Mliofanikisha kujenga nyumba, Tupeane uzoefu hapa

Mkuu Asante sana, nimejifunza kitu kutoka kwako, naamini nitaleta mrejesho hapa JF!
 
Jukwaa la ujenzi lipo kwa ajili gani? Mods hamisha hii thread
 
Hongera sana kiongozi, hiyo spirit sio poa kabisa!!
 
Hongera sana kiongozi, hiyo spirit sio poa kabisa!!
Acha kabisa,
Kuziishi ndoto Ni mtihani Sana, hasa hasa Kama Ni mzee wa kujilipua.

Kujenga mfululizo hivyo kumeniyumbisha kibiashara,
maana balance nlokua nmebaki nayo nkijua ntazungusha angalau biashara iendelee kusurvive.

Nlkuja nkapata bahat mbaya nikapigwa matukio mawili, Moja la kuibiwa, jingine la kuunguliwa Moto dukan.

Yalinirudishaa nyuma Sana kibiashara, ukizingatia nyumba Zenyewe nlijenga kupangisha, Ela inarudi slow slow mno.

Mbili zimejaa,
ila Moja ya mwisho Bado Ni tupu tangu ilipojengwa wapangaj hamna.

Mpaka nafikiria ile pesa nilozika kujenga nyumba zote 3 zakupangisha Ni Bora ningejenga GUEST HOUSE Ningekua nakula elfu kumi kumi sahv.
 
Jinyime,epuka matumizi ya ovyo,punguza bata
Ili utimize lengo lako

Ova
Ukiwa unatembelea saiti Mara kwa Mara, matumizi yanajibalance yenyewe.

Kila senti unathamini maana ujenzi kwa asilimia kubwa unatembea kwa Ela ndogo ndogo.
Mf: kokoto buku, ubao elfu 10, misumari 1,500, maji 100 n.k
 
Ukiwa unatembelea saiti Mara kwa Mara, matumizi yanajibalance yenyewe.

Kila senti unathamini maana ujenzi kwa asilimia kubwa unatembea kwa Ela ndogo ndogo.
Mf: kokoto buku, ubao elfu 10, misumari 1,500, maji 100 n.k
Nlikuwa nawaambia watu hata ukiwa na 50000 au 100000 utaitumia kujenga nyumba
Ukiweka huko itasukuma kazi

Ova
 
Hongera sana kiongozi, hiyo spirit sio poa kabisa!!
Nilichokua nakifanya,
Ni kujenga Kwanza fense na kuweka geti.

Kisha kinachimbwa kisima Cha maji.

Kisha ndani ya uzio naweka contena la ft 40, Banda dogo la mabati la mlinzi na kujikinga mvua pamoja na mlinzi wa usiku tu kwa elfu 50 kwa mwezi.

Kisha kila nkipata Ela
naanza kununua material za JUMLA jumla najaza Kwenye contena.
Cement, rangi,nondo, bati za getting,flatbar,square pipes, fittings, Mbao, gypsum board&powder, tiles n.k

Material zikishajaa,
Naandaa chakula Cha mafundi Cha JUMLA mchele,MAHARAGE, mafuta vitunguu, kuni watatumia vipande vya mbao pale pale, na kiposho kidogo cha kubadilishia mboga.

Ela ya ufundi nayo haiumizi sana, maana wanakua Wanachukua kidogo kidogo TU baada ya sikU kadhaa.
 
mkuu, huna haja ya kujilaumu, nyumba ni asset
 
Mkuu wewe ni mpambanaji, nazidi kuifunza kwako
 
Nlikuwa nawaambia watu hata ukiwa na 50000 au 100000 utaitumia kujenga nyumba
Ukiweka huko itasukuma kazi

Ova
Kabisa,
Kuna v vikazi vidogo vidogo,
Vinahitaji Ela ndogo ndogo havipiwagi mahesabu mwanzoni ila unakutana navyo saiti na vinahitaji pesa ya lazima.

Ambapo utapaswa uweke watu wakusaidie.

Mf: kusogeza kifusi, kupanga vipande, kushusha cement, kuchota maji, kumwagilia sakafu/ukuta, bodaboda, kupachika madirisha, kukodi bomba za nguzo, kuchimba mtaro, kusogeza tofali, kung'oa visiki n.k
 
mkuu, huna haja ya kujilaumu, nyumba ni asset
Kweli mkuu,
Binafsi Hizi nyumba nazijenga Kama akiba ya wanangu.

Kimahesabu nmeziwekea malengo kua Ada zao za shule zitokane na Kodi za wapangaji ili zisinivurugie mzunguko was biashara yangu.

Na zote nimezipa majina ya wanangu Wote watatu,

Nafikiria Tena na wife tukipata mtoto mwingine tumjengee ya kwake nae Ada yake itoke palepale.

Yaan kila tukipata mtoto, tunaongeza na nyumba.

Huu ni mkakati wa familia yangu
 
Kosa kubwa sana ambalo watu wengi wanaojenga nyumba hulifanya ni kukosa mchanganuo halisi wa gharama za nyumba wanayotaka kujenga na namna watakavyoweza kuzikabili.

Kwa mfano, mtu ana kiwanja na mfukoni ana milioni 10 (hana uhakika wa kuendelea kupata kipato cha kujenga) , ghafla anakimbilia kuanza kujenga nyumba ambayo gharama zake zitahitaji sio chini ya milioni 30 ili kukamilika. Ataishia kwenye lenta na kuliacha gofu kwa zaidi ya miaka mitano bila kufanya chochote. Na hii sio sawa. Ni kujitesa. Angepaswa kuwaza tofauti kuhusu ujenzi.
 
Habari za jioni
Mimi nauliza hivi ukiwa na milioni 10 cash..
Labda ukanunua kiwanja kwa 2.5Mil.. ikabaki 7.5Milioni..
Unaweza ukajenga nyumba ya vyumba viwili( sebule na chumba) na choo Cha ndani, Arafu ukajenga na choo Cha nje Cha kawaida Cha wageni???
Ukapau Ila mabati ya kawaida
Ukapiga sakafu
Ukaweka willing nzima ya umeme
Ukaweka milango miwili ya grill na madirisha matatu ya grill.
Ukasakafia ukavuta na umeme
Gharama mpaka nyumba hiyo ya vyumba viwili kukamilika kutagharimu kiasi gani? Na Je hiyo 7.2M itatosha???
 
Mimi ningekupa hizi siri za kuweza kujenga nyumba.

1. Tamani kumiliki nyumba yako.
2. Pambana kumiliki kiwanja mahali unapopapenda.
3. Tafiti kujua gharama za chini kabisa kuweza kujenga nyumba tofauti tofauti.
4. Amua unataka kujenga nyumba ya gharama gani.
5. Weka malengo ya namna ya kuhimili hizo gharama mpaka kupata nyumba yako.
6. Fanya ujenzi kwa awamu lakini endelevu.
 
Haitoshi kwa mtazamo wangu
 
Kwa ninachokisoma hapa naona kujenga is next to impossible.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…