Mliofanikiwa kibiashara, mliwezaje kupambana na changamoto ya mtaji kukata/ kuisha?

Mliofanikiwa kibiashara, mliwezaje kupambana na changamoto ya mtaji kukata/ kuisha?

Mimi hapa huwa naloga...
Kuna mganga mmoja hvi anapatikana majimatitu kule bondeni wanapaita churwi..

Yule babu alinitibu sana kwanza anakupa dawa ya kutoa gundu ambayo ni maji ya gudu gudu .

Baada ya hapo anakupa dawa ya kuchoma na kuweka kwenye fremu yako ...
Hapo wateja watakua kama mchanga
Na mganga mwenyewe ndiyo mimi
 
Nakuombea hii thesis yako au research utatoboa🙏 Ntakachokwambia tu kila kitu kilianza na Wazo, I submit.
 
Vipi taasisi za mikopo ambazo hawanariba sana kama ASA nasikia haya makampuninya wahindi yanamambo yao ukikopa ili ufanye biashara haundelei ni kweli au nimahesaabu mabovu kuna aliyekopa microfinance au taasisi kama ASA,OYA akafanikiwa kibiashara alete ushuhuda? Samahani sibadili mada
 
Wakuu mambo vipi,

Hivi kwa wale ambao mmefanikiwa kwenye biashara zenu, hiki kiunzi cha kupambana na changamoto ya mtaji kukata mlikiruka vipi ndugu zangu. Ni njia gani mlizitumia ili na sisi ambao bado tunahangaika kuruka hiki kiunzi tuzitumie

Kuna muda unaona kabisa, nikifanikiwa kuvuka hapa, hakika haya maisha natoboa. Ila kadri unavyochelewa kukiruka ndivyo kiunzi kinazidi kuwa kikubwa, mbaya zaidi kwenye familia tunazotoka na jamii zinazotuzunguka hakuna wa kutupa msaada. Tunaishia kuumiza kichwa ni wapi tunakosea ila majibu hayapatikani.

Tafadhali ndugu zetu mliotutangulia, tunaomba mtupe ABC ili na sisi tuweze kujikwamua hapa tulipo.

Asanteni.
Unafanya biashara gani iliupewe maoni au ushauri mahususi.
 
Mtaji ni tatizo kwa biashara nyingi hasa ndogo ndogo muarubaini ni kujibana tu na kupunguza malengo ishi kulingana na kipato chako
 
Tafuta vitabu vinavyofundisha nidhamu ya pesa
 
Back
Top Bottom