezi kuzidi 50k ya faida. Gharama ya mafuta pia ni kubwa
 
Ndio maana watu wa Morogoro bado wanalia sana na barabara,

Barabara zote zipo Morogoro mjini tu ndanindani hamna kitu

Halafu mkoa nao mi mkubwa sana, masaa manne mtu unasafiri ndani ya mkoa mmoja tu. Huu mkoa unatakiwa ugawanywe, watu wa ifakara na Mlimba wako mbali mno na Morogoro mjini, wako karibu na Njombe kuliko Morogoro mjini
Lack of government support.....ukubwa sio issue.
 
Back
Top Bottom