Mliofanikisha kujenga nyumba, Tupeane uzoefu hapa

Mliofanikisha kujenga nyumba, Tupeane uzoefu hapa

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
wakuu natumai hamjambo!

Kama jinsi ilivyoada, kila mtu anatamani kuwa na mahali pake binafsi pa kuishi yeye na family yake, ingawa kwa upande mmoja kwa baadhi ya watu hili suala si changamoto kwao kwa sababu ya uzoefu ama mfuko umekaa njema kiuchumi, lakini kwa upande mwingine kwa watu aina yangu kumekua na changamoto sana, ukilinganisha na hali ya uchumi wa kati tulionao!

Sasa wakuu, kwa wale mliofanikisha kujenga ( Hasa kipindi cha Jiwe na Mama), mmefanikiwaje ndugu zetu?
Naomba kwa faida ya tulio wengi hasa mimi, tupeane skills na experience, ili sisi nasi tulio na makazi ya kulipia kila mwezi, tulipie kodi za majengo kihalali!
 
image-2021-08-29-15:20:41-940.jpg
 
Anza na kiwanja kwanza ,Kama mtaa una usalama weka matirio taratibu

Wekeza kwanza kwenye kilimo na siyo mshahara wala duka wala posho za safari, vinginevyo hutajenga. Utaishia kufukuzwa kila kona kwenye hizi nyumba za kupanda maana kodi kila mwaka inapandishwa na wewe itabidi uwe unakurupuka kila msimu kukwepa kupanda kodi!
 
mkuu, kwenye kilimo?
 
Kujenga lazima ujikatae na uwe focus kwy lengo hilo na pengine moja la ziada kwa wkt huo!
Mkuu, nko focused, but si unajua mambo ya uchumi wa kati wa mama samia?! sasa nataka niende hivi hivi!
 
Back
Top Bottom