Kwa kweli kwa hali ya maisha ya ubepari kama huna Mungu ndani yako au mental na psychological calmness unaweza kufanya vitu ambavyo watu watakuona hauna akili kumbe mwisho wako wa kufikiri ndipo ulipoishia.
Unaweza in au kusikia watu mliokuwa nao shuleni au kambini washatoboa. Au unaenda maeneo kama Mlimani ukiona jinsi vijana au watu wanavyospend unaweza kujisonya sana.
Ktk nchi za Ulaya na US suicide na kuuana cases ni nyingi koz ubepari umekomaa. Sitamani tufike huko lakini kwa hali ilivyo ni kama vile safari imekaribia.
Zamani mtu akijinyonga inakuwa taabu kila mtaa utajua au kusimulia kwa wikii na mawiki ila Sasa imekuwa kawaida na sababu ni nyingi kuanzia maisha, mapenzi, kazi, kukataliwa, Kukosa tumaini, Kukosa Mali, kudharauriwa, masomo, kubakwa, kushindwa kuhimili tatizo nk.
Hivi karibu kuna kijana wa hapa Stend ya Magufuri wale wanaoshika chati za magari naye kajinyonga kwa sababu ya mapenzi. Mke wake alikuwa anamsumbua jamaa sana.