Mlioajiriwa mnakabiliana vipi na changamoto ya kurudia jambo lilelile (Monotony)

Kwani ukijiajiri kuuza nguo kuna siku utaenda dukani kwako ukute nguo zimebadilika na kuwa bajaji ?
 
Na wewe unajisikiaje kila siku jioni au usiku kuoga? yaani unafanya jambo lilelile kuoga kila siku.
 
Kiuhalisia hili jambo linakera,, tena kumhudumia mtu yule yule kwa shida ile ile isiyoisha ndo inakera zaidi....
Japo siyo vizuri ila huwa ikitokea ukapata mtu mwenye shida ya ziada itakayokufanya ujiongeze zaidi huwa kuna utofauti...
Unakuta mjamzito kila wiki yuko kakuletea sura yake eti anatapika sana, kisa ana hela kalipia na vipimo anataka apimwe ultrasound akati ndo hata wiki hajamaliza umempima....
 
Kula ni suala lile lile mpaka unakufa... Ishu inakuwa kwenye ufahamu wako sio kwenye hilo unalofanya. Unafanya jambo hilo hilo kwenye siku tofauti, majira tofauti, mwaka tofauti, umri tofauti na mengine mengi.
Unaweza kuamua kufanya kwa utofauti kila unapofanya.
 
Hata mimi zamani niliwahi kuwaza jambo hilo, yaani mwalimu anafundisha leo what is geography, mwakani tena anaanza palepale what is geography, mwaka mwingine anaanza tena what is geography hachoki?
Ila baadae mawazo hayo yaliisha pale ambapo na mimi kwenye kazi kazi zangu mfumo ni ule ule. Inafika hatua hata kulala nachoka, yaani kila usiku lazima nilale Kisha asubuhi niamke,...kuna siku niliamka saa4 nikanywa chai nikalala nikaamka saa8 nikala nikalala, baada ya muda kidogo eti siku imeisha. Nikawaza tumekuja kufanya nini duniani mbona kama muda ni mdogo sana hautoshi? Yaani kulala kidogo tu siku imeisha?

Kwa hiyo mkuu, hakuna jambo jipya kwenye kazi yoyote, labda ubadilishe kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…