Mliochezea Mashine Pale Temeke Hospitali Nina Ujumbe wenu

Mliochezea Mashine Pale Temeke Hospitali Nina Ujumbe wenu

Malisa ndo nan?
Mchaga flani hivi.Unataka kujua Malissa au alichopost.Alisema X-ray za Temeke hospitali zilikuwa hazifanyi kazi(ukweli) na waziri wa afya akaja kusema kuna vitu watumishi wa hiyo hospitali walifanya ndivyo sivyo.

Anyway Malissa yupo humu JF unaweza kumtafuta kama utahitaji kuhusu yeye
 
Huyu mwamba mwenye dhamana ya Wizara yenu hatanii na Wala hataniwi, ni Bora mkafikiria kwenda kuishi nje ya nchi kama bado mnapenda kuendelea kupumua katika hii Dunia kabla hamjaaimbiwa parapanda.

Natumaini mmenielewa.
Hivi CCM ndo mmeamua kuwa mazuzu kabisa. Kila anayekosea adhabu yake ni kifo? Mnathinitisha Mchengerwa anahusika kwenye Mauaji nchini?
 
Weka link hapa
Habari inahusu X-ray kuwa hazifanyi kazi hospitali ya TMK.Habari alianza kuripoti Malissa(ambaye ni member pia JF) anadai alidokezwa na mdau kwamba hospitali ya Temeke X-ray hazifanyi kazi(ilianza kama tetesi badae ikawa ni kweli baada ya waziri kufika pale)

Waziri wa afya alidai kuna watumishi wanafanya hujuma kwa kuzima hizo X-ray na kusisitiza kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika.

Anyway kati ya jeshi la polisi na JW nani bora? Vipi yule mpasua tofali aliyechezea Mwanza kwa askari polisi anaendelea vipi kiongozi?
 
Wauaji huwa hawawezi kuficha kiu yao ya damu kama huyu mtoa mada

Ila wale waliochezea Mashine siyo wauaji??? Wewe subiri bango la Boss wao likiwa na kichwa cha habari TANZIA
 
Kama wanapenda sana kuchezea mashine, basi tutawapa mashine wachezee vizuri, hakuna nyumbu atakaechekewa katika suala zima la kuhujumu Taifa .

Wewe subiri bango la Mganga Mkuu wa Temeke likiwa na kichwa cha habari TANZIA
 
Yaani utasema hakuna sheria za kumshughulikia Mfanyakazi anayevunja taratibu za kazi..UDIKTETA uchwara tu

Kwenye Afya ya Mwananchi masikini huu upuuzi haikubaliki. Tusubiri bango la TANZIA kutoka TEMEKE.
 
Ila Tanzania Kuna baadhi ya wahudumu wa afya ni wauaji sana,

Na Mwamba anawatafuta wa namna hiyo ili awashughulikie vizuri. Watendaji wa Afya wasipobadilika mabango ya TANZIA yatakuwa mengi Sana Awamu hii.
 
Hivi CCM ndo mmeamua kuwa mazuzu kabisa. Kila anayekosea adhabu yake ni kifo? Mnathinitisha Mchengerwa anahusika kwenye Mauaji nchini?

Mimi sijui ila ninachojua afya ya Mwananchi masikini ni suala la muhimu Sana, wasipobadilika tutaona mabango mengi Sana ya TANZIA
 
Back
Top Bottom