markbusega
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 826
- 848
bado najenga, nikimaliza nitasimulia. Nilianza hivi, kuanzia January mwaka 2018 hadi 2019 Desemba nilikuwa naweka akiba nikafikisha sh milioni 5, milioni 5 hiyo nilinunua kiwanja.
mwaka 2020 niliweka akiba ikafika milioni 2, nilimwaga mawe trip 19 saiti hapa ilinigharimu kama sh mil 1.3.
nikabakiwa na sh 700,000, nikawaza niweke Tofali hii hela? Au niendelee kuitunza kama akiba? kabla sijaamua cha kufanya, siku moja nimeenda site nilimtembelea jirani yangu kwenye kiwanja changu, yeye alikuwa anainua boma, nikamuuliza swali amepata wapi ujasiri wa kujenga nyumba kwa ramani yenye ukubwa ule? ( ilikuwa na vyumba vinne viwili self, jiko, sebule, dinning, study room, stoo n.k) akaniambia tofali ameweka watu wanafyatua ananunua tofali moja la udongo ambalo halijachomwa sh 100 anamlipa mpanga tanuri sh 50,000. mchoma tanuri sh 70,000 kwa njia hiyo imemuwezesha kufika hapo alipo. na Mimi "nikakopi nikaenda kupesti"
sikutunza hela tena kama akiba badala yake nikawa nagharamia uandaaji wa tofali, mwaka ule nikawa nimesogeza matofali ya kutosha ilinigharimu kama milioni 2.5, nikawa ninamawe, na Matofali site.
Kuanzia January 2021 hadi Mei nilifanikiwa kuweka akiba ya sh milioni 2, nilimtafuta fundi nikampa ramani akanijengea msingi kwa milion 1, fedha nyingine nilinunulia vifaa mbalimbali vya ujenzi kama saruji n.k. nikapatana naye tena fundi huyo kujenga boma kwa sh mil.1.2, kwa makubaliano yakumlipa kwa awamu. Kwa sasa nafunga linta/beam, nasogea taratibu huo ndio uzoefu wangu kwa kifupi