Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

sisi sote tupo safarini mwenzetu amefika safari yake tupo nyuma yake one day tutaonana.
mkuu pole sana mungu akujaze moyo wa subira.
 
Mimi nilimpoteza mama mwaka 2020, nikampoteza mtoto mwaka 2021, mwaka huo huo 2021 mwezi uliofuata nikampoteza baba...haya mambo nikumuachia Mwenyezi Mungu tu na katika kipindi hicho kila jambo unaloliwaza kumbuka kwamba Mungu yupo na unazidi kumuomba yeye akupe uvumilivu na akuvushe salama...pia amini wazazi wapo mahali salama na siku Moja tutaonana katika heriiii ....

Pole sana kwa magumu unayopitia na Mwenyezi Mungu atakuvusha salama.
 
Pole sana.
 
Reactions: Ok9
Mkuu Mimi mama yangu alifariki akiwa na umri mdogo Sana yaani alikuwa na miaka 32 Mimi nikiwa na miaka 7 tu [emoji24][emoji24]
 
Ukijizuia kulia hutapona!!lia utoe uchungu ndugu!
Pole Sana kwa msiba huo mzito!

Umenikumbusha mama yangu alifariki nikiwa chuo mwaka wa tatu tukiwa kwenye mitihani ya semester ya mwisho,nilijikaza sikulia,kilichofuatia wiki moja mbele nilianza kulia,pona yangu ilikuwa ni kuhama nyumbani,lakini mpaka leo nikifika nyumbani lazima machozi yananilengalenga.
 
Miaka 17 imepita tangu mama yangu atoke duniani nakumbuka vizuri ulitoka ukiwa msaada mkubwa sana kwangu na ndio nilikuwa nakutegemea kwa kila kitu

Ni uchungu usiyoelezeka nakumbuka nililia sana kwenye ule msiba ila naamini upo sehemu salama nakupenda sana mama yangu na nilikupenda sana ata wewe ulijua ilo
 
Mishe zakufiwa zisikie tu kwa jirani! My parents gone when I was 5yrs! Alianza Dingi 1990 December,karibu na x-mass akafata Maza 1991 pia was karibu na pasaka! Hua nikiona mtu kazinguana na mzazi wake, hua nasema I wish angekua wangu,niite tu japo Mama au Baba! All in all now nipo na maisha yangu,tunasonga taratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…